MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,784
Huwa najiuliza sana lakini sipati majawabu, lakini naomba wasomi wa humu ndani mnisaidie.
Hivi Mzee Nyerere alikuwa ana roho ya namna gani kuona mambo kama haya yakitokea kwa wananchi lakini bado hataki kubadilika na akaendelea kutumia mkono wa chuma kuhakikisha anasigina kabisa uwezo binafsi wa mtanzania kuweza kujikwamua kiuchumi. Ujamaa wa Tanzania hakuleta matokeo yoyote makubwa na ya kuchangaza ukilinganisha na kule Asia na Ulaya ambako walau walifanya mapinduzi ya sayansi na teknolojia.
Uchina walifanikiwa sana baada ya Raisi Deng Xiaping kuanza kuwaonea huruma raia wake akifahamu kabisa kwamba njia waliyokuwa wanaenda ilikuwa siyo sahihi. Aliruhusu watu waanze kumiliki mali zao binafsi na kufanya biashara. Najiuliza sana, miaka yote 18 ya Ujamaa, yalifanyika na kutokea mambo mengi mno kwa watanzania, kiasi kwamba kiongozi yoyote mwenye huruma na wananchi ni lazima angekaa chini na kujifanyia tathmini, lakini Raisi Nyerere hakufanya hivyo, aliendelea kuwa na moyo mgumu kama Farao. Hebu tuzingatie haya:
1. Sera ya utaifishaji wa mali, ilileta umasikini mkubwa sana kwa watu.
2. Kufuta vikundi ya ushirika (Cooperatives) na kuweka vile vya TANU kulididimiza mno sekta ya kilimo.
3. Kupiga marufuku watu binafsi kuagiza bidhaa nje ya Tanzania kulipelekea uhaba wa bidhaa na huduma muhimu.
4. Kuweka ugumu katika kusafiri (Travelling Restrictions) kulisababisha ukosefu wa ujuzi kwa watanzania.
5. Kuminya uhuru wa mawazo na kutumia nguvu ya dola kunyamazisha watu kulidumaza ukomavi wa demokrasia.
Mpaka kufika miaka ya 80's Ujamaa ulikuwa umefeli vibaya mno. Tanzania tulikuwa hatuna hata unga wa kupikia, mafuta, wala sukari. Mtaa mzima mlikuwa mnaenda kwa mwenyekiti kuomba sukari au sabuni kutoka maduka ya ushirika. Ukikamatwa na mafuta, sabuni au dawa za binadamu zilizolanguliwa kutoka Kenya lazima ushughulikiwe na dola. Kama ulisoma miaka ya 80's unaweza kukumbuka kwamba hata sare za shule zilikosa rangi, watu tukawa tunavaa vitu vya ajabu vilivyochakaa kama vile vichaa. Ukibahatika kukutana na wamishionari au taasisi za kidini ndiyo ulikuwa unaweza kupewa hata nguo, mahitaji na wazungu.
Yote haya yanafanyika, Mzee Nyerere na Sokoine wakaingia mtaani kuanza kushughulikia maelfu ya watanzania ambao wanahujumu uchumi. Ila ukifuatilia zile kesi nyingi, utafahamu kwamba hao wahujumu uchumi ni wale watanzania wenye akili za haraka ambao walijiongeza na kuweza kupata mahitaji muhimu ili kuhudumia familia zao. Wahujumu uchumi kwelikweli, ambao wengi walikuwa ni vigogo wa serikalini hawakuguswa. Kiukweli, kama nchi ina kiongozi mwenye huruma haya yote yasingetokea bila yeye kujirudi.
Hivi kwanini MTAKATIFU na MWENYEHERI, Raisi Nyerere hakuwa na chembe ya huruma moyoni ?
Kuna mambo nikikumbuka huwa naumia sana na nakosa majawabu. Hivi alikuwa anapenda kutuona sisi vile ?