Dar_Millionaire
JF-Expert Member
- Aug 6, 2008
- 227
- 85
Wadau wa JF,
Kuna hii stori nilipata kuisikia kitambo ila sikuweza kufuatilia ukweli wake. Kwa mnaojua undani wake (kama ni kweli au la) naomba michango yenu.
Stori yenyewe ni kwamba baada ya Nyerere kutangaza sera ya Ujamaa huku dunia ikiwa imegawanyika kati ya ubepari na ukomunisti, upande wa ubepari (hususani kinara wao Marekani na mchumba wao Uingereza) walikuwa na shauku ya kujua "Ujamaa" ni kitu gani.
Inasemekana jibu walilopata toka kwa Nyerere ni kwamba Ujamaa sio tafsiri ya moja kwa moja ya ukomunisti kama ambavyo walikuwa wanadhania. Bali ni sera inayolenga kuunganisha jamii kwa kuzingatia utamaduni wa asili wa kushirikiana uliokuwepo miongoni mwa Waafrika. Kwamba lengo sio kuiga sera za nje za kiuchumi bali kujenga nguvu za kiuchumi kwa kuzingatia utamaduni na mazoea tuliyokuwa nayo waafrika hata kabla ya ukoloni.
Inasemekana Wamarekani na Waingereza baina yao walikiri kwamba Nyerere alikuwa amepatia kwa kuzingatia utamaduni na asili za watu katika kutengeneza sera ya kiuchumi. Kwa upande mwingine inasemekana waliona kuwa mafanikio ya sera yake mpya (ambayo walihisi ingefanikiwa) yangesababisha nchi zingine za Afrika kuiga mfumo wa Tanzania na hivyo kutengeneza muungano wa kiafrika ambao wao hawakupenda utokee.
Hivyo inasemekana CIA walitoa classified memo kwenda M16 ikiwa na agizo moja kuu kwamba M16 wahakikishe Nyerere hafanikiwi.
Mdau aliyenipa hii stori anadai memo hiyo iligundulika hivi karibuni baada ya kuexpire muda wake toka kwenye classified materials.
Binafsi ningependa kupata resources za kuthibitisha kama hii stori ni kweli au sio kweli. Wenye data naomba tuhabarishane.
//DM