Kweli wewe ni tahira unajiuliza na kujijibu mwenyewe.
Umekazana mabeho mabeho,
Hata mabeyo tu kuandika huwezi.
Hizo habari zako za niamini mimi peleka kwenye vijiwe vyako vya kahawa
Ohoo sorry. Kumbe anaitwa Mabeyo? Lakini nadhani ujumbe umeupata pamoja na utaahira wangu. Alipelekwa Nairobi na walitumia uwanja wa Wilson airport. Madaktari wakajaribu lakini hawakufanikiwa, akarudishwa akiwa kwenye hali mbaya na kufia Mzena.
 
Nafuatilia Clip Mimi...Angejua hali asingeendelea na yake mpaka mwenzake anakata roho...Kama Kuna mambo ya muhimu kumkabidhi ambayo hayakuwa documented je? Kwani Katiba inasemaje? Nani anakuwa Rais kama aliyepo hawezi majukumu? Kwanini basi hakuwepo hapo wakati huyu ameshindwa majukumu?
Ndiyo maana ni vigumu sana kuamini kwamba hawakuwa wakifahamu kinachoendelea.

Halafu na vile mitandao ya kijamii ilivyokuwa imejam kwa taarifa kibao za taharuki! No way!
 
Kumbe mtaala wa kujifunzia lazima autunge mwanafunzi mwenyewe?

Kwa nini tusijifunze kutokana na uzoefu wa wengine?

^Why isn't you seatbelt on?^

^'Cause I never had an accident.^

Halafu kule kwenye anga za CJ wanasema ^Tumetoa adhabu kali ili iwe funzo kwa...^

Katiba na sheria zao, uzoefu wa utawala, Marekani ni tofauti na Tanzania.

Tanzania waganga njaa wengi sana. Wengine walihudumu nafasi za juu kabisa, ila hawajakubali kuwa ni wastaafu na wakae pembeni.

Kila siku ni kupenyeza hila na majungu waendelee kula kwa upole
 
Ahukumiwe inavyostahili! Bahati mbaya, alikufa bila kuomba msamaha kwa baba wa Ben Saa Nane, Tundu Lissu na wengine wengi aliowapoteza, aliowaua wakitembea na aliowatesa sanaaa!

Na huyu bwana anatunga hadithi tuuu, hakuwepo!
 
Nadhani ilikuwa sahihi asipewe kwanza hizo taarifa za kifo Cha Raisi Makamu wa Raisi taarifa.Kwa kawaida kama keep kikao hata Cha uchaguzi wajumbe wanataka kumjadili mgombea ni kawaida kumtaka mgombea atoke Nchi wajumbe wamjadili bila yeye kuwepo.Sasa Makamu wa Raisi ndie mrithi wa kiti Cha Uraisi .Ilibidi mambo mengi ya kuhusu kurithi kiti ,taratibu za kuapishwa Kwake nk zijadiliwe na kupangwa tayari ili akitaarifiwa kifo Cha Raisi Kila kiti kiwe kimejadiliwa na kimepangika vizuri

Hebu fikiria anapewa taarifa halafu anakuwa sehemu ya mjadala Wengine Wanasema asiapishwe apewe mwingine mbele yake ni very embarrassing.Heri mivitano yoyote ilikuwa huko ndani bila kumhusisha Makamu wa Raisi ingeleta shida mfano mama angegoma kuwa sitaki kama Hali ni hii Nchi ingeingia kwenye mgogoro mkubwa wa kikatiba nk

Nilichoona kwenye Haya mahojiano inaonyesha yalikuweko mambo mengi muda mchache kuyaongea CDF ila Jeshi lilisimama kidete kuhakikisha mwishowe katiba inazingatiwa japo Kwa kuchelewa kinyume na masaa 24 ya katiba Inavyotaka

Yote heri tushukuru Mungu Nchi ilivuka salama
Muhimili huwa ni mitatu(Serikali,Bunge na Mahakama)Je? Muhimili wa Mahakama ukisaulika katika mtiririko wote wa ushauri ,ina maana muhimili wa Mahakama Viongozi wa Juu wanaupuuza?!!!
 
Naweza kuwa mimi ndiye Mabeho nimekuja anonymously! Una ushahidi gani kuwa mimi siyo yeye? Mabeho anaweza kuwa ndiye rafiki aliyeniambia. Una ushahidi kuwa sivyo? Mabeho anaweza kuwa anasema ukweli nusu. Una ushahidi gani yote anayosema ni ukweli? Mabeho anaweza akawa hakuwepo muda wote! Mabeho anaweza kuwa anadanganya kama waziri mkuu alivyodanganya Magufuli ni mzima na anachapa kazi!
Ukweli ni kwamba story yako ni ya kutunga tu ndo maana unakosea ata kuandika jina la muhisika. Hongera ata hivyo kwa unayoaminiswa na baadhi yetu tupe hongera kwa kuaminiswa na mabeyo. Yote kwa yote ni uhakika mimi na wewe hatukuwepo karibu hivyo tunapokea story kama zinavyokuja
 
Hakika suala la kifo ni fumbo sana sana sana sana

Ukibahatika kufa mbele za watu Mwombe Mungu

Leo hii tumepata simulizi nzuri ya EX CDF kumbe magufuli wakati anakufa hakuwa mikononi mwa mtoto wake,Mkewe wala ndugu yoyote ili ni kwa sababu ya cheo chake lakini hata mke hakurusiwa kuwa pale kumuuguzia mumewe?

Wewe ulie na ndoa kumbe usiringe yawezekana siku unakufa hata mkeo hatokuwa karibu na wewe wala watoto ulio wazaa

Aise
Bora maisha ya upadri fundisho kubwa

Simulizi ya CDF ipo wazi

Magufuli alipata nafasi ya kutubu dhambi zake zake kupitia Baba paroko na Kadinari pengo ili ni daraja la pekee sana sio wote ulipata

Magufuli alitaka akafie nyumbani kwake bira shaka hakupendezwa kuuguzwa paspo mkewe kuwa pale au watoto wake

Magufuli alitaka kujiua kwa kutaka kutolewa hosptali akafie kwake hii ni roho ya mauti uwa inamsumbua kila mmoja anae karbia kufariki uwa anachaguo lake.

Mwisho kwa uhakika

Magufuli kwa simulizi ya ex cdf yupo mbinguni

Je mlio kuwa karibu na Nyerere,Mkapa na Mwinyi Nini kilijili ili sisi tujipange kukutana nao either mbinguni hama motoni?
 
Muda Sasa wa kujaribu kuipunguza maneno ya kiarabu kwenye mifumo yetu ya utawala " Nimetafakari Sana " neno AMIRAT na AMIR na nikiangalia vile vikundi vyenye itikadi Kali navyo vinatumika maneno hayo
 
Katiba na sheria zao, uzoefu wa utawala, Marekani ni tofauti na Tanzania.

Tanzania waganga njaa wengi sana. Wengine walihudumu nafasi za juu kabisa, ila hawajakubali kuwa ni wastaafu na wakae pembeni.

Kila siku ni kupenyeza hila na majungu waendelee kula kwa upole
Basi tatizo siyo kukosa uzoefu, bali kukosa weledi.

Nakuhakikishia hata tungekuwa na uzoefu kuliko Marekani, hali ingekuwa ileile.

Angalia mfano wa majanga: kuzama kwa meli, ndege kuanguka, ukame, njaa na majanga mengine ya asili kama mafuriko na matetemeko.

Tumejifunza kitu chochote kama taifa au kila tukio linatushtukiza sie ni kama wageni?
 
Hivi mnaamini hizo porojo anazosema Mabeho? Kwanza Magufuli hakufariki huo muda anaosema. Pili Magufuli alipelekwa Nairobi na ndiyo maana alikuwa anasema nirudisheni nikafie nyumbani. Ni kweli walimrudisha na akaja kufia Mzena. Tatu, suala la kuapishwa lilicheleweshwa kwa sababu ya mvutano wa kutaka Samia asiapishwe. Kwa kifupi amezungumza ukweli nusu.
Namim ndio nilivyoelewa
Naunga mkono hoja
 
Chozi la Mabeyo linaungana na machozi ya maelfu ya watanzania waliolia na wanao endelea kulia kutokana na madhira waliyo yapata wakati ule wa mtu yule.
Kwa uchache tu nawakumbuka watumishi 12 Elfu walio ondolewa kazini kwa kuwa eti walifoji vyeti.
Wengine walikuwa wamefanya kazi zaidi ya miaka 20...!
Hivi kweli unaona ni sahihi mtu kufoji cheti Ili apate ajira na baada ya kubainika na kuthibitishwa kuwa amefoji aachwe aendelee na kazi? Mimi nina mashaka na uwezo wako wa kufikiria
 
Binafsi siioni maajabu general Mabeyo kulia. Watu wanaleta stori za uaskari. Hivi ni wapi mwanajeshi alisomea ukakamavu wa kutolia akiumizwa au kukuguswa na jambo la kusikitisha au kufurahisha. Hapa ndo huwa tunaona watu hasa wa tz wanavyokuwa waoga kutetea haki zao mbele ya askari kwa kudhani askari huyo yeye kaumbwa tofauti na yeye au ana moyo wa chuma. Huyu ni mwanadamu km wewe isipokuwa yeye kaongezewa tu somo la ukakamavu na ujasiri kitu ambacho hata raia kibao tu wanacho hasa wakazi wa mkoa wa Mara, Wamasai nk. Nafikiri hivi karibuni tulishuhudia Wamasai Zanzibar wakiwatia bakora askari wa Zanzibar hadi kukimbia.

Askari nao wana hisia, mzuka, nk. Hakuna mbabe wa hivyo vitu. Ni sawa na kusema general hawezi kuhisi njaa, kitu ambacho siyo kweli, maana hakuna baunsa wa njaa.

Mtu hulia hata kwenye msiba usiomhusu, wakati unaomhusu anaweza kujikaza. Kwa hiyo mazingira huamua hisia za mtu atende nini. Hivyo mtu kulia sababu ya huzuni au furaha husababishwa na factors nyingi, wengine hulia kwa kuvuta kumbukumbu ya matukio ya nyuma yaliyomkuta na kumuumiza, ndo maana mwingine anaweza kulia hadharani sababu ya mapenzi na mwingine asilie. Tena mwingine akavalishwa tu pete akalia tena mbele ya umati wa watu.

So, kulia kwa general publicly is not a big deal, a big deal is why is he crying repeatedly. Alilia siku ya mazishi lakini nashangaa hadi kwenye kumbukizi.
Mleta mada kauliza swali juu (title yenyewe ni poser) kwa alichoona na kutafsiri yeye? Hakuna hitimisho rasmi.

Nchi nyingi duniani wananchi wameaminishwa army generals sio watu wa kutoa matone kirahisi au kuwa too emotional mbele ya public. Sasa kama huo ndio ukweli wa jeshi au ni myth tu, mimi sijui ndio maana nimeuliza.

Mwisho lengo halisi la mada baada ya kuona marehemu kama vile jamii aimpi airtime anayostahili siku ya leo nilipokutana na hiyo interview nikahisi nikiweka JF inaweza leta mjadala labda na angle tofauti. Hilo ndio lilikuwa kusudio apate airtime tu.

Otherwise nothing personal kwa mtu yeyote raisi aliyepo, retired CDF na CCM kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom