Chonde chonde Rais Samia, wakulima hatutaki kurudi tena kuuza mahindi kilo 200, nasi tutakuja huko mjini

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,836
Habarini wadau,

Nimeona watu mtandaoni wakilalamika kuwa serikali ifunge mipaka ili wakulima tukose sako, na mazao yetu yashuke bei.

Namuomba Rais asikubali na hii hoja, sababu hivi sasa wakulima tunauza mahindi kilo 500 hadi 600 huku shambani.

Huko mjini unga nasikia haujashuka bei, kama Dar kilo moja nasikia bado ni 2000, lakini hili siyo kwa sababu wakulima tunauza ghali, ni kutokana na matatizo kwenye supply chain zetu au sijui ni nini.

Kufunga mipaka kutafanya mahindi yetu turudi kuuza tena 200 au 300 kitu ambacho kitatuumiza wengi wakati gharama za maisha kila kitu kimepanda, hatutaweza kuendesha maisha kwa kilimo, tutahamia mjini.
 
Mkulima au dalali?
Kilimo kinamfaidisha sana Dalali kuliko Mkulima...dalali anaweza kukutia umaskini hivi hivi unaona
 
Hoja yako imenikumbusha topic niliyojifunza juzi kati inayohusu ' Neo - liberalism'.

Anyways: Katika hili nadhani tungekuwa na serious governace, ilitakiwa Serikali itoe subsdies kwa wakulima ili baadhi ya gharama za kilimo zibebwe na kodi za wananchi kupitia Serikali. Hali itakayopelekea wakulima kutumia gharama kidogo. Consequently, bei ya mazao ingeweza kushuka.

Jambo lingine ni namna ambavyo mamlaka ingeona jinsi ya kupambana na madalali hapo kwenye chain ya biashara ya mazao maana hao madalali kwa ufahamu wangu nadhani wana impact kubwa sana kwenye suala la bei ya mwisho ya mlaji.

Kuhusu suala la kufunga mipaka, hilo nalo ni la kitaalamu zaidi. Maana Serikali inatakiwa ijue uwezo wa wakulima, demand ya soko la ndani na kiasi gani kinaweza uzwa nje. Naomba nisiingia ndani zaidi kwa hatua ya sasa.

Ahsante mtoa mada maana umenirejesha darasani kidogo.
 
Mkulima mwenzangu usiwe na wasiwasi, kwasbb Bashe amelisemea jambo hili zaidi ya mara 4 kwamba mahindi ya wakulima siyo mali ya umma. Hivyo serikali haina mamlaka ya kuwaamulia wakulima wapi wauze mazao yao.

Haya makelele ya mtandaoni yanapogwa na wadangaji, wanaobeti, wacheza pool, machinga, wapiga debe na mapanya road. Haya majitu kamwe hayatasikilizwa na serikali ya mama yetu mtulivu wa maamuzi Dr. Samia Suluhu Hassan.
 
Mkulima au dalali?
Kilimo kinamfaidisha sana Dalali kuliko Mkulima...dalali anaweza kukutia umaskini hivi hivi unaona
Dalali hana cha kupoteza, yauzwe nje au la bado atapata commission yake ile ile
 
Back
Top Bottom