Njombe: Rais Samia Awahutubia Wananchi Katika Mkutano wa Hadhara, Asema Serikali Imezuia Kupandisha Hadhi na Kukata Maeneo ya Utawala

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
1,678
9,609
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa Njombe katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Sabasaba Njombe Mjini, leo tarehe 10 Agosti, 2022.DKT. PINDI CHANA – WAZIRI, MALIASILI NA UTALII

Kwa niaba ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwakweli tunakushukuru sana kwa vision kubwa ambayo umekuja nayo – The Royal Tour.

- Royal Tour imefungua Nchi
Mh. Rais, kupitia program hii, leo hii Tanzania imefunguka. Tunapata wageni kutoka mataifa mbalimbali, kutoka mabara yote duniani. Wageni hawa wanapokuja Tanzania siyo tu kwakuwa Tanzania ipo kwenye ramani, lakini pia suala la uongozi bora, siasa safi na political stability chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Zipo nchi zingetamani sana kupata wageni kama Tanzania lakini wakiangalia nchi hizo hazijatulia kwa mapigano, hazijatulia kisiasa – hata ukisema wageni waje inakuwa si rahisi…

- Utalii wapanda Nyanda za Juu Kusini
Tunapozungumzia utalii Mh. Rais, upande huu wa Southern Circuit (Nyanda za Juu Kusini) watalii hawa wanafika. Takwimu zinaonesha Ruaha National Park watalii wametoka takribani 9000 mpaka 13000. Hapo vipi? Upande wa Kitulo watalii sasa hivi hawapungui 1200.

- Mipaka ya Hifadhi
Kuhusu Mipaka ya Hifadhi hili tunaendelea nalo chini ya Kamati ya Mawaziri 8 kuhakikisha kwamba maeneo yote ya hifadhi yapo salama na pale Kitulo tumetoa maelekezo kwamba wataalamu wanakwenda kuweka mambo sawa ikiwa ni pamoja na maendeo ya Kipanga Kipengele.

Royal Tour imeongeza masoko ya bidhaa zetu za vyakula iwe ni parachichi, ngano. Wageni hawa Wazungu kwa siku wanakula mara tatu – wanakula vizuri. Kwahiyo Royal Tour imeongeza thamani katika bidhaa zetu.

HUSSEIN BASHE – WAZIRI WA KILIMO

Mkoa wa Njombe unazalisha sana zao la chai. Mkoa huu unazalisha kiwango kikubwa cha zao la parachichi pamoja na mahindi.

- Mapitio ya Mfumo wa Bei ya Chai
Mh. Rais, Chai ni moja kati ya mazao ambayo yalipata msukosuko. Nataka niwaambie wakulima wa chai wa mkoa wa Njombe Mwenyezi Mungu akitupa uhai, tutakutana hapa Njombe na wanunuzi wote wa Chai ili kupitia upya mfumo wa bei ya chai. Na sababu zipo. Sababu kuwa ni mbili: Serikali inatoa ruzuku ya mbolea. Maana yake estate zote na wanunuzi wote wa chai watakuwa sehemu ya wanufaika wa bei ya ruzuku, kwahiyo gharama za uzalishaji zitapungua.

-Mnada wa Chai Kufanyika Tanzania
La pili Mh. Rais, chai yetu imekuwa ikiuzwa kupitia mnada wa Mombasa. Serikali ya Awamu ya Sita tukishirikiana na kampuni ya Mtanzania inayoitwa Bravo – kwasabatu mfumo wa uuzaji wa chai duniani kote unakuwa ni public na private partnership – tunaanzisha mnada wa chai Dar es Salaam na sasa hivi ma-godown yameshaanza kuandaliwa, mfumo wa kuuza chai umeanza. Ninataka niwaambie wanunuzi kuwa mikataba yote ya kuuza chai itasajiliwa katika soko la chai la Tanzania ili tuweze kujua bei halisi ya chai inayouzwa nje ili tuangalie bei anayoipata mkulima siku ya mwisho.

- Ruzuku ya Mbolea
Tarehe 8 umezindua skimu ya kutoa ruzuku ya mbolea. Hapa Njombe kuna mawakala wengi wa mbolea. Nataka nitumiwe nafasi hii niwaambie mawakala kuwa bei ya mbolea iliyozinduliwa na Mh. Rais na ambayo itatangazwa kwa kupitia magazeti na televisheni, itakayoanza tarehe 15 mwezi wa 8. Bei hiyo ni moja kuanzia Dar es Salaam mpaka mwisho wa Tanzania ikiwa kijijini au mjini.

HAMAD MASAUNI – WAZIRI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI

Ukiangalia nyumba wanazoishi askari wetu, inasikitisha. Ukiangalia hata wananchi wakitaka kupata huduma vituo vya polisi havipatikani au vipo katika hali mbaya. Hapa Njombe ninyi ni mashahidi. Hata jingo la makao makuu ya Polisi ya mkoa hayakuwepo. Sasa hivi linajengwa ghorofa kama five-sta hotel, linaendelea kukamilika.

- Mpango Kabambe wa Vituo vya Polisi/Nyumba za Askari
Nilisema juzi Njombe, sitaki kuona haya malalamiko wabunge wakija kila siku Bungeni wanazungumzia masuala ya vituo vya polisi, masuala ya makazi ya askari. Kwanini tusiwe na mpango ambaoutakuwa ni mpango utakaosaidia kupatia ufumbuzi wa kudumu changamoto za askari wetu – si polisi peke yake, askari wa vyombo vyote.

Na ndipo tukaja na mpango kabambe wa kujenga vituo vya polisi na makazi ya askari zaidi ya 51,780 nchi nzima kwa kipindi cha miaka 10. Na hapa Njombe tumeona matunda yake. Wanging'ombe kuna kituo cha class 1 kabisa. Zaidi ya milioni 900 zimetumika. Mpango wetu umeanzia Njombe.

Nina hakika, kwa namna ninavyomuamini Rais, utakamilika kabla ya miaka 10.

UMMY MWALIMU – WAZIRI WA AFYA

- Afya za Wananjombe

Nianze kwa kuwapongeza wana-Njombe kwa kulinda na kuzitunza afya zao. Nikiangalia viashiria vikuu vya afya kwa mkoa wa Njombe kwakweli wanakwenda vizuri. Hongereni!

Bado tunahitaji vituo vya afya katika vijiji, baadhi ya kata lakini kwa kiasi kikubwa umetekeleza uliyoyaahidi kwa watu wa Njombe.

- Lugha na Kauli Zetu kwa Wananchi
Deni ambalo limebaki ni watumishi wenzangu wa afya tunayo madeni mawili makubwa kwa Rais Samian a Watanzania. La kwanza ni kuhakikisha tunatoa huduma bora za afya na siyo bora huduma. Mwananchi akija katika kituo cha kutoa huduma za afya, iwe ni zahanati, kituo cha afya au hospitali – lugha zetu na kauli zetu ziwe ni za upendo, huruma na za kutibu. Hili lazima tuhakikishe tunalifanyia kazi.

La pili, ubora wa huduma; tunazungumzia upatikanaji wa dawa pamoja na vipimo.

La tatu, tunazungumzia muda ambao mwananchi atafika kuptata huduma. Mh. Rais, hili tunataka kuahidi kwamba tutalisimamia.

- Kupunguza Gharama za Matibabu
Jambo lingine ambalo tuna deni kwako Mh. Rais na Watanzania ni kupunguza gharama za kupata matibabu nchini Tanzania. Mh. Rais, kama ulivyofanya kwenye mbolea na mambo mengine, sisis pia sekta ya afya tumeona tunao wajibu wa kuwapunguzia mzigo Watanzania kwa kulipa fedha nyingi kwa ajili ya kupata huduma katika hospitali zetu.

Jana nilieleza, hivi kumuona tu Daktari unalipa Tshs. 15,000 ni kwasababu gani? Mh. Rais, timu yangu tayari inafanya tathmini, tutashusha gharama za kumuona daktari ili tuweze kuwapunguzia mzigo Watanzania kama ulivyotuelekeza kwasababu afya siyo biashara, afya ni huduma.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Nimefarijika zaidi na tamko la Mkuu wa Mkoa (Anthony Mtaka), mgeni ana wiki sasa lakini ameivaa Njombe kama amekuwepo siku zote. Nimefarijika na tamko lao kuwa kwa nilichokiona kwenye ziara yangu hii, nikija tena nitakuta mara nne, mara tano zaidi ya nilichokiona. Hilo limenipa faraja na niwaombe wana-Njombe mtoe ushirikiano mkubwa kwa uongozi wa mkoa na wilaya zenu ili mambo yaende kuwa mazuri zaidi.

- Ukusanyaji wa Mapato
Jengine ninaloshukuru katika mkoa huu ni ukusanyaji wa mapato; mmekusanya vizuri sana. Niwashukuru sana ma-DED, mmefanya kazi nzuri sana. Lakini niseme kuna uwezekano wa kukusanya zaidi na zaidi. Naomba sana ongezeni juhudi tuweze kukusanya mapato kwa ajili ya maendeleo.

Kwa siku nilizokuwepo hapa nimetembelea majimbo yote isipokuwa Ludewa, na niwaahidi ndugu zangu wa Ludewa. Nitakapokuja kwa ufunguzi wa miradi niliyowekamawe ya msingi, nitakuja Ludewa na mtanifaidi kwasababu nitakuwa na muda wa kutosha.

- Chekechea Sokoni
Kuhusu soko, nimetoa maagizo pale. Akina mama wale wanaoshinda na watoto mgongoni, basi muwawekee chekechea ya kulea watoto wakati wao wanafanya kazi ya ijasiriamali.

Pamoja na hayo, kuna maombi yametolewa nikiwa ziarani hapa na ningependa niyazungumze.

- Zuio la Kukata na Kupandisha Hadhi Maeneo ya Kiutawala
Kuhusu Njombe Kuwa Manispaa
Nadhani jawabu viongozi wanalifahamu lakini nataka niseme kwamba tumezuia kukata maeneo yote ya utawala – yote! Na kila ninpopita Tanzania watu wanaomba kukatiwa maeneo ya utawala au kupandishwa hadhi. Lakini kwa hali yetu ya uchumi na mzigo mkubwa kwa wananchi unaotukabili, tumezuia kupandisha hadhi au kukata maeneo ya utawala. Kufanya hivyo ni kuongeza gharama za uendeshaji kwa Serikali. Kwa sasa tuende hivi tulivyo, mwelekeo ni wananchi…

La pili, jana nilipozungumza na wazee niliombwa ulezi wa Mkoa wa Njombe.

- Ulezi wa Mkoa wa Njombe
Sasa hili nataka niseme kwamba ulezi upo wa aina mbili. Kwenye chama chetu cha Mapinduzi tumeweka walezi kila mkoa. Na kwa mkoa huu, ndugu yetu Hawasi ndiyo mlezi wa CCM. Lakini kwa upande wa Serikali hatuna utaratibu wa walezi isipokuwa Rais ni mlezi wa Tanzania yote. Ni mlezi wa mikoa yote.

Hivyo, si kwamba nakataa kuilea Njombe, hapana. Nitakuwa napendelea mtoto mmoja katika watoto 26. Nataka niwapende watoto wangu wote 26. Hilo ndiyo jawabu langu kwenye ulezi wa mkoa.

- Ujenzi wa Chuo Kikuu Njombe
Kuhusu kuwa na Chuo Kikuu katika mkoa wa Njombe, tuna mpango tunaouita HET. Mradi huu unaruhusu vyuo kuweka matawi yao katika mikoa. Tutakwenda kuangalia kwenye mradi huu kama bado kuna nafasi ya Chuo Kikuu chochote kuweka tawi hapa. Kama mradi umebana, tutaangalia maeneo mengine lakini mradi huu uwe na tawi angalau na tawi la chuo kimoja.
 

Binti 1

Member
Dec 1, 2018
8
51
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kwamba kwa sasa serikali imezuia kukata maeneo ya kiutawala.

Ameyasema hayo leo akiwa ziarani mkoani Njombe kutokana na maombi mbalimbali ambayo yamekuwa yakitolewa katika maeneo mbalimbali ya kutaka maeneo kupandishwa hadhi au kutaka kuwa manispaa.

Rais Samia ameongeza kuwa serikali imezuia kukata maeneo yote ya utawala kwa sasa kwa sababu kufanya hivyo kutaongeza gharama za uendeshaji.
 

Statistics

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
2,324
4,181
Halmashauri za jiji, manispaa na miji wapokonywe landkruza, hata ist zinawatosha. Kruza wabakiziwe wa vijijn tu. Ataokoa zaid ya mabilion.

Apunguze majimbo yawe mawili kila mkoa

Mawaziri wasiwe wabunge.

Afute cheo za mkurugenz wa halmashaur, majukum yake das anayaweza.

Awafute kaz maafisa wa trafiki, na hicho kitengo kiwa ndan ya tra ili wakusanye masuruf ya gavoo.

Afute cheo cha makam wa rais, na wazs mkuu. Majukum yao yafanywe na katibu mkuu kiongoz.

Aifumuo tamisemi, vitengo vyao virud wizara mama.
 

kunena

JF-Expert Member
Nov 29, 2016
473
632
Halmashauri za jiji, manispaa na miji wapokonywe landkruza, hata ist zinawatosha. Kruza wabakiziwe wa vijijn tu. Ataokoa zaid ya mabilion.

Apunguze majimbo yawe mawili kila mkoa

Mawaziri wasiwe wabunge.

Afute cheo za mkurugenz wa halmashaur, majukum yake das anayaweza.

Awafute kaz maafisa wa trafiki, na hicho kitengo kiwa ndan ya tra ili wakusanye masuruf ya gavoo.

Afute cheo cha makam wa rais, na wazs mkuu. Majukum yao yafanywe na katibu mkuu kiongoz.

Aifumuo tamisemi, vitengo vyao virud wizara mama.

Hivi unafahamu kazi ya kichwa sio kizibo cha shingo bali kina kazi ya kufikiria?
 

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,627
14,026
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kwamba kwa sasa serikali imezuia kukata maeneo ya kiutawala kwa sasa.

Ameyasema hayo leo akiwa ziarani mkoani Njombe ambapo amesema kutokana na maombi kmbalimbali ambayo yamekuwa yakitolewa katika maeneo mbalimbali ya kutaka maeneo kupandishwa hadhi au kutaka kuwa manispaa.
Rais Samia ameongeza kuwa serikali imezuia kukata maeneo yote ya utawala kwa sasa kwa sababu kufanya hivyo kutaongeza za uendeshaji
Tunataka Manispaa sio kukata maeneo..

Njombe kuwa Manispaa hakuna kitu Kipya kitaogezeka in terms of administration isipokuwa stahiki za hadhi ya Manispaa..

Seems haelewi kinachozungumzwa,kukata maeneo mapya na kupandisha hadhi Miji midogo kuwa Halmashauri ndio kunaongeza gharama ila sio kuitoa TC kuwa MC.
 

All truth23

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
422
430
Halmashauri za jiji, manispaa na miji wapokonywe landkruza, hata ist zinawatosha. Kruza wabakiziwe wa vijijn tu. Ataokoa zaid ya mabilion.

Apunguze majimbo yawe mawili kila mkoa

Mawaziri wasiwe wabunge.

Afute cheo za mkurugenz wa halmashaur, majukum yake das anayaweza.

Awafute kaz maafisa wa trafiki, na hicho kitengo kiwa ndan ya tra ili wakusanye masuruf ya gavoo.

Afute cheo cha makam wa rais, na wazs mkuu. Majukum yao yafanywe na katibu mkuu kiongoz.

Aifumuo tamisemi, vitengo vyao virud wizara mama.
Acha wivu kwa wenzio

Ungekuwa wewe unapanda hayo magari ya Kluza usengesema hayo
 

Bemendazole

JF-Expert Member
Nov 14, 2020
1,397
3,305
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kwamba kwa sasa serikali imezuia kukata maeneo ya kiutawala.

Ameyasema hayo leo akiwa ziarani mkoani Njombe kutokana na maombi mbalimbali ambayo yamekuwa yakitolewa katika maeneo mbalimbali ya kutaka maeneo kupandishwa hadhi au kutaka kuwa manispaa.

Rais Samia ameongeza kuwa serikali imezuia kukata maeneo yote ya utawala kwa sasa kwa sababu kufanya hivyo kutaongeza gharama za uendeshaji.
Chonde chonde mama Teresa ops! Mama Samia. Ikikupendeza naomba uniteue kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Chanika- Dar Es Salaam.
Sina makuu mie (ctak steless), nataka nikawatumikie majirani zangu wa Chanika... 😎😎😎
 

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,131
688
Tunataka Manispaa sio kukata maeneo..

Njombe kuwa Manispaa hakuna kitu Kipya kitaogezeka in terms of administration isipokuwa stahiki za hadhi ya Manispaa..

Seems haelewi kinachozungumzwa,kukata maeneo mapya na kupandisha hadhi Miji midogo kuwa Halmashauri ndio kunaongeza gharama ila sio kuitoa TC kuwa MC.
Hili ni jambo la maana sana wakina mama wanajua budhet kwakweli maana vitu vingine sio vya msingi kuwepo safii sana Rais Samia napenda ahadi zako za kibabe
 

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,627
14,026
Hili ni jambo la maana sana wakina mama wanajua budhet kwakweli maana vitu vingine sio vya msingi kuwepo safii sana Rais Samia napenda ahadi zako za kibabe
Kwa kweli yaani kwenye bageti aisee sio mchezo..

SSH akiona kuna changamoto na akakupa madaraka na nyenzo,aisee anataka matokeo ukizingua unaenda na maji.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
17,609
19,036
Ushauri wa makamu mwenyekiti wa CHADEMA taifa na wadau mbalimbali naona umezingatiwa na Rais Samia Hassan kuhusu maeneo ya kiutawala sasa imebaki kutazama idadi mbunge anayoiwakilisha bungeni upande wa Tanzania bara:

 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
17,609
19,036
Ramani ikionesha mikoa mipya ya Simiyu, Geita, Katavi, Njombe, Songwe na ule mpya unaopigiwa chapuo mkoa wa Chato uanzishwe.
1660150370018.png


Je kutengeneza eneobunge, wilaya mpya, mkoa mpya ni kwa ajili ya kupeleka huduma karibu na wananchi au ni kwa ajili ya kujiongezea viti vya ubunge na nafasi zingine za kuendelea kupeana vyeo huku walipa kodi wakibeba mzigo mkubwa kulipa mishahara, marupurupu, safari, wasaidizi, majengo na magari ya kifahari.

1660150422774.png
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
17,609
19,036
SENSA 2022 ITUMIKE KWA SERIKALI IJITAFAKARI KUHUSU: UTAWALA BORA, MAENEO YA KIUTAWALA NA DEMOKRASIA

Matokeo ya SENSA 2022 yatumike gharama za kiuendeshaji za utawala kwa serikali kupunguza maeneo ya kiutawala, maana mikoa imekuwa mingi bila sababu za msingi.

Matokeo ya sensa ya 2022 yatumike kwa serikali kujisahihisha

Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi
Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali;

Taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote;

Kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi;

Taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira; na

Msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa.

Source : Hii ndiyo tofauti ya Sensa ya 2022 na zilizopita
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Top Bottom