Nampongeza Rais Samia kwa kusimama na wakulima kwa kuwaruhusu kuuza mahali popote palipo na Bei nzuri

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,206
9,642
Ndugu zangu Sote tunafahamu kuwa secta ya kilimo katika nchi hii imeajiri na kubeba kundi kubwa Sana la watanzania, Ni secta ambayo ndio pumzi ya familia na Kaya nyingi, Ni secta inayotegemewa na watanzania wengi Kama shughuli kuu ya kiuchumi, Ni kimbilio la wengi, Ni ngazi ya wengi, Ni njia ipitayo na kupitisha watu wengi Sana kuinuka kiuchumi, kilimo Ni mgongo uliowabeba watu wengi Sana katika nchi hii, Ni ziwa ambalo kila mtanzania ananyonya , kilimo ni Mbeleko iliyowabeba wengi Sana,Kilimo Ni MAMA Mlezi wa Taifa hili,

Hivyo ukikipuuza kilimo Ni sawa na kuwa umewapuuza watanzania, ukikiacha kilimo Ni sawa na kuwa umewaacha watanzania wanyonge nyuma, ukikinyonya kilimo kibajeti Ni sawa na kuwa umewanyonya watanzania na ukikibana kilimo Koo Ni sawa na kuwa umewabana watanzania Koo na kuwanyima puumzi.

Sote Ni mashahidi namna ambavyo wakulima wa nchi hii kwa miaka mingi tu ambavyo wamekuwa wakipata hasara kubwa licha ya kuwa wamekuwa wakihenyeka na kuvuja jasho mwaka Hadi mwaka, lakini maisha ya mkulima yamekuwa yakibaki na kuwa duni tu kila siku, hii nikutokana na Bei mbaya ambayo mkulima amekuwa akiuza na kuipata, mkulima licha ya kutumia gharama kubwa katika uzalishaji lakini amekuwa akipangiwa Bei ya kuuza na mahali pa kuuza, amekuwa akipewa mashariti ya kwamba hutakiwi kuuza kule na kule na utauza hapa nchini pekee na mipaka ikawa inafungwa,

Hivyo mkulima amekuwa kwa miaka mingi akibeba misalaba ya watanzania wote, licha ya kulilisha Taifa hili lakini mkulima huyu amekuwa akibaki fukara Sana kwa kuwa Hana uamuzi katika kujitafutia na kuuza mahali ambapo soko Ni zuri na Bei ni ya uhakika,

Rais Samia alipoingia na kuapishwa kuwa Mkuu Wa nchi na Amiri Jeshi mkuu amekuja na mtizamo tofauti wa kukifanya kilimo Ni biashara ,hivyo biashara yoyote lazima itoe faida na itafutiwe soko zuri lakini pia kuwe na mipango mizuri yakuifanya biashara inawiri na kushamiri, mh Rais Samia amekataa kufunga mipaka kuzuia mahindi yasiuzwe nje ya nchi, Jambo lililopelekea mkulima kuuza Bei nzuri Sana mwaka huu tangia wakati wa mavuno,, huku mh Rais akihakikisha kuwa chakula kinakuwepo nchini Cha kutosha kwa usalama wetu

Sasa wakulima wanafaidi jasho lao, wanafaidika na juhudi zao, Sasa vijana wanahamasika kujiingiza katika kilimo, Sasa uzalishaji wa kilimo unaongezeka kwa kila mtu , Sasa watu wanaitafuta Aridhi ili walime maana Sasa kilimo kinalipa na hakimtupu mtu, Sasa kilimo kinakwenda kuwa kimbilio lenye matumaini kwetu vijana, Sasa kilimo kinatoa nuru ya kuinuka kiuchumi, Sasa kilimo kinarudi katika mioyo ya watanzania waliokuwa wameanza kukata tamaaa baada ya kuwa wahanga wakupata hasara kila mwaka,

Nataka niwaulize mnaolalamika uamuzi wa mh Rais wetu mpendwa kutofunga mipaka, Hivi mnajuwa adha za kilimo? Hivi mnajuwa gharama za kilimo nyie? Hivi mnajuwa misukosuko ya kilimo nyie? Hivi mnajuwa ugumu wa jembe nyie? Mmewahi kulima? Mmewahi kushika jembe nyie? Mnajuwa hata namna ya kushika mpini wa jembe au jembe la kukokota na ng'ombe? Mnajuwa mkulima anaamka saa ngapi na kulala muda upi? Mnajuwa mwili wa mkulima unapata maumivu kiasi gani? Au kwa kuwa mnaona vitu vikija sokoni tu? Jembe Ni Vita inayohitaji kujitoa kujitolea na kuwa mvumilivu Kama Asikari Jeshi aliye vitani kupigania nchi yake, mkulima amechoka kupata hasara kila mwaka

Muwe na huruma na mkulima jamani, jaribuni kuvaa viatu vya mkulima muone Kama vitawatosha, vitawashinda kwa uzito na ukubwa wake, lazima vitawapwaya na mtavivua tu, Kama mnaona mkulima hastahili kufaidika na jasho lake Basi nendeni nanyi mkalime, nendeni mkashike jembe, msikae tu kunyonya jasho la mkulima huku mkiwa kimvulini

Kazi iendeleee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
 
Kwenye hili hata mm nampa rais Samia 100%. Ni uwendawazimu kumpangia mkulima wapi pa kuuza na namna ya kuuza mazao yake ili kuwanusuru wadangaji, machawa, wacheza pool, bodaboda, mama ntilie, machinga na madalali wa viwanja eti wasife kwa njaa.

Yaani nguvu kazi ya taifa inafanya kazi za kidwanzi kama hizo inaacha kwenda kulima??

Kama kuna "kima" yeyote anayeona mazao yako bei juu aende mashambani akalime mazao yake
 
Kwenye hili hata mm nampa rais Samia 100%. Ni uwendawazimu kumpangia mkulima wapi pa kuuza na namna ya kuuza mazao yake ili kuwanusuru wadangaji, machawa, wacheza pool, na madalali wa viwanja eti wasife kwa njaa.

Kama kuna "kima" yeyote anayeona mazao yako bei juu aende mashambani akalime mazao yake
Nashukuru Sana ndugu yangu kwa kuliona Hilo na kutambua maumivu anayoyapata mkulima na namna alivyookuwa anapata hasara kila mwaka licha ya kuvuja jasho jingi
 
Of course,

Huwezi kupangia watu bei kwa shughuli walizogharamia wenyewe...

Hata hivyo, sio siri tena kwamba bei ya vyakula imepanda sana duniani, na huenda ikaendelea kupanda!!

Kutokana na hilo, hakuna busara yoyote kwa uamuzi huo wa SSH kwa sababu Food Security ni kipaumbele cha taifa lolote lile!

Ningemuona kafanya jambo la maana endapo serikali yake ingenunua hayo mahindi kwa hiyo bei nzuri na kuyahifadhi kwenye maghala yake!!

The National Food Reserve Agency aims at guaranteeing national food security by addressing food shortages through procuring reserving and releasing food stocks efficiently and reliably.
 
Sahihi kabisa mkuu fikiria mafuta yanavyopanda na kushuka mbona watu wananunua na wanakazana kuyachimba na kilimo sasa watu wtalima kwa hiyo kithaminiwe kama mafuta au zaidi.
Bei ya kilo moja ya mbegu ni sh.6,500/=.
Tumekuwa tukiuza kilo moja ya mahindi [mavuno] kwa sh.150/= hadi sh.300/=.

Hii ina maana ili kupata pesa ya kutosha kununua kilo moja ya mbegu unalazimika kuuza mahindi kati ya kilo 22 na 44.

Tuhurumieni wakulima.
 
Kwenye hili hata mm nampa rais Samia 100%. Ni uwendawazimu kumpangia mkulima wapi pa kuuza na namna ya kuuza mazao yake ili kuwanusuru wadangaji, machawa, wacheza pool, bodaboda, mama ntilie, machinga na madalali wa viwanja eti wasife kwa njaa.

Yaani nguvu kazi ya taifa inafanya kazi za kidwanzi kama hizo inaacha kwenda kulima??

Kama kuna "kima" yeyote anayeona mazao yako bei juu aende mashambani akalime mazao yake
Swadqta!
Yaani mi huwa nakereka sana nnapoona Makundi hayo yamejazana mjini halafu wanalalamikia bei za vyakula.
Wengine wanashindia kukera tu abiria eti wanajiita wapigadebe.

Mama shikilia hapo hapo, mpk kila mmoja aone umuhimu wa kilimo.
Atakayeona anaonewa aende akalime na yeye basi
 
Of course,

Huwezi kupangia watu bei kwa shughuli walizogharamia wenyewe...

Hata hivyo, sio siri tena kwamba bei ya vyakula imepanda sana duniani, na huenda ikaendelea kupanda!!

Kutokana na hilo, hakuna busara yoyote kwa uamuzi huo wa SSH kwa sababu Food Security ni kipaumbele cha taifa lolote lile!

Ningemuona kafanya jambo la maana endapo serikali yake ingenunua hayo mahindi kwa hiyo bei nzuri na kuyahifadhi kwenye maghala yake!!
Nchi Ina chakula Cha kutosha,muwe mnafuatilia mambo
 
Nchi Ina chakula Cha kutosha,muwe mnafuatilia mambo
Chakula cha kutosha kwa muda gani?!

Na huko kutosha kwake kumezingatia affordability?! Kama nilivyosema, kuna globe food crisis... je, hicho chakula cha kutosha kimezingatia hayo?!
 
Back
Top Bottom