Fredrick Sumaye: Samia anaandaa Tanzania ya kesho

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,117
1669183530707.png

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amesema Rais Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa ya kuandaa Tanzania ya kesho.

Sumaye alisema hayo jana katika Kata ya Bonga, mkoani Manyara wakati alipopewa nafasi na Rais Samia ya kusalimia wakati msafara wa Rais uliposimama hapo akiwa njiani kwenda Babati.

Rais Samia jana alianza ziara ya kikazi mkoani Manyara. “Ninashukuru sana Rais kwa kunipa nafasi hii, jana (juzi) nilikuwepo kwenye uchaguzi wa kumpata mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara,” alisema Sumaye na kuongeza:

“Baada tu ya kuchaguliwa nilimwambia lengo la CCM ni kuendelea kuongoza dola na bendera tumekukabidhi wewe Rais Samia uongoze nchi yetu hadi 2025 na tena 2025 hadi 2030, tunasema sio kwa kukupendelea, bali kwa mambo makubwa unayofanya katika nchi yetu.”

Sumaye alisema watu wanaoona mbali wanaelewa anachokifanya Rais Samia kuijenga nchi na Tanzania ya kesho na akaahidi kumsaidia kwa kuwa anachapa kazi kwa kushirikisha Watanzania wote.

Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul alimshukuru Rais Samia kwa namna anavyotumikia taifa na kuleta maendeleo kwa wote.

“Ninakushukuru Rais Samia umenifanya sehemu ya serikali yako na ninapewa ushirikiano na watendaji wake, siwezi kulaumu na kwa unayofanya ya maendeleo kwa wananchi, tutasimama na wewe hadi mwaka 2025,” alisema Gekul.

Alisema Kata ya Bonga ni moja ya kata zilizonufaika na fedha za serikali kwa wananchi wake ambapo imepata shilingi milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa sekondari mpya ya kata na kwa sekta ya elimu kwa ujumla katika eneo hilo zaidi ya Sh milioni 665 zimetolewa.

Aidha, wameahidiwa pia kuongezewa zaidi ya shilingi milioni 100 kuboresha sekta ya elimu huku pia maji, umeme na miundombinu ikiendelea kuboreshwa.

Awali Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alizungumzia hali ya ukame na upatikanaji wa chakula nchini na kusema hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa kwa sababu serikali imejipanga kufikisha chakula cha bei nafuu katika maeneo yote yenye uhitaji.

Bashe alitoa kauli hiyo baada ya Rais Samia kusimama Kondoa mkoani Dodoma kusalimia wananchi.

Alisema halmashauri nchini zinapeleka taarifa za mwenendo wa bei ya mahindi katika maeneo yao na kwenye maeneo yenye bei kubwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), hupeleka mahindi na kuuza kwa bei nafuu kwa wananchi.

“Tumeshapeleka chakula katika halmashauri 41 zenye uhitaji wa chakula na sisi tunafungua duka chini ya maelekezo ya halmashauri na tunauza chakula kwa mwananchi mmoja mmoja kwa bei ya chini na sio kwa wafanyabiashara,” alisema Bashe.

Alisema pia serikali imetoa ruzuku ya mbolea ili wakulima waweze kumudu gharama na kutumia katika shughuli za kilimo kiweze kuwa na tija.

Aidha, Bashe alisema serikali pia inatoa ruzuku ya mbegu na kuwa miaka mitatu ijayo nchi itakuwa inajitosheleza kwa uzalishaji wa mbegu bora.
 
Kwenye mkutano wa hadhara wa Mama Samia uliofanyika mkoani Manyara nimemsikia Sumaye akimpongeza Rais Samia ila Sumaye hakumbuki alikotoka wala anakoelekea.

Samia kinachompoteza ni uchaguzi wa viongozi wasiofaa kuongoza Serikali Ssumaye hajatambua hilo.

Samia alishiriki na JPM kufukuza watu kazi watu wale wale wamerejeshwa Serikalini tena kwa nafasi zile zile, Sumaye hakukumbuka kutaja hili.

Viongozi wa ngazi ya mkoa na wilaya kupitia CCM waliochaguliwa ni wale walioondolewa na JPM akina Karamagi , Sumaye hakukumbuka kumweleza hayo.

Samia anakusanyiwa watu kwenye mikutano ya hadhara kazi yake ni kuongea na kuondoka kwa kusifiwa hana muda kusikiliza vilio vya maji, njaa na umeme. Sumaye hakuliona hili amuambie Samia.

Suala la Zanzibar kupokea fedha za mikopo na madeni kulipwa na bara Sumaye hakuliona hilo na hakumwambia.

Suala la bei za vyakula mfano mafuta, mahindi, maharagwe na mchele kupanda bei mara dufu Sumaye hakuliona hilo ili amuambie Samia

Suala la kufanyia vikao vya CCM Ikulu badala ya ofisi za CCM, Sumaye hakuliona ili amwambie Rais amia.

Wambulu wana akili ila Sumaye hajulikani uwezo wake kiakili ni mbovu, Havard university ulimaliza chuo Sumaye?
 
Mzee mzima anakuwa chawa hata haipendezi
 
hivi hawa watu hawaoni aibu kuongea hivo? miaka yote hiyo bado tu wanaandaa Tanzania ya kesho? labda ya kukatika maji na umeme forever.
 
Sekta ya kilimo imependelewa sana aisee hongera sana Rais Samia Suluhu kwa kuipa kipaumbele sekta hii maana asilimia kubwa ya Watanzania wamejiajiri katika kilimo.
 
Tulipokuwa vijana tuliambiwa vijana ni Taifa la Kesho.

Leo tu naanza Kusikia Maza anapanda Tanzania ya kesho.

Miaka 60 ya Uhuru kila kitu ni kesho tu. Hiyo kesho itafika lini!? Huu uhuni wa CCM unaudhi sana. Bora North Korea, China na Russia. Sisi tuna act tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom