Hebu twende taratibu kaka. Keleta ushabiki unamaanisha nini?? Mimi ni shabiki wa mpira na ndio maana nimechangia hapa. Kuhusu dogo De Bruyne ni kwamba ni miongoni mwa vijana wadogo ambao timu ya Chelsea iliwanunua na kumuacha timu aliyonunuliwa kwa msimu wa 2012. Msimu uliofuata 2012/2013 alipelekwa kwa mkopo na alipoonekana amefuzu alirejeshwa Chelsea kwa ajili ya kuja kuchezea timu kubwa. Ila bahati yake mbaya akakutana na mtu asiyejua kuwajenga watoto kisaikolojia Mr. Mourinho ambaye dogo alipokosea mechi mbili tu Mourinho alitoka nje na kuanza kumponda na kumkatisha tamaa. Kama ilivyokuwa kwa Lukaku, dogo alikata tamaa na ikalazimika kumuuza kwa Paund 18m. Hebu nambie kijana aliyenunuliwa miaka miwili tu nyuma kwa paundi 7m anapouzwa kwa 18m je huyo ni mbovu??
Kuna kitu ambacho unatakiwa ukifahamu kaka. Mourinho anatatizo la kutowaamini vijana na ndio maana hivi sasa yuko busy kununua wachezaji wapya huku akiua vipaji zaidi ya 20 vilivyopelekwa kwa mkopo timu nyingine. Lukaku alipelekwa kwa mkopo na kufunga goli 17, je washambuliaji wote waliobaki Chelsea walifunga goli ngapi?? Leo hii Mourinho na hicho unachokiita wewe uongozi wa Chelsea umakazana kununua Coasta, mtu ambaye ni prone wa majeraha na atakuwa na muda mrefu wa kujiadabt kwenye ligi ya uingereza huku wakimuacha Lukaku ambaye sasa amekuwa na yuko katika hali nzuri.
I won't wonder kama akina Ake, Omruo, na vijana wengine wakaishia kupoteza ndoto zao. Timu ya Chelsea chini ya Mourinho ni timu inayotaka ushindi wa muda mrefu. I'm sure na msimu huu mtaambulia patupu. Ilikuwa ndio muda wa kuwarudisha vijana waje wacheze na kuwaamini. Ila ndio kwanza mnaongeza msururu wa mibabu.
Usitake kumweka Mourinho nje ya lawama hizi.
Hiyo ndo tunaita PURE BUSINESS!