Moises Caicedo tayari ni legend wa Chelsea — na hii ndiyo ushahidi kwamba tayari amejijenga kama legend. Anapokosekana, kiungo inasambaratika na mabeki wanaonekana hovyo. Akiwepo uwanjani, kila mchezaji ghafla anaonekana kama superstar. Caicedo si anakaba tu, ana itercept mipira, anarudisha umiliki wa mipira, lakini pia ana uwezo wa kusoma hatari mapema na kufika mahali sahihi kwa wakati ili kuokoa.
Jana pia niliona jinsi wachezaji wenye uzoefu walivyokuwa wanachukua majukumu yao. Jordan Henderson alikuwa anawaelekeza wachezaji mara kwa mara huku akicheza kwa kiwango cha juu.
Kwa takwimu za jana, hakuna mchezaji wa Chelsea wala Bournemouth aliyekimbia umbali mkubwa kuliko Henderson — alikimbia km 12.
Martínez, kule nyuma, naye alikuwa akifanya kazi kubwa kupanga na kuongoza safu ya ulinzi.