Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

1769600538854.png
 
Utabiri wangu kwa usiku wa leo mechi zinaanza saa tano usiku kwenye UEFA Champions League: msiwe na roho juu, Chelsea inashinda leo
  • Arsenal wakiwakaribisha Kairat Almaty – ushindi wa 4–0
  • Bayern Munich ugenini dhidi ya PSV Eindhoven – ushindi wa 2–1
  • Real Madrid ugenini kwa SL Benfica – ushindi wa 4–1
  • Liverpool nyumbani dhidi ya Qarabağ FK – ushindi wa 1–0
  • Tottenham Hotspur ugenini kwa Eintracht Frankfurt – ushindi wa 3–2
  • Chelsea ugenini kwa Napoli – ushindi wa 4–3
  • Barcelona nyumbani dhidi ya FC Copenhagen – ushindi wa 3–1
  • Athletic Club nyumbani dhidi ya Sporting CP – ushindi wa 1–0
  • Manchester City nyumbani dhidi ya Galatasaray – ushindi wa 3–1
  • Atlético Madrid nyumbani dhidi ya Bodø/Glimt – ushindi wa 2–0
  • Atalanta ugenini kwa Union Saint-Gilloise – ushindi wa 2–1
  • Inter Milan ugenini kwa Borussia Dortmund – ushindi wa 3–2
  • Juventus ugenini kwa AS Monaco – ushindi wa 3–2
  • Paris Saint-Germain (PSG) wakitoka sare ya 2–2 dhidi ya Newcastle United uwanjani Parc des Princes
🎯 Ikiwa haya yatatimia, basi ni usiku wa kichaa kabisa kwenye #UCL. Moto wa soka wa kweli! 🔥⚽️✨

1769620692838.png
 
Kwaheri Raheem Sterling.

Ukurasa umefungwa rasmi!


Chelsea na Sterling wameachana kwa makubaliano ya pande zote, ambapo Chelsea imemlipa takribani £10m kama sehemu ya mshahara wake uliobaki—kati ya karibu £22m katika mkataba uliotarajiwa kumalizika tarehe 30 Juni 2027.

Safari yake imekuwa na dalili za ubora wa kipaji, lakini ikajawa na kukosa umakini golini, maamuzi mabaya na kutotulia kulikokwenda kinyume na viwango vya Chelsea, hali iliyomtoa kabisa kwenye kikosi cha kwanza.

 
Napoli vs Chelsea

4-2-3-1

------João Pedro------

Neto --- Enzo -- Estevao--Gusto

--Santos---Caicedo --

Cucurella--Fofana--Jame(C)

--------Sánchez--------

Subs:
1) Jorgensen
2) Merrick
3) Acheampong
4) Badiashile
5) Chalobah
6) Hato
7) Palmer
8) Garnacho
9) Gittens
10) George
11) Delap
12) Guiu

1769626697731.png
 
Duniani kuna vituko, eti Fofana ni beki!
Fofana ni beki mzuri, kocha ndie kaboa kumfanya CCB, hili suala Enzo Marseca alishasema kwamba nyakati zote alizomjaribu Fofana kwenye CCB hakucheza vizuri. Fofana anafaa beki wa pembeni ndipo anacheza vizuri
Kocha asipobadilisha mfumo kwa kuweka Backline ya 4 tutafungwa mengi
Anatakiwa kuingizwa Chalobah ili Fofana aende kwenye nafasi yake
 
Hongereni Chelsea kwa kupanda hadi nafasi ya 6, hatua kwa hatua tunapanda pamoja, tukijenga nguvu ya pamoja.
FT:
Napoli 2–3 Chelsea
💙🔥

Ushindi mkubwa, mentality thyabiti, na moyo wa kupambana hadi mwisho.
Safari inaendelea na tunaelekea hatua ya makundi 16 bora kwa ushujaa kabisa.

1769637478054.png
 
Chelsea kipindi cha kwanza

Pressing ilisababisha uwazi mkubwa katikati ya uwanja
Backline ya 3 na hasa Fofana kucheza kama CCB imesababisha difensi iwe butu

Kipindi cha pili baada ya Chalobah kuingia
Difensi ilikuwa imara zaidi
Kocha aliwaagiza wachezaji kuacha kupress sana na hivyo ule uwazi wa katikati ya uwanja ukaondoka. Chelsea ilirudi kuwa stable, balanced na tukashinda mechi. Hongera sana Rosenior kwa mabadiliko ya Kipindi cha pili
 
Chelsea wamevunja rekodi ya Napoli na Conte ya kutokufungwa nyumbani tangu 8 Desemba 2024, takribani miezi 13 na siku 21 bila kupoteza katika Uwanja wa Diego Armando Maradona.

Ushindi huu mkubwa pia umehitimisha safari ya Napoli kwenye UEFA Champions League msimu huu.
The Blues boys wanasonga mbele vifua wazi na majigambo.
 
Usipumbazwe na hayo matokeo anapata, pale hamna kocha.
Hivi raha mnapata wapi mkiwa mnapinga tu, mnatengeneza upinzani ndani ya ushabiki. Nakubali kama kuna mambo hayaendi vizuri ukipinga inamake sense. Lakini hata timu ikishinda kocha kabahatisha, akifungwa takataka hajui mpira..
Enzo Maresca alijitahidi hivyo hivyo mkamwita takataka, hata alipobeba makombe mawili bado mlimkebehi.
Mnapata wapi raha ya mpira kama kila wakati mnapinga tu na kuopose kila jambo ndani ya Chelsea.
Hamieni kule kwenye timu zinazofanya vizuri
Arsenal wanafanya vizuri, kashinda UEFA zote na kwenye ligi anaongoza. Nendeni huko mtuachie Chelsea yetu takataka tunajua jinsi ya kupambana nayo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom