Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Jamani jamani chelsea mkiweka yule beki wenu mwenye nywele kama kimba la mavi aloohhhh, barcola atamlambisha nyasi mpaka basi 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Sometimes mchezaji kuwa mzuri au mbaya hutokana na Kocha mwenyewe na mifumo yake.

Mfano beki Rudiger alivyokuwa akirudisha mipira nyuma na kubadilika kisha kuwa bora na kuuzwa toka Chelsea FC na kusajiliwa Real Madrid FC.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Nimeanglia mpira vzur Chelsea anaweza kumfunga PSG final madrid hakucheza kitimu
Wewe unajua soka


Xabi Alonso Bado Anatest Mitambo
Xabi Alonso bado yupo katika hatua za awali za kuelewa muundo bora wa timu yake—hajafahamu kikamilifu ni nani acheze wapi na kwa mtindo gani ili walingane na nafasi zao. Mashindano haya yameonekana kumshangaza, kana kwamba hayakuwa sehemu ya mpango wake wa maandalizi.

Kwa mtazamo wa kimantiki, huenda itamchukua msimu mzima kufahamu kwa undani kiwango cha vipaji alivyonavyo: nani anaweza kukabili presha, nani ndiye mhimili wa timu, na nani ana uwezo wa kubadilisha mwelekeo wa mchezo katika nyakati muhimu.

Tusisahau—Xabi Alonso bado ni kocha anayekua na anajifunza kadri siku zinavyosonga. Yuko mbali sana na mkongwe Luis Enrique ambaye tayari ameweka mizizi imara katika ulimwengu wa ukocha. Huu ni mchakato wa hatua kwa hatua, si mchezo wa kubahatisha.

Kudhibitisha hii, jana mchezo ulikuwa wa upande mmoja na pia wachezaji wa Real Madrid ni kama hawakujua wachezeje na wakabe naman gani, wamebaki kusngaa tu hadi mechi imeisha

Natarajia msimu ujao Laliga Real Madrid itafanya vibaya sana kama Xabi Alonos bado atakuwa hajaijua vizuri jinsi ya kuwatumia hao wachezaji
 
Sikuona mchezo wowote mzuri wa PSG jana, wanaonekana wazuri kwa sababu wale wapuuzi wa Real Madrid hawakucheza kama vile walikuwa kwenye mgomo.

Nilitazama hadi dakika ya 70 nikaenda kulala, kwani mchezo ulikuwa wa kuchosha kutokana na Real Madrid kutokuwa na ari ya kushindana.

PSG walitumia vyema mapengo, mapenyo na makosa ya Real Madrid,
Walicheza mpira na mabeki, wakivunja safu za ulinzi, na kufunga mabao rahisi.

Ilikuwa kama marudio ya kichapo cha kihistoria cha Ujerumani dhidi ya Brazil kwenye Kombe la Dunia mwaka 2014.

Kama Liam Delap, Joao Pedro na Pedro Neto wakicheza kule mbele wakawapress hao mabeki wa PSG ili wasipasiane wenyewe kwa wenmyewe tita wa botafogo nakuambia

Tusubiri jumapili tuone na tumuombee Maresca aone kama nilivyoona mimi na kuiandaa timu kwa kuwapress hao mabeki
 
Chelsea dhidi ya PSG

-----------Delap------------

Pedro --- Palmer ---Neto

-- Enzo --------Caicedo/Santos-

Cucurella -- Colwill ---Tosin----James

------------- Sanchez-----------------

Tumuombee Maresca aone safu hii
Ombea pia Sanchez aamke katika hali nzuri siku ya Jumapili
 
1752112658960.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom