MosDef na
Jaslaws - @agosti8 na
kalou, kuna arguments mbili hapa ambazo ninavyoona zinafanya majibizano yote haya: UBORA VS MAFANIKIO kati ya LIVERPOOL NA CHELSEA
Mtazamo wangu ni kuwa;
1. Liverpool tangu kuanzishwa kwake hadi sasa ina mafanikio (kwa mantiki ya idadi ya makombe) zaidi ya Chelsea
2. Chelsea kwa sasa ni timu bora kuliko Liverpool.
3. Historia: Kuna mtu ameandika hapo juu kuwa Liverpool ilikuwa na makombe 18 wakati huo Man utd wakiwa na 7. Liverpool ikabaki hapo hapo hadi sasa man utd ina makombe 20. Je, bado tuiite Liverpool ni timu bora England kwa kuwa aliktangulia kuwa na makombe mengi zaidi ya timu zilizopo sasa kwenye ligi?
4. Lakini historia hiyo hiyo imetuonesha kuwa Chelsea ya miaka 14 ya hivi karibuni imekuwa iki-improve na kujiwekea historia ya aina yake. Hivyo majibizano haya siyatofautishi sana na kipindi ambacho man utd alitwaa labda kombe lake la 8. Liverpool (kama kawaida yao ya historia) nina uhakika walikuwa wakiongea kama wanavyoongea sasa (historia historia historia...sisi ni bora kwa kuwa tuna makombe 18 nyie mmechukua haka ka nane tu msipige kelele)
5. Kwa mantiki hiyo basi ninyi mashabiki wa liverpool nendeni kwenye thread yenu mkajinadi jinsi mlivyokuwa timu BORA NA MAARUFU YENYE MAFANIKIO kipindi hicho mtuache sisi tukijinadi jinsi tulivyo TIMU BORA NA YENYE MAFANIKIO kwa sasa.
6. Kuna possibility (as a chelsea fan: 0.000000000000001%) ya nyie kuchukua kombe la EPL (khe khe khe) mwaka huu. Mtakapolichukua, ndipo mtakapokuwa na haki ya kusema KWA SASA na KIPINDI HICHO (mara ya mwisho kwenu kuchukua kombe) ninyi ni timu bora na yenye mafanikio uingereza.
7. Sasa basi, hadi hapo mtakapoweza kufanya hivyo, hamtusumbui sana (zaidi ya kujaza comments zisizo na mantiki kwenye thread yetu) mnapoongelea historia kwani nina uhakika kwa miaka mingine mingi ijayo Chelsea bado itakuwa ni timu yenye mafanikio na bora Uingereza na Ulaya. Mtakuwa na la kusema?
8. Historia imetufunza, "Kutangulia sio kufika" mlitangulia mkapitwa...kaeni kimya mjipange! Na kama kwa kikosi mlichonacho sasa ndio mnadhani mmejipanga kuendelea kubaki pale juu..think again!!!
9. Oh kuna aliyesema anayeshabikia chelsea kazaliwa 2000. Hiyo ni argument ya kitoto sana na sijui kwa nini huwa mnaitumia. So what..aliyezaliwa 2000 hana haki ya kushabikia mpira na timu aipendayo?
10. Mfano wangu mimi niliyezaliwa 1987: Mimi nilipoanza kuufaham mpira wa ulaya kulikuwa na Arsenal ya Highbury na manchester united (honestly Liverpool ilikuwa ile ile ya kujisifia historia so haikuwa kwenye wish list yangu). Nilisafiri kwenda Nairobi mwaka 2000, nakumbuka tukaenda supermarket na nikatakiwa kuchagua kitu cha kununua. Nilienda section ya nguo na kukuta jezi ya blue ya chelsea (I love the blue color) among other jerseys na nyingine yenye maneno ya KARIBU KENYA. Nilizitaka zote..nikazibeba! Nilipofika pa kulipia mama yangu mdogo akanitaka nichague moja kati ya zile...sikuweza kuchagua. Bahati nzuri kulikuwa na mzungu nyuma yetu alivyoona vile akasema atanilipia moja. Tangu siku hiyo ndipo nilipoanza kuifuatilia timu ya Chelsea na kuipenda.
Na kwa kipindi kile ilikuwa rahisi kujivunia kuishabikia timu hiyo kwani ilikuwa na wachezaji weusi wanaofahamika kama kina Babayaro, Hasselbaink, Desaily mfaransa huyu namkumbuka kwenye world cup zaidi!
Mtuwache na timu yetu...maana kipindi hicho nina uhakika huyu Abramovich hakuwepo (au sikumbuki but am sure hakuwepo) na bado vikombe vidogo vidogo tulichukua na kuwafunga hao kina man utd na city liverpool na arsenal...
Ni hayo tu kwa sasa sitaki kuwasikia tena mkija kuongea pumba zenu hapa! nendeni kwenye thread lenu tutaonana 27th April..