Ninapenda jinsi Maresca anavyosimamia mazoezi ya wachezaji ingawa yeye hatoi mazoezi makali ya mwili. Nadhani hatutakuwa na majeraha mengi ya misuli msimu huu, ikiwa tukiwa nao, haitakuwa kubwa kama ilivyokuwa miaka miwili ya nyuma.
Sisemi kuwa hatutakuwa na majeraha, lakini huenda haitakuwa mbaya kama ilivyokuwa miaka ya hivi karibuni. Pia, kuwa na wachezaji wanaoweza kucheza nafasi nyingi hurahisisha balance ya kwenye timu hata pale wachezaji muhimu wakiwa hawapo.
Hili tulilalamikia kwamba mazoezi ya Pochettino yalikuwa ya kizamani na yenye kuweka mzigo mkubwa kwa wachezaji na kusababisha matatizo ya misuli na hivyo kuongeza majeruhi yasiyotakiwa na yanayoweza kuzuilika.
Hii ndio appraoch ya Kipara na ndio maana Man City hawana majeruhi wengi.
Kama tukifanikiwa kwenye hilo na balance ikawepo kwenye defensi yetu, top 4 tumeingia kwa sababu sio Spurs, Aston villa au Man u wataweza kutuzuia