Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Huyu hapa Willian Estevão akiwa na familia na wakala André Cury baada ya kusaini mkataba wake Chelsea hadi Juni 2033.

"Hongera Palmeiras kwa mauzo makubwa zaidi kuwahi kutokea kutoka Amerika Kusini kwenda Ulaya", Cury alisema.
1719097873923.png
 
Sisi Tanzania ndiyo hatuna vipaji au shida ni nini? Huko Africa Magharibi kusikia mtu kwenda Ulaya kujiunga na timu kubwa ni kawaida sana.
 
Napendelea hii approach waliokuja nao, hakuna haja ya kuanza kumlipa mchezaj hela kubwa halaf uwanjan impact yske ni ndogo
Fabrizio Romano: "Chelsea wamefanya mawasiliano katika miezi ya hivi karibuni ili kuelewa masharti yeyote ya kuweza kumsajili Williams.

Ninachoambiwa sasa, ni kwamba ingawa Chelsea wanamkubali Williams, Chelsea haitasonga mbele kumsajili Williams, kwa sababu ya gharama ya dili hilo."

1719140276497.png
 
View attachment 3023882
Hakuna kitu humu, madueke wa spain.
 
Hakuna kitu humu, madueke wa spain.
Nico Williams ni mzuri sana na usimfananishe na Madueke
Ana miaks 21 tu na msimu uliopita ana assists 14 kwenye ligi tu
TATIZO lake litakalomfanya asisajiliwe na Chelsea ni kuhusu mshahara wake mkubwa

"Vilabu vya Premier League vimearifiwa kuwa mshahara wa Nico Williams anaouhitaji ni zaidi ya £300,000 kwa wiki."
 
Chelsea wanasonga mbele zaidi katika mazungumzo ya kumsajili Marc Guiu kwa kuanzisha release clause yake ya pauni milioni 5.

Makubaliano na Guiu yalihusu mkataba wa muda mrefu yanazidi kukaribia na kuzidi ile ya Bayern baada ya mazungumzo chanya wikendi hii.

❗️ Barça ilimpa Guiu mkataba mpya - bado hakuna jibu la mwisho kutoka kwa upande wa mchezaji.

1719178716567.png
 
View attachment 3024178
Lamasia product, tukimpata huyu tumepata lulu. Ni striker mzuri sana
 
Jonathan David
Huyu ana consistency kwenye ufungaji tangu akiwa Gent. Kwa saidi ya misimu sita
Kule Lile kaweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa mara zote na kumpiku Eden Hazard
Tumchukue tusimchukue?

1719208249466.png
1719208319045.png
 
Chelsea wamepoteza hamasa ya usajili wa striker wote isipokuwa wamebaki na
  1. Jonathan David wa Lile ana miaka 26 kwa chini ya £30m
  2. Marc Guiukinda wa Barcelona kutoka Lamasia academy, ana miaka 18 kwa £5m
 
Haya mambo ya ajabu tunashindwa vipi kwenda brentford,dormond, astonvilla,new castle ,Rb leipzig wapo wafungaji wawili,tuchukue mfungaji mmoja wa maana kuliko kukusanya vikundi vya watoto?inakuwaje lb leipzig ina openda na benjamin sesko sisi tuna jackson?
 
Nico Williams ni mzuri sana na usimfananishe na Madueke
Ana miaks 21 tu na msimu uliopita ana assists 14 kwenye ligi tu
TATIZO lake litakalomfanya asisajiliwe na Chelsea ni kuhusu mshahara wake mkubwa

"Vilabu vya Premier League vimearifiwa kuwa mshahara wa Nico Williams anaouhitaji ni zaidi ya £300,000 kwa wiki."
Unasema ni mzuri ulishamuona akicheza? Mchezaji mchoyo sana huyo.
 
🚨 Marc Guiu yuko mbioni kuondoka FC Bracelona

✅ Kuhamia Chelsea kunakaribia sana

📌Kama hakuna mabadiliko, yatatokea

1719304096095.png
 
Asists 14 na unamuita mchezaji wa miaka 21 mchoyo? hujitambui kweli
Ndio mana nikakuuliza ww unaejitambua ulishawahi kumuona akicheza uchezaji wake? Au umeishia tu hapo kwnye Assist 14 ukaconclude kuwa ni mchezi mzuri.
 
🤝Makubaliano yamefikiwa na uamuzi kuchukuliwa: Marc Guiu atasaini Chelsea hivi karibuni

💰Chelsea yakubali kulipa milioni 6 RC.

💙📘FC Barcelona ilitoa milioni 2 pamoja na addons, lakini Klabu ya Chelsea iliongeza ofa hiyo mara tatu.

@marca

1719305549221.png
 
Ndio mana nikakuuliza ww unaejitambua ulishawahi kumuona akicheza uchezaji wake? Au umeishia tu hapo kwnye Assist 14 ukaconclude kuwa ni mchezi mzuri.
Nilishaeleza kwa ufupi style ya uchezaji waek, hata nikisema hapa hutaamini kwa sababu wewe ukishamchukia mchezaji damu yako imemkataa.

Pamoja na kwamba hatutamchukua lakini ngoja nieleze aina ya uchezaji wake

Nico Williams ni winga mpana mkatili sana
anapenda kunyang'anya mpira kutoka kwa wapinzani wake na anaweza kudhibiti mpira usichukuliwe
Ni mmoja wa wachezaji wa Laliga wenye kasi kubwa
Ni mchezaji ambaye akipata mpira hufanya maamuzi ya haraka ya kutafuta wenzake
Amefanya hivyo wakati akiichezea Athletico Bilbao na pia alifanya hivyo wakati akiichezea timu yake ya taifa ya Hispania.
Nimemfuata katika baadhi ya mechi za Laliga na katika timu ya taifa ya Uhispania
 
Marc Guiu kwenda Chelsea, here we go! Klabu hiyo imeiarifu Barcelona kuhusu mpango wa kulipa release clause ya euro milioni 6 kwa mshambuliaji aliyezaliwa 2006.

Makubaliano ya mdomo yamekamilika kupitia maajenti wa Guiu, sasa yanayoendelea ni hatua rasmi baadaye wiki hii.

Guiu anatarajiwa kusaini mkataba wa muda mrefu katika klabu ya Chelsea

1719339273357.png
 
View attachment 3026187
Hivi dogo anakuja timu ya wakubwa au anaenda chelsea B
 
Hivi dogo anakuja timu ya wakubwa au anaenda chelsea B
Wakubwa, first team. Ni striker mzuri akipewa dakika kadhaa pale hata 10 au 5 na baadhi ya mechi ndogo kama za Karabao itamtosha kukua na kukomaa. Akifikisha 20 huyo atakuwa ni striker wa kutufaa sana. Ukufuatilia maoni ya mashabiki wa Barcelona wanalaani ile mbaya.
Barcelona wameshindwa kumuweka kwa sababu hali yao ya kifedha wasingeweza kumpa mhshara wa mil 6 kwa mwaka ambao Chelsea wamemuahidi

Baadhi ya sifa zake
• Mrefu na mzuri hewani
• Ni mzuri kwenye kupiga mashuti ya nguvu
• Hutumia miguu yote miwili
• Agressive na mwenye nguvu
• Anajua kufanya mbio za timing kuwapita mabeki
• Kwa release clause ya £5m sio gamble mbaya, ni nzuri

Similar Discussions

Back
Top Bottom