Alama za uchezaji kwa wachezaji wa Chelsea dhidi ya Arsenal jana
-Mauricio Pochettino - 0
Hakuwa na mbinu yeyote ya kujilinda wala kufunga magoli, kazembea makosa ya wachezaji hadi tukafungwa mabao matano bila
-Djordje Petrovic - 6
Alifungwa mabao matano, lakini kwa uungwana, aliokoa mabao kama 8, yaani asingeokoa tungefunkwa mabao 13-0.
-Alfie Gilchrist - 3
Kutupwa katika kina cha maji marefu huku hana uzoefu wa kuogelea
Axel Disasi - 3
Sehemu ya safu ya ulinzi iliyoruhusu mabao matano, bila kupata hakiki nzuri.
Benoit Badiashile - 4
Ilianza vizuri ila baadaye akaanza kupoteza mipira hovyo na kuonyesha ulegevu katika kumkabili adui anaposhambulia
Marc Cucurella - 5
Ilionekana kufanya vizuri mapema katika kipindi hicho cha kwanza tulipokuwa kwenye mchezo. ila baadaye alizidiwa na Saka na White kwa pamoja bila wenzake kumsaidia
Moises Caicedo - 4
Kapotezwa na kasi ya wachezaji wa Arsenal na hakukuwa na lzaidi kufanya kwenye tim u ya Chelsea ambayo haikuwa tayari kutoa ushirikiano kwenye kukaba
Conor Gallagher - 5
alijitahidi sana kucheza ila uwezo wake haukuunmgwa mkono na wenzake
Enzo Fernandez - 4
Tena kama Caicedo, kapotezwa kabisa
Noni Madueke - 3
Angalau alijaribu kuchukua watu wachache hapa na pale lakini hakuweza kusaidia timu kujilinda
Nicolas Jackson - 6
Alijitahidi sana kupeleka mashabulizi mbele lakini alijikuta yuko peke yake mbele kama mgeni aliyepotea porini
Mykhailo Mudryk - 2
Hakuonyesha chochote. Hakuna akili ya mpira, kama vile hakuwa na hamu ya mpira, hakimbii, hakabi wala kukimbia uwanjani. Alitisha sana.