Mauricio Pochettino ameweka msisitizo mkubwa na hata shinikizo kwa wachezaji kucheza na kushinda usiku huu.
Pochettino alitoa hotuba kwenye uwanja wa mazoezi - amechoshwa na mawazo ya wachezaji kuwa wako salama. testi ya akili usiku wa leo kwa wachezaji kujibu mashabulizi kwa kushinda
Maoni yangu
Tulikuwa tunamlaumu kocha tangu mwanzo kwa kutokuwa na demand kubwa kutoka kwa wachezaji
Sasa naona ameanza, akiendelea hivi, Chelsea itakuwa inashinda mechi nyingi za kutosha kuwepo kwenye michuano ya Ulaya
Nasikia pia kuwa mazoezi tangu Juzi yamelenga kwenye kujilinda na msisitizo kwenye kukimbia wakati wanamiliki mpira na wakati hawamiliki mpira
Again Tatizo la wachezaji wa Chelsea hasa kubwa niu wakati hawana mpira, tunatengeneza nafasi nyingi na nzuri sana ila wakipoteza tu mpira wanmaganda kama minazi ya pwani au milingoti ya kujengea na kuacha timu pinzani zikifanya kaunta na kutufunga
Hii mentality ya Pochettino ikiendelea hivi atakuwa sasa anajifahamu na mashabiki wengi tutaacha kumuandama
Tusubiri tuone bounce back ya leo