Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Panga la FFP inaweza ikalazimisha hilo, kama sio msimu huu, msim u ujao tusipokaa sawa tutapigwa hadi points 15 ambazo zinaweza kutuweka pabaya kwenye ligi
View attachment 2949820
james katika kuongeza mkataba msim uliopita tu.

Na huyu Duncan Castle sio source ya kuiamini katika habar zetu.

na hizi habar zote zinakuja kwa sababu tumefanya vibaya.

Wapo wakina lukaku,sterling,kepa,cucurela 50/50 hawa wote huenda wakaondoka

Lukaku saudi wanamnyemelea
 
FT.3-2

Tunahitaji kushinda kiporo chetu then huenda tukawa wa 8

Nafasi ya 11

Screenshot_20240331-212920.jpg
 
Confirmed
Chelsea wanapanga kuwauza Reece James na Conor Gallagher msimu huu wa majira ya joto
Klabu inataka kuingiza zaidi ya pauni milioni 100 katika mapato ya ziada ili kuepuka kukiuka Kanuni za Faida na Uendelevu za Ligi Kuu (FFP).
  1. Conor Gallagher = £50
  2. Reece James = £60
Pia hawa watauzwa
  1. Ian Maatsen
  2. Trevoh Chalobah
  3. Lewis Hall
  4. Armando Broja
  5. Romelo Lukaku
  6. Hakim Ziyech
  7. Kepa
  8. Sterling
Ungejua Chelsea walivyo wajinga
 
Team ambayo haina inachofundishwa ndio hii.

Hakuna tactics zozote inayofindishwa.
 

Attachments

  • IMG_2420.jpeg
    IMG_2420.jpeg
    1 MB · Views: 17
Mwekezaji na yeye mjinga tu , huwezi kubadilisha timu nzima afu unategemea uwe top four. Kwanza hapo walipo wamejitahidi sana.

Saa nyingine hivi vilabu viwe vinaangalia na sampuli za hawa wawekezaji.
 
To Chelsea

Mwandishi wa habari wa Italia Gaetano Fedele:

"Kuna kipengele katika mkataba mpya uliosainiwa na Victor Osimhen. Mnigeria huyo tayari amekubaliana na klabu nyingine na ataondoka majira ya joto. Nina hakika kwamba Mnigeria huyo anakwenda Uingereza. Niamini, anajua pa kwenda."

To PSG
Kulingana na wakala wa kocha wa Bologna, Thiago Motta, Dario Canovi, Victor Osimhen anarejea Ligue 1 badala ya Ligi ya Uingereza.

"Kwa maoni yangu, kuna uwezekano mkubwa akaichezea Paris Saint-Germain."

Maoni yangu
Sipendelei Victor Osimhen aje Chelsea kutokana na bei yake kubwa. Hata hivyo, ikiwa atajiunga na Chelsea, jambo moja ni wazi: hatakosa nafasi ambazo Jackson anapoteza kwa sasa.
 
Ebu soma Behdad Eghbali anavyosema kuhusu mmiliki wa Brighton. Kwa maneno yake anaitamani Brighton ambayo ina soko la kati na timu iliyokaa katikati ya table na kuimarikia hapoo. Nasema anatumia 10% kwenye mishahara na anashinda mechi kadhaa sawa sawa na timu zilizotumia pesa nyingi na huyo Tonny Bloom anatenengeza faida kubwa. Wau!

Tukumbuke kuwa huyo ndie mwenye share kubwa pale Chelsea na pia ndie anayetarajiwa kumrithi Tod Boehly kama Mwenyekiti na Mtendaji mkuu wa Chelsea kuanzia 2027. Tumekwisha

View attachment 2949707
Kama haya ndio maono yake sahauni kuhusu makombe. Sahauni kabisa
 
Kama haya ndio maono yake sahauni kuhusu makombe. Sahauni kabisa
Maneno ni vitu viwili tofauti

Huwez sema hivyo then utumie 1B katika usajili o utoe 100M kwa wachezaj watatu tofauti ndani ya miez 6


Nahisi hapo lengo ni kupunguza hasara na kuapata faida likes Liverpool,Madrid,

Na hiyo faida unaipataje ni kwa kuwin sema tu the approach wanayoitumia sio sahihi

Ngoja tuone hali
 
Nyie hata mshinde game zenu zote zilizobaki hamuwezi kutufikia

Hivi yule Tahit Chong hamjamuona? Maana nae anazo rasta,atawafaa sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom