lembu
JF-Expert Member
- Dec 31, 2009
- 19,383
- 25,490
Na mradi wetu unaogopwa zaidi kuliko hizo zingine, Kocha ajaye kama Pochettino ataachishwa kazi msimu wa kiangazi atakuwa na changamoto sana kwenye hii klabu kwa sababu ya wachezaji wengi wachanga, pili demand ya fanbase ya Chelsea ni kubwa na yenye kumuweka kwenye wakati mgumu kila kocha atakayejaribu kuchukua hii kandarasi ya kuirudisha meli iliyozama mahali pakeTunaweza kuwa tunawakat mgumu kumpata kocha ajaye maana vilabu vingi vikubwa nao wanataka kocha.
Liverpool
Bayern
Barcelona
Tunakaz kubwa sana kumshawishi kocha ajae kama tukimtimua yule Tapeli wa Argentina
Kitu ambacho nadhani itasaidia ni kwamba hadi wakati huu hawa wamiliki wamejifunza, nasikia pia hata walifikia sehemu hawaelewani kwa sababu ya jinsi mradi unavyoendeshwa
Kocha atakayefanikiwa Chelsea ni lazima kwanza awe ni
- kocha wa kaliba za juu na mwenye mbinu nyingi za kushinda makombe.
- Pia awe na uzoefu wa kuwanoa vijana wadogo kama akina Mudryk, Madueke, na wengine ambao wanaonyesha ishara ya kuja kuwa wachezaji wakubwa kule mbeleni.
- Pia kocha ajaye aweze kujua pancha za hii timu ziko wapi na awe na ujasiri wa kuwataka viongozi na wamiliki wasaidie kwenye kuziba hizo pancha
- Pia kocha ajaye apewe madaraka zaidi juu ya usajili management na uuzwaji wa wachezaji
TODDY - Chelsea fc ni Project UCHWARA na KITAPELI.
umenichekesha sana.