Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Boehly jasusi la CIA
20230416_165742.jpg
 
1st half tulicheza vizuri sema baada ya chukwumeka kupata injury tatizo likaanzia hapo. Maana mudriky huyu jamaa bingwa wa mtindo ya nywele mpira wake mchache labda bado hana confidence, sterling kacheza vizuri, lakini pale kwenye namba 9 bado Jackson jamaa anazulula sana japo anacheza vyema sema ange tulia kwenye box ange score vizuri sana huyu jamaa wa kutwa senesi nae mapepe
Anazurura vipi? Jamaa anacheza vizuri tatizo hama msaidizi pale mbele. If you watched a game utagundua
 
Let's wait and see. Ila haya mambo ya kuchezesha wachezaji out of position sio kabisa
Ni mbinu za kocha, zikileta matunda mazuri anasifiwa, zikileta matokeo mabaya kocha anakosolewa na sa nyingine kutukanwa. Hii ni mpira wa miguu. Kwa Maatsen alifanya hivyo akacheza vizuri na Chelsea ikashinda pre season.
 
Anazurura vipi? Jamaa anacheza vizuri tatizo hama msaidizi pale mbele. If you watched a game utagundua
Sometimes alikuwa anashuka kuchukua mipira pale Kati kule mbele Kuna kuwa hamna mtu zikipigwa krosi au pasi za kufunga yeye anakuwa hayupo eneo la tukio. Lakin simpingi anacheza vyema
 
Poleni sana wana Chelsea wenzangu
Kiushabiki tumefulia
Kimpira ni sawa kabisa, tumecheza vizuri
Mchezo wa leo umeonyesha tabia zote za wachezaji wasio na Chemistry na pia uzoefu
Mfano tofautisha mabeki wa Westham na wa Chelsea
Mabeki wa Westham walicheza kwa nidhamu ya hali ya juu
Sisi tumejilinda kitoto mno, kuanzia Kipa hakuna kitu pale kwa Sanchez, naona sura nzuri tu na urefu wa kupendeza, Afadhali Kepa wetu
Mabeki wetu wanahitaji kulindwa sana, sio wazoefu
Kipindi cha kwanza tulicheza vizuri ila kipindi cha pili mpira umekuwa ukichezwa zaidi na mabeki ambao nao wanapasiana kwa taratibu mno.
Tunahitaji striker wa pili ili kupeana ushindani na pia kupokezana
Hitimisho
Matokeo kama haya yalitegemewa kwa timu mpya na changa isiyo na uzoefu na wala hawana chemistry nzuri
Chelsea inavyoziodi kucheza inapata uzoefu na kujengezana chemistry na kocha naye atakuwa akijifunza kitu kwa hii squad changa
Caicedo na Lavia wakishatulia katikati ikatulia mambo yatabadilika tu
Sterling akiendelea kucheza kama leo atakuwa anautendea haki mshahara anaolipwa
Tukumbuke kuwa Westhama mwenye umri mdogo ni Paqueta ana miaka 26, wengine ni zaidi ya hapo. So leo ilikuwa ni mechi ya wazee wazoefu na vitoto vya miaka 21/22 kwa wastani
Leo umekosa Cha kusingizia?unadai una WATOTO daah wee jamaa hayo MAHABA YATAKUUA
 
Anazurura vipi? Jamaa anacheza vizuri tatizo hama msaidizi pale mbele. If you watched a game utagundua
Sometimes alikuwa anashuka kuchukua mipira pale Kati kule mbele Kuna kuwa hamna mtu zikipigwa krosi au pasi za kufunga yeye anakuwa hayupo eneo la tukio. Lakin simpingi anacheza vyema
 
Moja ya swali muhimu mnalotakiwa kujiuliza ni je, MTU kama Caicedo, tutamtumia kama alivyokuwa anatumika Brighton?

Inawezekana huko mbele akaja kuclick, lakini asicheze kwa ubora kama alivyokua anatumika Brighton.

Inshort karibu sajili zenu zote ni kamali, nyie mmeangalia mchezaji anacheza vizuri, mnabeba, kumbe huko mlipowatoa walionekana wazuri kwa sababu za mifumo ya huko
 
Derby hiyo hata kama Chelsea FC wangekuwa pungufu na West Harm wakawa wengi bado tu wangefungwa West Harm maana wanajuana vizuri sana.

Bila unafki Chelsea FC hii si ya kukosa kabisa kuangalia mechi zake zote ingawa mwanzo ni mgumu.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Hapa hakuna mwanzo.. hali ni hiyo hadi 2024.. watasomana season ijayo hao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom