Poleni sana wana Chelsea wenzangu
Kiushabiki tumefulia
Kimpira ni sawa kabisa, tumecheza vizuri
Mchezo wa leo umeonyesha tabia zote za wachezaji wasio na Chemistry na pia uzoefu
Mfano tofautisha mabeki wa Westham na wa Chelsea
Mabeki wa Westham walicheza kwa nidhamu ya hali ya juu
Sisi tumejilinda kitoto mno, kuanzia Kipa hakuna kitu pale kwa Sanchez, naona sura nzuri tu na urefu wa kupendeza, Afadhali Kepa wetu
Mabeki wetu wanahitaji kulindwa sana, sio wazoefu
Kipindi cha kwanza tulicheza vizuri ila kipindi cha pili mpira umekuwa ukichezwa zaidi na mabeki ambao nao wanapasiana kwa taratibu mno.
Tunahitaji striker wa pili ili kupeana ushindani na pia kupokezana
Hitimisho
Matokeo kama haya yalitegemewa kwa timu mpya na changa isiyo na uzoefu na wala hawana chemistry nzuri
Chelsea inavyoziodi kucheza inapata uzoefu na kujengezana chemistry na kocha naye atakuwa akijifunza kitu kwa hii squad changa
Caicedo na Lavia wakishatulia katikati ikatulia mambo yatabadilika tu
Sterling akiendelea kucheza kama leo atakuwa anautendea haki mshahara anaolipwa
Tukumbuke kuwa Westhama mwenye umri mdogo ni Paqueta ana miaka 26, wengine ni zaidi ya hapo. So leo ilikuwa ni mechi ya wazee wazoefu na vitoto vya miaka 21/22 kwa wastani