Nimekusikia ngoja na mimi nije na orodha yangu,
Makocha 10 bora wenye mbinu na style bora na inayofanya kazi msimu huu wa 2022/23 ni
- Mikel Arteta - Ana timu changa lakini ameweza kukaa kileleni mwa ligi na kuwashinda akina pep ambaye ana timu nzuri
- Ten hag - Tangu apoteze mechi mbili za mwanzoni kabisa mwa ligi na bado akiwa mgeni, toka hapo amekuwa na wining percentage nzuri sana nafikiri hata kuliko PEP ukichulia ubora wa squad aliyonayo PEP
- Antonio Conte - Pamoja na timu mbovu aliyonayo amefanikiwa kuibakiza timu kwenye top 4
- Pep Guardiola - huyu alitakiwa kuwa kileleni mwa ligi kulingana na wachezaji bora alionao lakini kwa sababu ya ufahidhina kwenye style of playing ameishia kuwa kwenye namba 2 ambayo nayo anaweza kupokonywa na Man U
- Eddie Howe - timu ya kawiada sana iliyokuwa mkiani lakini kajitahidi na kuipeleka timu hadi nafasi ya 5
- Marco Silva - Timu ya Championshio lakini amekuwa na mbinu na style dhabiti iliyompa point za kutosha kuwa kwenye top 7 hadi sasa
- Roberto De Zerbi - Pamoja na kweli kwamba Potter aliiacha timu pazuri lakini pia naye kaonyesha kuwa kocha mzuri na mwenye mbinu hasa kwa kuweza kuibakiza timu juu ya table na pia kuweza kufunga timu kubwa kudroo na kwuafunga Liverpool mara 2, kuwasuprise Chelsea kwa goli 4,
- Thomas Frank - Kama Silva ana timu ya Championshio lakini amekuwa na mbinu na style dhabiti iliyompa point za kutosha kuwa kwenye top 9 hadi sasa
- Klopp - ni kocha mzuri lakini mbinu zimemuishia hadi anastrugle kutoka kwenye midtable hadi nafasi ay 6
- Unai Emery - pamoja an kuipokea timu October ameweza kuitoa timu mkiani hadi nasfai ya 11
Nimejaribu kufafanua sababu za kufikria kocha anastahili kuwepo kwenye hiyo nafasi