Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Imebidi nicheke tu [emoji23][emoji23]
Hivi Cheltako ZOA ZOA FC mmeshakutana na Arsenal kweli
Saka hakabiki [emoji91][emoji91]
Xhaka wa moto
Nketiah kashindikana
Trossard kaingia kwenye mfumo
Odegaard ni iniesta mtupu
Msipopigwa 5 nipo pale
Beki kukulela kishingo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
1674499154321.png
 
UEFA SASA KUWEKA LIMIT KWENYE UREFU WA MIKATABA KUWA MIAKA MITANO (5)

Baada ya timu za EPL kulalamikia ujanja uliotumiwa na Chelsea kutumia pesa nyingi kusajili wachezaji wengi na kuwapa mkataba mrefu kama ule wa miaka 8.5 kwa Mudryk, UEFA wako mbioni kuweka mwisho wa mkataba kwa mchezaji kuwa miaka mitano tu.

Mabadiliko haya yataanza kutumiaka kwenye dirisha lijalo la kiangazi na hayo mabadiliko hayataadhiri usajili na mikataba iliyokwisha fanywa na Chelsea ila itazuia ujanja huo usiendelee kufanywa.

Sheria za sasa zina mwisho wa miaka mitano kwenye mikataba ila inaruhusu zaidi ya hapo kwa sababu maalum

Chelsea wametumia sababu hizo maalum kuwapa miaktaba ya muda mrefu wafuatao
  1. Marc Cucurella - £62m (Makataba wa Miaka 6)
  2. Wesley Fofana - £80m (Makataba wa Miaka 7)
  3. Carney Chukwuemeka - £20m (Makataba wa Miaka 6)
  4. Gabriel Slonina - £12m (miaka 6 na nusu)
  5. Cesare Casadei - £16.8m (Makataba wa Miaka 6)
  6. Pierre-Emerick Aubameyang. - £10.6m (Makataba wa Miaka 2)
  7. Mykhailo Mudryk - £88m (Makataba wa Miaka 8 na nusu)
  8. Benoit Badiashile - £33.7m (Makataba wa Miaka 7 na nusu)
  9. David Datro Fofana - £10m (Makataba wa Miaka 7 na nusu)
Mkakataba wa Mudryk umevunja rekodi ya kuwa mkataba mrefu kuliko yote katika historia ya EPL
Na pia gharama za usajili wa Chelsea wa msimu wa 2022/23 na huu wa January umevunja rekodi zote duniani za usajili

Chelsea hadi sasa imeshatumia £460m na bado usajili unaendelea
Matumizi hayo ya Chelsea imevunja rekodi ya msimu wa 2017/18, ambapo Man City walitumia kiwango cha takribani £330M kwa usajili.
 
UEFA kubadilisha sheria ya mikataba na kuweka mikataba mwisho wa miaka mitano(5) kuanzia msim ujao hii ni baada kuonekana kuna mwanya kwenye sheria ya sasa,lengo ni kufanya vilabu viendane na sheria za ffp.

Deal zote za Chelsea zilizokubaliwa kipindi hichi hazitokumbwa na sheria hiyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom