Lakini Mourinho msimu huu Mourinho anapenda sana 4-2-3-1.
Yah Mou anaupenda sn huo mfumo kwa sasa. Lkn timu nyingi msimu huu zimeonekana kuutumia huu mfumo sn!
zinatumia lakini tofauti na timu hizo na Chelsea ni kwamba Chelsea ina wachezaji 3 hatari sana katika eneo la viungo washambuliaji: Willian-Oscar-Hazard
Mkuu wangu Mentor asante kwa mchango wako!
Unajua unapotupia hivyo vitu vyako tunafurahi..Mimi na wadau wengine wa jukwaa hili tunataka Chelsea Fc thread iwe sehemu ya hoja za kitaalam muda wote;
cc: Ntuzu, Chivaro + wengine.
Kuna Kipindi Fc Porto ilikua juu sn! Wakati Wa akina Quaresma! Walikua wanacheza 4 3 3 vizuri sn.
Game mbili za UCL nusu fainali ilibidi Grant ampange Essien Beki Wa kulia kwaajili ya kumzuia Quaresma.
Lkn huyo Quaresma alivyokuja Darajani hakuonesha cheche Km alivyokua Fc Porto!
Hata ile mechi ya Barcelona vs Chelsea 2009 round ya kwanza kule Nou Camp Mikel na Ballack walicheza kiungo cha kukaba, Essien akacheza beki #2, wakati huo kocha wetu alikuwa mzee Guus Hidink tulitoka 0-0 mechi hiyo. Mechi ya Marudiano tukatoka 1-1 nyumbani Stanford Bridge. Goli la Essien dakika ya 16 lilikuwa goli bora la mwaka 2009 kwa timu ya Chelsea.
Nyie akina Ntuzu story zenu hata sizielewi kabisa....mfumo,mfumo huku mnachezea kichapo...hahaaaa, ngojeni tarehe 19 hapo
Lampard game ya j2 atacheza uwanjani baada ya kuumia misuri ktk game ya Ushindi ya 2 kwa 1 dhidi ya Liverpool. Na Ivanovic hatoweza kucheza hiyo game ya j2 ijayo!
Na mchezaji wetu mgeni Matic atacheza kwa muda Fulani ila hatoanza tangu mwanzo!
Lazima usizielewe kwasababu Filosofa ya mpira hauijui na Hasa ya Chelsea!
Kaa utulie une mpira Msafi siku hiyo!
Nazikumbuka Hizi game vizuri sn!
Tena game ya pale Darajani tulifungwa Hilo goli na Iniesta mpira dakika zikiwa zimekwisha kabisa na Refa akawa anaacha tu mpira uendelee!
Nakumbuka Mzee Guus alilalamika sn kwa refa kufanya hivyo!
Siku zote ukitaka kuifunga Chelsea lazima uifanyie Fitina mbaya ndo uishinde!
Huyo Siziga ana matatizo au ? Samahani sitaki kumdharau mtu lakini msimamo wa ligi unasemaje?
Timu zilizofungwa mechi chache: Everton = 2, Chelsea = 3, Arsenal = 3! Sasa tunachezea kichapo wapi na lini?
Hata msimu wa 1994 walikuwa wapi?epl au,kasomeni data sio mnashabikia chelsea wengi wenu baada ya Abramovich kununua timu,binafsi ninaamini wengi wa washabiki wa chelsea ni mamluki na wameanza kushabikia mwaka 2004,hata everton wanashika nafasi nzuri kila msimu na hawasajili majina makubwa.Angalia timu za uingereza uone ipi ni jembe kimataifa ndo uje useme hivyo!
Waulize Fc Barcelona au Fc B Munich au Waulize makocha wakubwa wote unaowafahamu duniani watakuambia mziki Wa Chelsea ukoje?
Miaka ya 1980 ilikua Miaka ya Liverpool
Na Miaka ya 1990 ilikua ya Man Utd
Chelsea ndio imevuruga zama za Arsenal Miaka ya 2000,
Na sasa ndio zama za Chelsea kwa Epl na Ucl.
Na Miaka yote hiyo tangu nyuma Chelsea sio Km walikua wanaburuza mkia hapana! Walikua wanashika nafasi nzuri tu!