Zifahamu tabia za thread za timu mbalimbali.
1. Manchester United hawa mashabiki wao asilimia kubwa wanaongelea usajili wa mchezaji fulani ukifanyika basi timu yao itakuwa bora. Hii ni trend toka aondoke Ferguson. Bahati mbaya wamesajili sana makocha na wachezaji lakini msiba haujaisha.
2. Manchester city wao ni mashabiki oyaoya, hawaujui mpira bali ni kelele nyingi kwasababu Guardiola anawapa mafanikio. Wengi wao ni wahanga kutoka klabu mbalimbali ambazo hazifanyi vizuri.
3. Arsenal ndio thread inayoongoza kwa uchambuzi wa mpira unaochezwa ndani ya uwanja. Wataalamu wote wa uchambuzi wa soka wapo pale. Pia ndio wanaongoza kupokea kejeli kutokana na kutofanya vizuri kwa misimu mingi ikiwemo kutobeba UCL wala Europa.
4. Chelsea wao thread yao imepambwa na malalamiko. Jamaa kila siku wako na lalamiko jipya. Kwa miaka kumi wamebeba karibu makombe yote makubwa lakini malalamiko hayaishi. Watamlaumu kocha, mmiliki, usajili m-bovu na hata timu pinzani.
5. Liverpool kwenye uzi wao utakuta wanaandika komenti ndefu sana lakini hamna cha maana zaidi ya kuwaongelea FSG, kiburi cha Klopp na majeruhi ya wachezaji. Wachambuzi wao wanapenda pia kutumia viingereza na huwa wanapotea kila timu inapofungwa na kurudi wakishinda.