Kumbuka maono yaliyopaswa kutekelezwa pale Chelsea ni ya Boehly na siyo Tuchel. Hivyo baada ya kutofautiana mitazamo, ilikuwa ni lazima Tuchel aondoke.
Mashabiki lazima tuujue ukweli kuwa Chelsea ya miaka ya 2011 - 2022 ilikuwa imejengwa on short term success. Hatukuwa na team ya kushindana hata misimu miwili mfululizo.
Mfano tulichukua champions league 2012 tukamaliza nje ya top four EPL.
2015 tukabeba EPL msimu uliofuata tulimaliza nafasi ya 10.
2017 tukabeba EPL msimu uliofuata tukamaliza nje ya top 4.
Inconsistency za namna hii zimekuwa zikiendelea msimu baada ya msimu.
Pia hata tunapoingia top four kuna kuwa na tofauti kubwa sana ya points kati yetu na wale top 2 kwenye ligi (Man City na Liverpool)
Katika kipindi hicho hicho ambacho tumekuwa na inconsistency, tumetumia hela nyingi kuwanunua Lukaku, Morata, Timo Werner, Tiemoe Bakayoko, Barkley, Ziyech, Pulisic, Sterling, Kepa Alizabaraga, Drink Water na wengineo ambao wamekuwa flop.
Kwa maana hiyo kuna ulazima wa kubadili namna ya uendeshaji club. Na suluhisho ni kujenga team ambayo inaweza kudeliver in a long term. Team haiwezi kujengwa ndani ya wiki sita. It takes time.
Graham Potter hajapata hata preseason moja na team.
Hajashiriki transfer window yoyote na Chelsea.
Ameingia clubuni wakati ambapo kuna mechi nyingi na wachezaji muhimu wakiwa injured.
Mimi nadhani tumpe GP transfer window mbili angalau. Hii ya January na ile ya Summer alafu tuone atakavyounda timu. Baada ya hapo angalau itakuwa halali kumhukumu.
Tukumbuke hata Guadiola msimu wake wa kwanza na City mambo hayakuwa marahisi. Kidogo tu timu isiingie top four.