Bobbyray
JF-Expert Member
- Dec 3, 2015
- 1,378
- 1,782
Umeongea Point TT anafanya wachezaji wanakuwa na presha sana wanakosa kujiamini kabisaOdoi asingeumia wakati wa Lamps angekuwa na confidence ya hali ya juu. TT hatakwepa lawama kwasababu ya kutoamini wachezaji wake. Anataka matokeo ya haraka. Ndio maana kamuuza Billy Gilmour. Hayuko tayari kumtengeneza. Ndege bila kukimbia runway haiwezi kunyanyuka. Kwanini Gallagher alipokuwa Palace alicheza vizuri na kwa kujiamini kuliko sasa? Kocha wake alimuamini na kumpa confidence. Wewe mwenyewe ulimuona Gallagher leo, decision making yake ilikuwaje. Kwanini akae na mpira hadi anaupoteza? Kuna vitu vingi vinatembea kichwani mwake: kwamba nikifanya hivi au vile huenda nitakosea. He wants to impress lakini hajui afanye nini aweke impression. Kocha yupo kwenye touchline anarap na kurusha mikono hewani kama anakemea mapepo.
Saka anaaminiwa na kocha wake. Anamwambia go and perform, enjoy your game. You've my backing. Unatarajia afanye vibaya? Hata hao under 23 ukiwatupa uwanjani umewajaza morali watafanya maajabu. Sisi kocha wetu ana mashaka saa zote, wachezaji wake watatuliaje. Labda sasa hivi kwenda mbele atatulia kwasababu amepata wachezaji aliowataka yeye.
Uliangalia game ya Aston Villa na Mancs? Uliona Gerald akibwekabweka hovyo? Aliwaaminisha wachezaji wake kwamba Mancs wanafungika ndio maana walijituma sana na kuwa na discipline ya hali ya juu.


