Je tunaviungo na wachezaj wale wale ambao wanaweza tupa hata nusu aliyokuwa anatupa Costa,Hazard,Willian,Matic,Fabregas
Nyuma pako sawa atleast, Luiz+Cahill+Azp
Na wing back hazina shida hizi idara zingine
Je kuanzia mid mpk mbele kuna mtu anaweza toa performance kama za hao hata nusu katika game 10 mfululizo??
Conte alicheza 14 games bila kupoteza, kwa kikos cha sasa unahis kinaweza cheza hata game 10 bila kupoteza??
Context haikuwa hiyo kwenye uchokozi wangu, context ilikuwa kuna madai kuwa Tuchel amekuta wachezaji wa makocha tofauti, Sari, Lampard hadi Conte
Na maelezo hayo yalibase hapo
Mbona Conte aliyakuta matakataka mchanganyiko na akayatumia kubeba kombe? hili swali haliitaji kukurupuka bali kupangilia hoja kwa sababu hata leo wachezaji tulionao sio wabaya kama tunavyoaminishwa. Tukumbuke pia kuwa style na falsafa ya kocha inaweza kuwainua wachezaji hawa na kuwapoteza /kuwaflopisha wachezaji wengine. TT alikuta wachezaji wa zamani na waliosajiliwa na FL lakini aliwainua viwango baadhi mmojawao akiwa ni Rudiger, Chilwell, James na wengine wakashindwa kuinua viwango. Kawatumia wachezaji hao kubeba UCL na kuipandisha timu hadi nafasi ya 3
Ukisema viungo Fabregas na timu nzima ilikuwepo iliposhika namba 10 2015/16
Mimi sitaki kuamini kuwa Willian alikuwa ni exceptional player, yule alikuwa just ordinary na aliwaudhi wengi sana kwa sababu ya mentality yake ya kutotaka kufunga magoli. So labda wa kumtaja hapo ni Fab na Costa tu, Luiz na Carhill walishachoka aliyekuwepo kwenye form ni Azpi tu. Tukubali kuwa style ya Conte inaweza kuwainua wachezaji wengi hata matakataka tofauti na style ya TT inataka wachezaji waliokwisha pikwa kwingineko ndipo waje kufanya vizuri na tena sio wote
So TT hadi aje kubeba ligi, lazima apatiwe wachezaji wa viwango vya juu tena waliokomaa kweli kweli kama akina Silva, Kou, Sterling, Kante, nk. Vinginevyo TT hawezi endana na wachezaji ambao hawajakomaa
Sababu kubwa ya kusema hivi ni kwamba TT hana mfumo mmoja wala style moja. anabadilika badilika
Siku moja nilijaribu kuwatofautisha makocha wanne na attributes zao
- PEP - mzee wa possessive football - hii falsafa binafsi siipendi kwa sababu inachosha kuangalia mpira wa naman hii kwa sababu ina sideways na back passes nyingi
- Klopp = mzee wa direct football, wachezaji wakirecover mpira ni mbele kwa haraka kwa ku break line hadi raha, inataka kufanana na counter attack. Mfumo huu hauchoshi kuangalia
- Conte = Mzee wa Counter attack, huu mfumo hauna pasi nyingi, pasi moja au mbili mfungaji wa tatu hadi raha
- Tuchel = Mzee wa tactics, uchezaji unabadilika badilika hata ndani ya mechi moja inawezxa mifumo na aina ya uchezaji ukabadilika. Hii style inasababisha hawa wachezaji wadogo washindwe kucheza vizuri consistently