Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Nimetokea kumchukia Ziyech kwa sababu sio professional na ndio maana kaachwa kwenye timu yake ya Taifa. ana utoto mwingi sana kama humjui. Hata anapocheza akifanya uzembe huoni akijutia kama kwa mfano Rudiger alivyokuwa. Yeye ni kama vile hajali. Yuko na goli akashoot nje yeye utamuona tu OK. Amezoea kucheza kwenye timu ndogo isiyo na competition ya namba sasa kaja Chelsea akiwekwa benchi kupisha wanaocheza vizuri yeye anaona anaonewa. Wacha aende AC Milan kule ataenda kufanywa mfalme kama alivyokuwa Ajax
Premier league ni ligi yenye high intensity wachezaji wegi inawareject sana, na wengi wana flop sio kwamba hawajui ni kwasabb hawezi kucope na intensity high, PL haina space ya mchezaji kuonyesha mbwembwe zake, ni kufunga na ku-defend,
 
Wapi ambapo kaonesha ataki kubaki chelseafc
Ziyech anaweza akaipa sumu dressing room. Mchezaji ambaye hajaridhika kabaki kunung'unika ni mbaya sana
Ziyech tangu mwaka jana alitaka kuondoka na kila akipewa nafasi hachezi vizuri kocha kaamua kuwarotate ili ampate anayecheza vizuri hakuna, Ziyech, Pulisic, Werner, Odoi na hao wengi wote wameshindwa kucheza kwa level ya kushindan na city na liverpool. Sasa yeye anataka tu yeyey ndie acheza hioyo right wing akipata majeruhi aje haraka haraka apewe kuanza , Chelsea is not Ajax ndio maana tunasajili wachezaji wengi ili asiwepo wa kukatia hati mili position labda acheze vizuri kuliko wenzake. Mimi naona sio afya kabisa kumng'ang'ania ZIyech. Mchezaji asiyeridhika anaweza kuichafua dressing room
 
Kama kusema uongo ni kutupwa kwenye lile ziwa la moto basi waandishi wa habari ndio watajazana huko kwenye moto

Mara utasikia De jong rulled out Man United
Mara utasikia De jong prefer Man United over Chelsea
Chelsea received a blow over Matthijs De Light
Matthijs De Light prefer BAyern Munich over Chelsea FC
Matthijs De Light is totally not aware of Chelsea interest
Matthijs De Light prefer Stanford Bridge over Allianz Arena
Ikaendelea uongo mwingi hadi kichwa kiume
 
Man United na Barcelona wamekubali kulipa ada isiyobadilika ya Euro milioni 65 pamoja na nyongeza ya Euro milioni 20 kwa Frenkie de Jong anayehamia Man United msimu huu wa joto.
Lakini licha ya makubaliano kati ya vilabu vyote viwili, hatua hiyo bado haijakamilika na hii ndio sababu:

1. De Jong anataka kuondoka Barca kwa vile ameambiwa na Xavi kwamba haanzii mbele ya Busquets na Pedri na Gavi wanapendekezwa katika safu ya kati kuliko Mholanzi huyo.

2. Frenkie de Jong hawezi kujitokeza na kusema anataka kuondoka Barca kwenda Man United kwa sababu ana haki ya kupata bonasi ya uaminifu ya Euro milioni 20. Ikiwa atalazimisha uhamisho huo, atapoteza bonasi ya uaminifu ambapo ikiwa Barca watamlazimisha nje, watakuwa na deni lake la kiasi cha Euro milioni 20 kama bonasi ya uaminifu ndiyo sababu Rais wa Barca Joan Laporta anajitokeza kwenye vyombo vya habari tena na tena akisema. klabu haimlazimishi De Jong kuondoka, badala yake wanataka kumbakisha klabuni.

3. Msimu wa 2019-20 Barca ilikumbwa na matatizo ya kiuchumi na ilibidi wapunguze malipo kwa masharti yaliyoahirishwa kwa wachezaji wao wote. Frenkie de Jong alikatwa mishahara iliyoahirishwa kwa 70% kwa misimu mitatu na Barca wanadaiwa karibu €19 milioni katika mshahara ulioahirishwa. Frenkie de Jong na wakala wake wanataka mshahara ulioahirishwa ulipwe kabla ya kukubaliana na masuala ya kibinafsi na Man United. Barca hawana pesa za kumlipa hadi sasa.

4. Frenkie de Jong hatakuwa mchezaji wa Barca msimu ujao, hata kama Barca wanataka hawawezi kuhifadhi nafasi yake kwenye kikosi kutokana na sababu za kifedha. Kwa mujibu wa mkataba wa de Jong mshahara wake utaongezeka kila msimu kwa €50k/wiki na pia ana haki ya kupata bonasi ya kila mwaka ya Euro milioni 5 kumaanisha ikiwa angebaki Barca atalipwa €400k/wiki na pia atapokea €19. milioni katika mshahara ulioahirishwa pamoja na bonasi ya uaminifu ya Euro milioni 20 pamoja na bonasi ya Euro milioni 5 kwa mwaka ambayo ni sawa na kitita cha euro milioni 62.3 ambacho Barca italazimika kumnunua msimu ujao na klabu haiwezi kumudu, kuna uwezekano wa Barca kutangaza kufilisika. ikiwa de Jong atasalia Barca.

4. Manchester United wana wasiwasi juu ya hali hiyo, hawataki kuharakisha na kulipa zaidi kwa mpango huu. Erik ten Hag anazungumza na Frenkie de Jong kila siku, mchezaji huyo anafuraha na yuko tayari kuungana tena na Hag kumi lakini hawezi kukiri waziwazi kutokana na sababu zilizotajwa hapo juu. Man United wana imani kuwa dili hilo litafanyika lakini linaweza kuchukua siku chache zaidi.

5. Barca itaanzisha mfumo wa pili wa kiuchumi tarehe 12 Julai kwa kuuza 49% ya haki zao za Bidhaa na Leseni kwa kampuni ya Marekani ya Fanatics ambapo watapokea €400 milioni kusawazisha akaunti zao na kutumia 20% ya mtaji huo kulipa mishahara iliyoahirishwa. ya wachezaji. Frenkie de Jong anasubiri Barca wamlipe mshahara wake ulioahirishwa baada ya hapo atajadili masuala binafsi na Man United na dili hilo litakamilika.

6. Frenkie de Jong atakuwa mchezaji wa Manchester United msimu ujao, kuna makubaliano kati ya Man United na Barca, ni suala la muda kabla ya Barca kulipa deni lao kwa De Jong na dili likasonga mbele.

KUMBUKA - BARCELONA HAINA CHAGUO NYINGINE BALI KUMUUZA DE JONG. NDIYE MCHEZAJI WAO ANAYE lipwa JUU NA KLABU HIYO ITATAKIWA KUMTUMIA Euro Milioni 63 MSIMU UJAO IWAPO WATATAKA KUMWEKA JAMBO AMBALO HALIWEZEKANI KWA MIZANI YAO.
FAKE NEWS
Over my dead body, De Jong aende kwenye dying team hata uwezo wa kusajili haina tena, hakuna mchezaji mzuri sasa hivi anaitaka Manure
 
Bayern wamefika paundi mil 76 kwa Matthijs De Light
Hata kama Delight ni mzuri Chelsea iachane naye kabisa
 
Ziyech anaweza akaipa sumu dressing room. Mchezaji ambaye hajaridhika kabaki kunung'unika ni mbaya sana
Ziyech tangu mwaka jana alitaka kuondoka na kila akipewa nafasi hachezi vizuri kocha kaamua kuwarotate ili ampate anayecheza vizuri hakuna, Ziyech, Pulisic, Werner, Odoi na hao wengi wote wameshindwa kucheza kwa level ya kushindan na city na liverpool. Sasa yeye anataka tu yeyey ndie acheza hioyo right wing akipata majeruhi aje haraka haraka apewe kuanza , Chelsea is not Ajax ndio maana tunasajili wachezaji wengi ili asiwepo wa kukatia hati mili position labda acheze vizuri kuliko wenzake. Mimi naona sio afya kabisa kumng'ang'ania ZIyech. Mchezaji asiyeridhika anaweza kuichafua dressing room
Wachezaji sumu ni wabaya sana katika jamii ya soka
 
Chelsea wanataka kumgeukia Dayot Upecano kule Bayern Munich
 
Mchezaji mwenyewe haipendi Chelsea kwanini tuna mlazimisha tutapata yale ya Lukaku, Raphinha sio world class top player, ni average playe kwa £60m is over rated wakati sokoni bado wachezaji wa wazuri na wa bei ndogo bado wapo wengi tu.
Hili siyo kweli. Raphina alishafanya makubaliano na Barca miezi kama mitatu iliyopita. Hivyo anaheshimu makubaliano aliyonayo tangu nyuma ya kujiunga Barca.

Ikumbukwe Raphinha alihitajika Barca ili kuziba pengo la Dembele endapo angeondoka klabuni hapo kama free agent. Ila kwa inavyooneka Bembele atasaini ili kubakia klabuni hapo Barca.
Kwa hiyo kitendo cha Dembele kubaki kinafanya usajili wa Rafinha uwe mgumu kwa Barca maana watakuwa wamemnunua mtu ambaye hatacheza katika first team kwa dau kubwa.

Uchezaji wa Raphina unafavour style ya Tuchel, mawinga ni wengi ila si wote wanaweza kupress from the front line.
 
Dembele kashasaini mkataba mpya wa misimu miwili, bodi ya Barca ndio inayosubiriwa. Nadhani kasaini tangu jana
 
Dembele kashasaini mkataba mpya wa misimu miwili, bodi ya Barca ndio inayosubiriwa. Nadhani kasaini tangu jana
Hii ndo inawafanya Barca wawe na kigugumizi kumsajili Raphinha ukizingatia pia Xavi anamtaka zaidi Dembele na siyo huyo Raphina anayetakiwa na board.
 
Hili siyo kweli. Raphina alishafanya makubaliano na Barca miezi kama mitatu iliyopita. Hivyo anaheshimu makubaliano aliyonayo tangu nyuma ya kujiunga Barca.

Ikumbukwe Raphinha alihitajika Barca ili kuziba pengo la Dembele endapo angeondoka klabuni hapo kama free agent. Ila kwa inavyooneka Bembele atasaini ili kubakia klabuni hapo Barca.
Kwa hiyo kitendo cha Dembele kubaki kinafanya usajili wa Rafinha uwe mgumu kwa Barca maana watakuwa wamemnunua mtu ambaye hatacheza katika first team kwa dau kubwa.

Uchezaji wa Raphina unafavour style ya Tuchel, mawinga ni wengi ila si wote wanaweza kupress from the front line.
Hapa ndio huwa tunawaambia wapenzi wa Zyech jinsi alivyo liability off ball likewise Dembele yaani wakipoteza mpira au wakiwa hawana mpira wanakabia macho kitu ambacho Raphinha kawazidi na ndicho kitu ambacho TT anavutiwa sana na Raphinha ile kuwa aggressive. Hapa ni kuombea Barcelona wamalizane na Dembele tu
 
Robert Lewandowski: Chelsea and PSG 'will enter race if Barcelona fail to sign striker'
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom