Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Kwa jinsi msimamo ulivyo. THE BLUES kumaliza nafasi ya 3:-

1. Tunatakiwa tushinde mechi 1 kati ya 2 zilizobaki au

2. Mechi 2 zilizobaki tuDRAW zote.

Tukifungwa mechi zote mbili zilizobaki tutamaliza nafasi ya 4.

HONGERENI THE BLUES KWA KUFUZU UCL MSIMU 22/23.

View attachment 2227641
Chief hata mimi nilidhani hivyo ila sio. Tunahitaji droo moja tu ili tubaki hapo kwenye tatu
Arsenal akishinda mechi yake anafikisha 69
Spurs akishinda mechi yake anafikisha pts 71 na GD ya 24+
Tukidroo mechi moja tunakuw ana pts 71 na GD41 or less
Ili Spurs atushinde kwa GD itabidi washinde mechi yao moja iliyobaki kwa mabao 15+ kitu ambacho sioni ikitokea
So one droo tunabaki hapo hapo, Droo mbili ndio tumeua kabisa
 
Hizo mechi 2 zilizobaki tutachezesha Academy players, tumeshafuzu UCL.

RUDGER, AZPLICUETA & CHRISTENSEN ruksa kuondoka.

Nasikia WERNER ameuambia uongozi anataka kuondoka.

ALONSO to Barcelona

JOGNHO to Juventus
Sasa ndio muda wa akina Marcus, GK,Xavier Mbuyamba, Sarr, Harvey Val, Bell, Lewis Hall kutamba
 
Abraham bado hataweza kufunga magoli mengi EPL
Ni striker mzuri ila kwa midtable team au timu za Europa kama Arsenal
Kule kwenye ligi legelege kafunga 15 tu
Angekuwa Chelsea kwa staili hii hata 7 asingefikisha
Mkuu hebu weka heshima kidogo kwa Abraham hata kama humpendi usisahau huyu dogo alifunga goli 15 za PL tena kwa kocha mbovu Lampard. Kadri anavyoenda anazidi kuimarika amini nawaambia ipo siku kila mtu atakuja kukubaliana na mimi hatukustahili kumuuza huyu dogo
 
Chelsea yangu bora ni ile ambayo ilianza msimu na kuongoza ligi kabla JAMES na CHILWELL kuumia.

JAMES na CHILWELL waliongeza nguvu kubwa sana kwenye ushambuliaji, ndio maana wakati ule Chilwell, James na Azpi walifunga magoli mengi kuliko washambuliaji wetu kule mbele.

James na Chilwell walivyopata injuries + Corona + injuries za wachezaji wengine + uchovu, timu ilipitia wakati mgumu sana kiushindani, mwisho kitu kizito kikatua kichwani baada ya Roman kutangaza anauza timu + vikwazo

Pamoja na changamoto zote hizo tumejitahidi kufika fainali mbili mfulilizo (CARABAO + FA), tunapambana kumaliza TOP 4. HONGERENI SANA

Binafsi naamini safu ya USHAMBULIAJI + KIUNGO imetuangusha sana msimu huu. Safu ya ULINZI nitailaumu kwa mistake ndogo ndogo ambazo utaziona kwa kuwa tulishindwa kufunga magoli mengi.

Kama msimu ujao tutaenda na viungo na washambuliaji hawa hawa tusahau kuchukua kombe la EPL mbele ya LIVER na CITY. TUSAHAU KABISA.

Ili kuboresha viwango vya wachezaji waliopo ni kuingiza maingizo mapya yenye ubunifu/uwezo mkubwa, nguvu na kasi.

Pale mbele tukipata winga 1 yenye uwezo wa kuassists 10+ na kufunga magoli 10+ anaweza kuwaamsha usingizini Kai, Werner na Lukaku. Winga mpya anaweza leta muunganiko flani ambao unakosekana kwa sasa.

Pale katikati tukipata kiungo mmoja mkabaji haswa, Kovacic na Kante wataoperate vizuri sana very comfortable. Jog, Saul & cheek watupishe.

Pale nyuma usajili wa mabeki sio chini ya watatu.

Kuna blanket la kocha TT tumejifunika nalo hatuoni nje, tunaona kwamba kwa sasa tunao wachezaji wazuri sana ila hawajitumi au viwango vimeshuka.

TUNAJIDANGANYA SANA, WACHEZAJI WETU WENGI WANA VIWANGO VYA KAWAIDA SANA.

Jiulize swali ni wachezaji wangapi wa THE BLUES wanapata namba kikosi cha CITY au LIVER?

Ile safu yetu ya ushambuliaji kule mbele hakuna mchezaji hata mmoja mwenye uwezo wa kuingia kwenye kikosi cha CITY au LIVER achilia mbali viungo na mabeki.

TUJENGENI TIMU YETU

#Pride of London

Kulingana na Mchanganuo wako Chelsea inahitaji £500M kuyafikia haya uliyoyazungumza.

Sasa Imagine tajiri atoe mpunga mrefu kuinunua Timu then at the same season atoe £500M za usajili.

#Impossible
 
Sasa ndio muda wa akina Marcus, GK,Xavier Mbuyamba, Sarr, Harvey Val, Bell, Lewis Hall kutamba
Sarr muondoe kwenye hiyo list huyu mchezaji ndio anatakiwa awe wa kwanza kuondoka kwenye team yetu
 
Sarr muondoe kwenye hiyo list huyu mchezaji ndio anatakiwa awe wa kwanza kuondoka kwenye team yetu
Hiyo list ni ya kumalizia msimu baada ya Chelsea kujihakikishia top 4, soma mwanzoni mleta mada alivyoandika
 
Kulingana na Mchanganuo wako Chelsea inahitaji £500M kuyafikia haya uliyoyazungumza.

Sasa Imagine tajiri atoe mpunga mrefu kuinunua Timu then at the same season atoe £500M za usajili.

#Impossible
Wewe umekuwa Marina sasa uanweza ukapata wachezaji wazuri watano hata kwa chini ya mil 200
 
GOOD NEWS
Serikali ya Uingereza na Abramovich wakubaliana kisheria na sasa Todd Boehly kupewa timu rasmi kabla ya Mei 31

Chelsea takeover 'on the verge of being approved' as 'Roman Abramovich's lawyers arrive at a solution which should satisfy Treasury officials' over a potential stumbling block to £4.25BILLION deal​

  • Chelsea's long-awaited takeover had been plunged into doubt over a £1.6bn loan
  • Reports now suggest a solution has been agreed, allowing the deal to go ahead
  • The Premier League are reportedly close to giving Todd Boehly the green light
  • A consortium led by Boehly have agreed terms on a £4.25bn takeover deal
 
Christopher Nkunku ana miaka 24 tu ana magoli 34 nachezea RB Leipzig ka forward, Ndie mchezaji bora wa mwaka wa Bundesliga, anauzwa paundi mil 60
hapo vipi
 
Christopher Nkunku ana miaka 24 tu ana magoli 34 nachezea RB Leipzig ka forward, Ndie mchezaji bora wa mwaka wa Bundesliga, anauzwa paundi mil 60
hapo vipi

Ni Sancho+Kai+Wener mwenye asili ya Kiafrika tu lakini hamuna kitu mule.
 
Leo Werner na Chirtasen hawatakuwepo
Kova na Kai 50/50
Werner ana tatizo la misuli
Kai wasiwasi ni fitness tu
Kova ana tatizo la kifundo cha mguu wake
Christansen hakucheza FA final kwa sababu za siri probably ugonjwa wa siri au kitu kingine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom