Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea sio kwamba ina wachezaji wabaya hilo nakataa ila ni mfumo wa kocha ndio kikwazo cha baadhi ya wachezaji kuonekana wabovu

Kama chelsea inamuhitaji zaidi Tuchel basi impe wachezaji watakaoendana na mfumo wake ambapo wakishindwa kupaform lawama ziwe juu yake

Hawa wachezaji walio Chelsea ambao mnaona wabovu wakienda timu nyingine watakuwa bora zaidi ya hapa nafikiri mifano mnayo Abraham aliyekuwa chelsea mbovu Roma kule ana goli zaidi ya 25

Hata kama tunataka kusajiri viungo lakini mjue jorginho bado atabaki kuwa kiungo bora umuhimu wake ni mkubwa tofauti na kante pamoja na kova ambao hamna msaada mkubwa waliotupa msimu huu
Sure, Jorginho ni wa muhimu, katika game anazokosekana unaona kabisq kuna tofauti in short chelsea isyo na jorginho ni kama day n night

Kante msim hajawa na kiwango kizuri,

Kovacic ni wamuhim akiwa fit,

Tammy ni poacher mzuri tu, kinachowakwamisha chelsea ni ukosefu wa creator, without a creator hata aje forward gan still atastruggle,
 
[emoji117]Chelsea yangu bora ni ile ambayo ilianza msimu na kuongoza ligi kabla JAMES na CHILWELL kuumia.

[emoji117]JAMES na CHILWELL waliongeza nguvu kubwa sana kwenye ushambuliaji, ndio maana wakati ule Chilwell, James na Azpi walifunga magoli mengi kuliko washambuliaji wetu kule mbele.

[emoji117]James na Chilwell walivyopata injuries + Corona + injuries za wachezaji wengine + uchovu, timu ilipitia wakati mgumu sana kiushindani, mwisho kitu kizito kikatua kichwani baada ya Roman kutangaza anauza timu + vikwazo

[emoji117]Pamoja na changamoto zote hizo tumejitahidi kufika fainali mbili mfulilizo (CARABAO + FA), tunapambana kumaliza TOP 4. HONGERENI SANA

[emoji117]Binafsi naamini safu ya USHAMBULIAJI + KIUNGO imetuangusha sana msimu huu. Safu ya ULINZI nitailaumu kwa mistake ndogo ndogo ambazo utaziona kwa kuwa tulishindwa kufunga magoli mengi.

[emoji117]Kama msimu ujao tutaenda na viungo na washambuliaji hawa hawa tusahau kuchukua kombe la EPL mbele ya LIVER na CITY. TUSAHAU KABISA.

[emoji117]Ili kuboresha viwango vya wachezaji waliopo ni kuingiza maingizo mapya yenye ubunifu/uwezo mkubwa, nguvu na kasi.

[emoji117]Pale mbele tukipata winga 1 yenye uwezo wa kuassists 10+ na kufunga magoli 10+ anaweza kuwaamsha usingizini Kai, Werner na Lukaku. Winga mpya anaweza leta muunganiko flani ambao unakosekana kwa sasa.

[emoji117]Pale katikati tukipata kiungo mmoja mkabaji haswa, Kovacic na Kante wataoperate vizuri sana very comfortable. Jog, Saul & cheek watupishe.

[emoji117]Pale nyuma usajili wa mabeki sio chini ya watatu.

[emoji117]Kuna blanket la kocha TT tumejifunika nalo hatuoni nje, tunaona kwamba kwa sasa tunao wachezaji wazuri sana ila hawajitumi au viwango vimeshuka.

TUNAJIDANGANYA SANA, WACHEZAJI WETU WENGI WANA VIWANGO VYA KAWAIDA SANA.

[emoji117]Jiulize swali ni wachezaji wangapi wa THE BLUES wanapata namba kikosi cha CITY au LIVER?

[emoji117] Ile safu yetu ya ushambuliaji kule mbele hakuna mchezaji hata mmoja mwenye uwezo wa kuingia kwenye kikosi cha CITY au LIVER achilia mbali viungo na mabeki.

[emoji117] TUJENGENI TIMU YETU [emoji123]

#Pride of London
Tukipata tu wachezaj 2+3 wenye uwezo wakutoa 10+ assist we are good. Na walio mbele wakaacha uchoyo

Tuchel akiendelea kuwepo na amini tunaweza compete na liver n city katika mataj, all we need ni kumsupport katika sajil, sio kuleta wachezaj ambao hawatak o hawaendan nae,

Katika fainal zote za FA n Carabao tulishindwa kuzimaliza hizi game, our player still wanaakili za kitoto kule mbele bar Havertz ila mount n pulisic katika carabao walitukosesha cup, jana pulisic karudia tena
 
Three wanataka kuactivate/revive udhamini wao kwa miaka miwili tena
Todd Boehly ana mpango wa kuwareplace na kuweka sponsor mwingine next season
Hawa Three wasepe tu tena sana, sisi tuko kwenye shida wao wanapress tuondoe logo yao kwenye jezi zetu
Theur are not royal sponsor, tena wapigwe ban kabisa wasilete pua yao huku darajani tena
 
Chelsea sio kwamba ina wachezaji wabaya hilo nakataa ila ni mfumo wa kocha ndio kikwazo cha baadhi ya wachezaji kuonekana wabovu

Kama chelsea inamuhitaji zaidi Tuchel basi impe wachezaji watakaoendana na mfumo wake ambapo wakishindwa kupaform lawama ziwe juu yake

Hawa wachezaji walio Chelsea ambao mnaona wabovu wakienda timu nyingine watakuwa bora zaidi ya hapa nafikiri mifano mnayo Abraham aliyekuwa chelsea mbovu Roma kule ana goli zaidi ya 25

Hata kama tunataka kusajiri viungo lakini mjue jorginho bado atabaki kuwa kiungo bora umuhimu wake ni mkubwa tofauti na kante pamoja na kova ambao hamna msaada mkubwa waliotupa msimu huu
Yaani wewe huijui Chelsea na wala Jorginho, Kante na Kova huwajui kabisa. Yaani Jorgninho legele unamp[a sifa hivyo kama vile ni meti wako wa geto
Kwa ufupi tu Kante umuhimu wake ni mkubwa sana, jana tu alipoingia ndani ya dakika 5 Chelsea ilianza kudominate hadi mpira unaisha kutoka kwenye possesion ya 32 hadi 48%
Kovacic usimlinganishe hata kidogo na Jorginho, Kova akiwa fit ni dribler mzuri na uwezo wake wa kupeleka mipira mbali unafahamika na fan yeyote wa Chelsea
Tunahitaji viungo bora zaidi lakini sio Jorgninho, not bad lakini sio level ya kiungo anayetakiwa
Mrithi wa Kante ni muhimu kwa sababu Kante habakii kuwa kijana, amezeeka na nguvu yake ya kuwepo uwanja mzima na kufanya recovery umepungua
 
Werner aliumia wakati wa warm up, au mlitaka aingie hivyo hivyo na majeruhi, kwa jinsi liver walivyokuwa wanacheza werner angekuwa mzima angecheza tu kulikuwa hakuna option
Angemuingiza hata kwa ajili ya penalti, Havertz kapotelea wapi?
 
Squad ya Chelsea ina quality ila imeshindwa kuadapt Tuchel's tactics, so timu inakosa balance & at times timu inalose form, Chelsea squad inafit vizuri wakicheza 433 kutokana na profile walizonazo but wanakosa DM (an orchestra) kama Declan Rice, taarifa zinaonesha chelsea wanamtrack Sangare.
Lampard na Sarri walitumia sana huo mfumo kwa merely wachezaji hawa hawa, tulitobolewa sana
In short we do not want that format. Conte ndani ya msimu mmoja alitumia 343 akatupatia kikombe
Timu inapokuwa na Wingbakc wazuri na inapokosa Viungo wakabaji wazuri, 343 ndio kimbilio
City na Liver wamefanikiwa kwenye 433 kwa sababu ya wachezaji waliopo, viungo wao ni wakabaji wazuri
Pia 433 au 343 inategemea kwa kiwango kikubwa na falsafa ya kocha. Kocha anapofundisha anawapanga na kuweka strategy zinazoendana na yeye anataka wachezaji wachezeje uwanjani
Mwalimu wa 343 ukamlazimisha afundishe 433 ni sawa na mwalimu wa English umlazimishe afundishe hesabu au fizikia

Kama TT yuko vizuri kwenye 343 tutaendelea na hiyo na tutasajili wachezaji wanaoendana na huo mfumo

Akija kocha wa 433 na tukapata wachezaji wanaoendana na huo mfumo tutabadili gia angani
 
[emoji117]Chelsea yangu bora ni ile ambayo ilianza msimu na kuongoza ligi kabla JAMES na CHILWELL kuumia.

[emoji117]JAMES na CHILWELL waliongeza nguvu kubwa sana kwenye ushambuliaji, ndio maana wakati ule Chilwell, James na Azpi walifunga magoli mengi kuliko washambuliaji wetu kule mbele.

[emoji117]James na Chilwell walivyopata injuries + Corona + injuries za wachezaji wengine + uchovu, timu ilipitia wakati mgumu sana kiushindani, mwisho kitu kizito kikatua kichwani baada ya Roman kutangaza anauza timu + vikwazo

[emoji117]Pamoja na changamoto zote hizo tumejitahidi kufika fainali mbili mfulilizo (CARABAO + FA), tunapambana kumaliza TOP 4. HONGERENI SANA

[emoji117]Binafsi naamini safu ya USHAMBULIAJI + KIUNGO imetuangusha sana msimu huu. Safu ya ULINZI nitailaumu kwa mistake ndogo ndogo ambazo utaziona kwa kuwa tulishindwa kufunga magoli mengi.

[emoji117]Kama msimu ujao tutaenda na viungo na washambuliaji hawa hawa tusahau kuchukua kombe la EPL mbele ya LIVER na CITY. TUSAHAU KABISA.

[emoji117]Ili kuboresha viwango vya wachezaji waliopo ni kuingiza maingizo mapya yenye ubunifu/uwezo mkubwa, nguvu na kasi.

[emoji117]Pale mbele tukipata winga 1 yenye uwezo wa kuassists 10+ na kufunga magoli 10+ anaweza kuwaamsha usingizini Kai, Werner na Lukaku. Winga mpya anaweza leta muunganiko flani ambao unakosekana kwa sasa.

[emoji117]Pale katikati tukipata kiungo mmoja mkabaji haswa, Kovacic na Kante wataoperate vizuri sana very comfortable. Jog, Saul & cheek watupishe.

[emoji117]Pale nyuma usajili wa mabeki sio chini ya watatu.

[emoji117]Kuna blanket la kocha TT tumejifunika nalo hatuoni nje, tunaona kwamba kwa sasa tunao wachezaji wazuri sana ila hawajitumi au viwango vimeshuka.

TUNAJIDANGANYA SANA, WACHEZAJI WETU WENGI WANA VIWANGO VYA KAWAIDA SANA.

[emoji117]Jiulize swali ni wachezaji wangapi wa THE BLUES wanapata namba kikosi cha CITY au LIVER?

[emoji117] Ile safu yetu ya ushambuliaji kule mbele hakuna mchezaji hata mmoja mwenye uwezo wa kuingia kwenye kikosi cha CITY au LIVER achilia mbali viungo na mabeki.

[emoji117] TUJENGENI TIMU YETU [emoji123]

#Pride of London
Chifu umeongea point zote ukweli mtupu ila kwenye hii ya blanketi mimi nina maoni tofauti
Viwango vya baadhi ya wachezaji kocha naye hatutamkwepa hata kama kocha kafanya vizuri
Viwango wa wachezaji wengi vingekuwa juu wangeweza kuingia kwenye lineup za city au liver ila sasa viwango viko chini kwa sababu kocha sio mkali hawasukumwi wafanye vizuri kama anavyofanya mzee kipara
Mimi naamini Werner ni bonge la mchezaji, Lukaku ni bonge la mchezaji hata kama hatafikia viwango vya akina Salah na Kane na Son. Mimi naamini Mount ni bonge la mchezaji, hivyo hivyo Kova. Naamini Havertz ni bonge la mchezaji. Kocha atumie mbinu na saa nyingine jeki kuwapusha hao watoto waamke
Mbone tuliposhinda UCL na pia tulipoanza ligi karibu kila mchezaji alikuwa anapata namba kule city na Liver?
Nakubaliana na wewe tusajili mabeki, wingbacks wa rotation, kiungo mkabaji kweli kweli ili hao viungo washambuliaji wawe na uhuru wa kushambulia. Nakubali tumsajili striker level ya Lewandowski. Pia Jorgninho, Cheek na akina Barkley na wenzake wakatumikie career zao kwingine nje ya Chelsea. Waongezwe hata kiungo mmoja mbunifu wa kushambulia. By doing so, Chelsea yetu itaweza sasa kushindana na akina Liverpool na City.

Kocha awe mkali kama Conte au PEP, wachezaji wengine wanapandisha viwango kwa fimbo hadi watakapokuwa watu wazima kwa maana wakifikisha miaka 24/25
 
Chelsea sio kwamba ina wachezaji wabaya hilo nakataa ila ni mfumo wa kocha ndio kikwazo cha baadhi ya wachezaji kuonekana wabovu

Kama chelsea inamuhitaji zaidi Tuchel basi impe wachezaji watakaoendana na mfumo wake ambapo wakishindwa kupaform lawama ziwe juu yake

Hawa wachezaji walio Chelsea ambao mnaona wabovu wakienda timu nyingine watakuwa bora zaidi ya hapa nafikiri mifano mnayo Abraham aliyekuwa chelsea mbovu Roma kule ana goli zaidi ya 25

Hata kama tunataka kusajiri viungo lakini mjue jorginho bado atabaki kuwa kiungo bora umuhimu wake ni mkubwa tofauti na kante pamoja na kova ambao hamna msaada mkubwa waliotupa msimu huu
Abraham bado hataweza kufunga magoli mengi EPL
Ni striker mzuri ila kwa midtable team au timu za Europa kama Arsenal
Kule kwenye ligi legelege kafunga 15 tu
Angekuwa Chelsea kwa staili hii hata 7 asingefikisha
 
Sure, Jorginho ni wa muhimu, katika game anazokosekana unaona kabisq kuna tofauti in short chelsea isyo na jorginho ni kama day n night

Kante msim hajawa na kiwango kizuri,

Kovacic ni wamuhim akiwa fit,

Tammy ni poacher mzuri tu, kinachowakwamisha chelsea ni ukosefu wa creator, without a creator hata aje forward gan still atastruggle,
Points zako ok ila kwa jo, dah, huyo kwa pasi ndio master ila pasi zake zinatufanya tumiliki mpira sana bila magoli. Tunahitaji viungo wa direct play with a lot of dangrous pass through passes. Tutawalaumu washambuliaji ila pia muda mwingi hawapati huduma ya mipira
Game ambazo mipira mingi inapelekwa mbele magoili yanapatikana, hata tu ile mechi na Leeds, kila mcheza alikuwa anapeleka mbele na tulipata magoli. Hii ya Jo ya back na sideways passes inaboa mashabiki mimi nikiwa mmoja wao
 
POINT

[emoji117] Binafsi naamini TT ni bonge la kocha kwenye TOP 5 ya makocha bora duniani anaingia.

[emoji117] TT amekuja Stanford Bridge akakuta timu yetu iko shangalabangala, ndani ya miezi 3 ametupa UEFA, SUPER CUP NA CLUB BINGWA WA DUNIA

[emoji117] Na msimu huu ametuingiza fainali mbili (CARABAO na FA) na tunapambana TOP 4.

[emoji117] Nadhani TT anazo sifa zote ndani ya vyumba cha kubadilishia nguo na uwanjani (Mbinu, styles, mifumo nk)

[emoji117] Staki kuamini kwamba TT ni weak kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Perfomance tulionyesha msimu wa mwaka jana, ilikuwa ya hali ya juu sana

[emoji117] Perfomance ile ilianzia kwenye vyumba vya kubadilisha nguo.

[emoji117] Naamini TT ana demand MORE and MORE kutoka kwa wachezaji ila kuna baadhi ya wachezaji uwezo wao ndio umefika mwisho.

[emoji117] SWALI:- Unataka kuniambia WERNER, LUKAKU kushindwa kuweka mpira wavuni ni kosa la TT?

Kosa kosa za PULISIC mbele ya goli ni kosa la TT?

[emoji117] Pamoja na nafasi wanazotengenezewa za kufunga wao wenyewe wanatumia jitihada gani za zaidi mpaka sisi mashabiki tuseme goli lile ni uwezo binafsi/ziada wa mchezaji?

Ndio maana nataka tusajili viungo wabunifu zaidi kwenda mbele tuone je kule mbele watafunga au lah?

[emoji117] Nitaendelea kusimama na TT uwezo wake wa kuwajenga wachezaji kisaikolojia, kimorale, mbinu zake ni EXCELLENT sana.

[emoji117] Niko against na baadhi ya wachezaji kwamba viwango vyao sio hadhi ya THE BLUES watupishe.
Tungekuwa na TT hapa tungemuuliza, UCL alifanyaje hadi wachezaji wakapanda viwango?
Najua kwa swali la kushuka viango moja ya jibu ni injuries kwa key players kama James na Chilwell
Najua pia itakuja swala la Corona ila hilo jibu ni weak kwa sababu hata timu zingine zilipatwa na janga hilo pia
Jibu lingine atasema ni Sanctions na uuzwaji wa timu, ila hilo lilitukuta tayari hatuka sawa
Kwa hiyo jibu la msingi ni Injuries
Sawa je injuries timu zingine au makocha wengine wanakwepaje?
Mim naona ni jukumu la kocha pamoaj na kiunua viwango vya wachezaji lakini pia kuja na mbinu na mkakati wa kupunguza injuries ili zisi affect performance ya timu.
Ukisema TT hana weak areas utakuwa husemi kweli. Yeye ni binadamu na binadamu yeyote anazo weknesses. Na tusipumbazwe na mafanikio aliyoyapata harakaharaka alipokuja mwaka jana, bado tuna matarajio makubwa kwake kwa kuwa Chelsea ni timu kubwa na matarajio ya timu kama Chelsea ni kubeba makombe mbalimbali.
Kusu swala la Lukaku, bado Kocha atabeba mzigo japo mzigo mkubwa na wa mchezaji au bodi. Labda uniambie kuwa TT hakumhitaji Lukaku. Kama alimhitaji basi alitakiwa kujua nama ya kumfanyia optimization ili afunge magoli kama Conte alivyomfanyia akiwa Inter
 
Hawa makocha ukiambiwa uwapange kwa ubora ungeanza na nani na ukaishia kwa nani na uondoe ushabiki.
  1. PEP
  2. Klopp
  3. Tuchel
  4. Conte
  5. Arteta
  6. Rodgers
 
MASWALI:-

1. Tangu atue TT tulishawahi kusikia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kuna ugomvi, matabaka, makundi?

2. Kuna mchezaji tulishawahi kusikia amepewa adhabu na kocha kwa uvunjifu wa maadili?

3. Je kuna wachezaji wameshatoka mbele ya camera wakasema hawakubaliani na mbinu za kocha au ni mbaguzi/upendeleo baadhi ya wachezaji?

Kwasababu hata press ya LUKAKU alisema amemiss Italy, angewish asingeondoka inter Milan

4. Tukimwangalia TT uwanjani anabehave vipi kwa wachezaji? Kuwakumbatia, kuwasifu, kuna mchezaji anayembagua? Haonyeshi kumpenda?
Hayo uliyoyataja hana ila bado point yangu iko hapa
Mimi namuona TT sio mpole sana lakini pia sio mkali wa kumfikia Conte au PEP au Klopp
Namuona pia sio demanding sana kuwafikia hao nilowataja
 
Naangalia mpira wa CITY hapa

WERNER & LUKAKU wakicheza CITY watakuwa butu zaidi ya THE BLUES.

CITY wanacheza na kushambulia kwenye space ndogo ndogo sana, kila mchezaji wa CITY wana uwezo + ubunifu wa hali ya juu kumiliki na kushambulia kwenye space ndogo ndogo.

LUKAKU anataka sebule nzima aweze kucheza, LUKAKU 1st touch yake mbovu sana, kwenye space ndogo ndogo atamtulizia adui mpira.
Ila Chief mchezo style yao mimi siupendi sana, uko so conservative na wa kukariri, wachezaji hawachezi kwa uhuru kabisa. Unaona wazi hizo ni notes za kipara wanabukua hadi uwanjani. Unachosha kwa vile una a lot of short passes, sideway passes na back passes. Hata kama fursa ya kucheza vizuri uko kwa mchezaji wa mbali hawatumii hizo fursa, hata kama muda umeisha unatakiwa kupeleka long balls golini wao wamekazana na short, side na back passes
Liverpool wana direct and free au uite open football ambayo inavutia hata kwa watazamaji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom