Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Hahahaha[emoji1787] umeua kaka. Sasa the blues tupo tayari kumlipa mshahara wa £450k kwa wiki?
ktk umri huo na kwa COVID-19 delta variant bado inashamiri hakuna klabu itamlipa huo mshahara, mwisho laki mbili tu angalau kwa misimu miwili ijayo akicheza kwenye ligi ngumu ili aprove consistency yake
 
Yaani unaongea useless mkuu, kwamba klopp ang'ang'anie mane n salah kwa sababu ya chelsea? Kwanza sisi wenyewe hatuna majigambo kama yenu ya kuwa tunakikosi kipana na hilo lipo wazi je' nyie wenyekikosi kipana?
Salah na Mane wakienda afcon, Liver inakuwa real fools, hawajui la kufanya mbele, mkibisha tusubiri tusiandikie mate ilihali wino upo. Kusanyeni points nyingi kabla jamaa hawajaenda Afcon tena nasikia wataenda wiki kabla kama ilivyopangwa kwa sababu ya Al ahly wanapush mashindano yaanze tarehe 3 January 2022 badala ya tarehe 9 January 2022, ikiwa hivyo Mane na Salah itabidi waondoke kabla ya ya mwaka mpya na hivyo kukosa mechi kati yake na Chelsea ambayo imepangwa kucheza Stanford Bridge tarehe 2 January 2022
 
Huyu dgo Gallagher ana hatari sana game ya leo ya Everton amefanya mambo ya hatari sana natamani January arudi kundini
Kuna watu mwanzoni niliwaambia huyu dogo ni hatari wakaponda, arudishwe tu. Tusije tukatumia pesa nyingi kuwanunua akina Havertz wakati tunao wanaomzidi Havertz kwa bure kabisa
 
Chelsea wanafikiria kumrejesha nyumbani Gilmour kutoka kwenye mkopo Norwich city endapo majeruhi ya viungo wa Chelsea itaendelea kuwa tatizo
Hivi sasa Chelsea inapwaya sana katikati kawa sababu ya kukosekana kwa Kante na Kovacic
Gilmour ni kiungo mzuri sana kwenye kukaba zaidi ya walioko sasa yaani9 Jorginho, Cheek na saa nyingine Mount, hata James ameshachezeshwa kwenye nafasi hiyo kwa sababu ya wenye nafasi kuwa majeruhi
 
Huo ni mtizamo wa utoto, mtoto kuchagua chakula ni jambo la kawaida lakini akishakua atashika adabu, Dotmund hawezi kubaki, Real Madrid wamefocus kwa Mbape, Bacelona ndio hiyo imejifia kwa sababu ya corona. Kuja Chelsea sio uchaguzi ni lazima, labda Chelsea wamkatae
Ndio tunamkataà na ssi
 
Mino Raiola sasa aigeukia Chelsea, nadhani anaiona Chelsea ndio pekee kwa sasa ina mahela ya kumninua Haaland
Sasa hivi timu zote zinazofanya vizuri hazina straika wa kusimama Chelsea ndo tunapofeligi kuchukua mastaika wa kusimama tuu

Hata huyo Halaand Chelsea watapoteza pesa zao bure tuu Kama kwa Lukaku
 
Sasa hivi timu zote zinazofanya vizuri hazina straika wa kusimama Chelsea ndo tunapofeligi kuchukua mastaika wa kusimama tuu

Hata huyo Halaand Chelsea watapoteza pesa zao bure tuu Kama kwa Lukaku
Kumbe kwa Lukaku fedha imepotea? Nyinyi Chelsea ndoo mlikuwa mnashangilia kwelikweli mnasema kila siku Lukaku atakuwa anaondoka na mpira?
 
TT alishapata utamu wa mfumo wa false no.9 (Kai Harvetz), mfumo ambao umempa makombe 2 makubwa.

Sasa sijajua kama ni yeye TT aliidhinisha striker asajiliwe, au uongozi ndio uliamua hivyo.

Kama TT alipitisha Lukaku asajiliwe, still bado hamtegenezei style ya uchezaji afunge magoli mengi sijajua shida ni nini?

Lukaku ni bonge la striker namba zake za kufunga magoli zinaonyesha hivyo.
Nani kakuongopea kua Lukaku ni bonge la mchungaji, mmepigwa hapo.
 
Hakuna mfumo wa kushambulia ninaouchukia kama stiker kusimama pale mbele kama mlingoti.

Mfumo wa kumtegemea stiker ndio afunge magoli.
Akikutana na timu au mabeki wenye kujua kumkatia striker RB ndio kazi imeisha hapo. Ni kweli ila bado kuna strikers wengi wenye uwezo wa kucheza kama wide winga na mfano mzuri ni Kane
 
Lukaku kufunga magoli ni TT kubadili mfumo utakaomtegemea Lukaku afunge magoli. Sioni TT akifanya hilo

Kwa mfumo uliopo sasa hivi wa kila mchezaji anafunga magoli sioni Lukaku akifunga magoli mengi.

Labda Lukaku abadilishe style yake ya uchezaji, acheze kama Kai Harvetz kushuka chini kuchukua mipira, kushambulia kutoka kushoto, kulia & katikati.

Ila akiendelea kusimama pale kwenye box lango amelipa mgongo, sorry kwake.
Mfumo wa TT ni wa kila mchezaji kuwa mobile, ndio maana unaona kiungo akikaba kama CB na CB akishambulia kama striker
Wingbacks wakicheza kama viungo washambuliaji na kadhalika
 
Lukaku kufunga magoli ni TT kubadili mfumo utakaomtegemea Lukaku afunge magoli. Sioni TT akifanya hilo

Kwa mfumo uliopo sasa hivi wa kila mchezaji anafunga magoli sioni Lukaku akifunga magoli mengi.

Labda Lukaku abadilishe style yake ya uchezaji, acheze kama Kai Harvetz kushuka chini kuchukua mipira, kushambulia kutoka kushoto, kulia & katikati.

Ila akiendelea kusimama pale kwenye box lango amelipa mgongo, sorry kwake.
Huyo Kai anafunga sasa mpka Lukaku abdli style ya uchezaji?
 
Leo ndo leo
20211213_113045.jpg
 
Yaani unaongea useless mkuu, kwamba klopp ang'ang'anie mane n salah kwa sababu ya chelsea? Kwanza sisi wenyewe hatuna majigambo kama yenu ya kuwa tunakikosi kipana na hilo lipo wazi je' nyie wenyekikosi kipana?
Majigambo yayoke wapi wakati kweli hamna kikosi kipana....

Imagine timu ukitoa wachezaji wawili tu kwisha habari yake...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom