Hazard
Willan
Pedro
Odoi
Vs
Ziyech
Pulisic
Odoi.
Kai ni false No.9, kumchezesha pembeni ni kucheza pungufu. Kai sio mchezaji wa kasi, nguvu na chenga kutoka pembeni kukatiza kulia au kushoto kuingia golini na kufunga/Assist
Pulisic kila siku yupo kitandani, tangu atue darajani 2019 hajawahi kucheza full mechi zaidi ya mechi 13 za EPL kwa msimu
EPL ni mbio ndefu jamani, tunamuhitaji Pulisic angalau acheze mechi 28 au 30 za ligi. Sioni Pulisic akifanya hilo.
Labda FA wapitishe sheria itakayomlinda Pulisic akiwa na mpira asichezewe rafu za miguu bali asukumwe kwa mikono
Wakati Ziyech kiwango kimeshuka kwa sasa, Pulisic ndio angeziba pengo, ila ndio huyo yupo kitandani muda wote.
Mount bwana mdogo, timu kubwa kama The BLUES kumtegemea dogo atubebe ni AIBU.
Dogo AMECHOKA sana ametumika mechi mfululizo tangu enzi la Lampard panga pangua, Achwe apumzike na kuendelea kujifunza.
Kai, Ziyech, Odoi, Mount mpaka sasa NO ASSIST TO Lukaku.
Tuchel afanyaje sasa apange viungo 3 (Jog, Kovacic, Kante) au awapange Ziyech, Kai pembeni tucheze pungufu?
Kwa sasa sioni ile safu ya ushambuliaji kule mbele ikitufungia magoli mengi bali namuona Lukaku kuanza kupata uhaba wa magoli.
Mimi naendelea kulia na usajili wa WINGERS Madrisha yajao ya usajili, tukipata Magoli 10+ na Assists 10+ kutoka kwa (LW + RW), itapendeza sana. Hapo LUKAKU lazima abebe Golden Boot