Tofauti ya Mount na wachezaji wa kiingereza ndo hii, pamoja na kubeba ubingwa wa ulaya akiwa na umri mdogo bado anaonekana mwenye njaa
Mwaka 2018 baada ya Dele Alli kutinga fainali ya UEFA na kutajwa kwenye kikosi bora cha ulaya cha mwaka huo alijisahau na kujiona amefika, mwisho aliishia kuponda raha kwenye fukwe za bahari na mwisho aliongezeka uzito, baadae alileta dharau mbele ya kocha Jose Mourinho mwisho aliozea benchi pale Spurs, now yuko wapi?
Wachezaji wengi wa kiingereza wana tabia za kujisahau hasa baada ya kufanikiwa kidogo, huanza vizuri mwisho huishia kusikojulikana.