Nimeipenda hiii....
Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone kuhusu Chelsea ya Thomas Tuchel; "Tulielewa ubora wao kwenye kucheza na nafasi. Mara zote wanakuwepo watu kwenye nafasi zao." "Nililipenda sana hilo na timu inayoweza kufanya mambo mengi. Walilionyesha hilo kwenye mchezo dhidi ya Man city. Waliwafunga Real Madrid kama walivyotufunga sisi. Tuchel amefanya kazi kubwa sana." "Tuchel ni kocha anayezuia au kushambulia? Ni timu inayozuia vizuri na inakupa presha kubwa kwenye kushambulia. Tulifikiri kwamba ni timu ya kawaida ambayo tumeshaiona hapo kabla." "Lakini walikuwa bora sana. Mechi ya marudiano walikuwa na kasi ya tofauti kabisa, walikuwa wanakufanya utengeneze nafasi. Jambo hilo tulilipenda sana." Unapigwa, unafundishwa na soka.....kuna watu wanaweza kusahau kwamba Suarez na ubora wake wote hakupiga shuti lolote[emoji23] #d1905_updates