Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Haya sasa kumekucha....wale 12 ambao tayari wameshamwaga wino kuitumikia European Super Cup ni hawa hapa:

AC Milan, Arsenal, Atletico Madrid, Chelsea, Barcelona, Inter Milan, Juventus, Liverpool, Manchester City, Manchester United, Real Madrid and Tottenham Hotspur tayari wanakulikana kama 'Founding Clubs'. (Waanzilishi)

Wengine ambao bado hawajaanguka saini ni ma giants wa Ujerumani yaani Bayern Munich and Borussia Dortmund pia na wale mastaa wa Ufaransa Paris Saint-Germain.

Huu mpango ni balaa kubwa!!
Je game zetu za kesho je nazo zimefutwa?
 
UTABIRI UTATIMIA KWA CHELSEA BAADA YA MIAKA TISA?

Mara ya mwisho 2012 Chelsea anabeba ubingwa wa FA na UEFA, Barcelona alicheza fainali ya Copa del Rey dhidi ya Bilbao, mwaka huu tena imerudia

Chelsea anafanya makubwa 2012, mchezaji wake Mwandamizi na tegemeo ambaye ni beki wa kati anaumia Raundi ya 16 UEFA alikuwa ni John Terry, mwaka huu ameumia Thiago Silva

2012 wakati Chelsea anatwaa UEFA, nyota Lionel Messi anakosa penati kwenye hatua za mtoano UEFA, mwaka huu pia Lionel Messi amekosa penati dhidi ya PSG kwenye mtoano UEFA

Wakati wanabeba UEFA na FA 2012, golikipa alikuwa Petr Cech waliomnasa kutoka Rennes na alikuwa na miaka 29 wakati huo, Mendy nae kajiunga kutoka Rennes na kwasasa ana miaka 29 hiyo hiyo

Kocha alietupa ubingwa alikuwa amezaliwa tarehe 29 ya mwezi ambaye alikuwa Roberto Di Mateo, mwaka huu pia Thomas Tuchel amezaliwa tarehe 29 kama Mateo na anaelekea vyema kwenye mbio

Msimu wa 2011/12 Man United walipigwa 6-1 na alitolewa Mchezaji kwa kadi nyekundu, msimu huu pia imejirudia United wamepigwa 6-1 na Mchezaji wao alitoka kwa kadi nyekundu

Mara ya mwisho Chelsea tumekutana na Guardiola nusu fainali, tulishinda FA na UEFA, msimu huu pia katolewa Pep na City yake tumeenda fainali ya FA na tupo nusu UEFA

Kwenye huo msimu wa UEFA 2011/12 Didier Drogba alikuwa na mabao sita, mawili ya kichwa, matatu ya mguu wa kushoto na moja mguu wa kulia, msimu huu pia Oliver Giroud ana mabao sita na takwimu kama hizo

Nahodha wetu alikuwa John Terry msimu wa 2011/12 na alikuwa na miaka 31, kama ilivyo sasa kwa Cesar Azplicueta nae ana miaka yake 31 pia

Tulipangiwa timu ya Hispania hatua ya nusu fainali ilikuwa FC Barcelona kwenye UEFA na msimu huu tumepewa Real Madrid kwenye nusu fainali ya UEFA

Mara ya mwisho fainali ya FA kuchezwa kabla EPL kuisha ni 2012 na Chelsea alikuwa bingwa na msimu huu Fainali itapigwa kabla ya EPL kutamatika na Chelsea tupo fainali

TUPEWE UEFA NA FA KABISA?



Hii hatari sana
 
Mchezo wa leo baina ya Leicester city na Southampton ni mbovu mbovu kwenda mbele. Kwenye fainal Leicester city wakicheza kama walivyocheza leo tunabeba kombe asubuhi na mapema

Ninachoamini Leicester tunaenda kumfunga hata awe kwenye form kiasi gani.

Ingawa ametufunga mara mbili msimu huu lakini kwenye fainal aesabu maumivu. Kaptain Azipilikueta na Thiago Silva hawawezi kubali ujinga huo
Kufungwa mara tatu ndani ya msimu mmoja no the Big noooo🤪🤪
 
Nyie mbwa tutakutana epl ..

Narudia tena haijaisha ,tunakutana epl ,na ndio tiketi ya kutoka top four ...

Tuanenda kuwatoa top four...

Mnagame na

Westham

Man city

Arsenal

Lecister city

Aston villa


Kudadek hamchomoki walahiiiii
 
Jamani mbona hamcoment chochote kuhusu MOU kufukuzwa au ndio damu ya undugu na Chelsea umeshaexpire?
 
Jamani mbona hamcoment chochote kuhusu MOU kufukuzwa au ndio damu ya undugu na Chelsea umeshaexpire?
Lilikuwa suala la muda tu Mourinho atafukuzwa kutokana na matokeo mabaya alikuwa anayapata na dalili zingine ni kupoteza game nyingi against big teams ndio maana hakuna hata mmoja ambaye ameshangaa.
 
Kosa kubwa alilofanya MOU ni kukubali kwenda kuifundisha timu isiyoweza kuingia sokoni. Mimi nilitegemea haya yatatokea kwa sababu MOU ana wachezaji wake asipowapata hatapata matokeo
Spurs walishindwa kumsajilia ma CB anaowataka na wachezaji wa kiunga wakabaji hata viungo washambuliaji hawana. Kane na Son wamekuwa wakicheza mara nyingi kama viungo ili kujitengenezea nafasi
Poor Spurs, sasa watakuwa mid table team wasipoajiri kocha mzuri zaidi
 
Ikiwa uefa wakafanikiwa, super leagu sidhan kama itaweza tokea labda washindwane kwenye makubaliano
IMG_20210420_180913.jpg
 
Kwa hiyo sasa kutakua na Super ligi na UEFA na UROPA?
Worry yangu ni kuwa hizi timu kubwa kwa muda mrefu walitaka UEFA wabadilike ili timu hizo ziwe na manufaa zaidi na hayo mashindani lakini hawakusikilizwa, sasa supa league imeanzishwa kama kuwakomoa UEFA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom