UTABIRI UTATIMIA KWA CHELSEA BAADA YA MIAKA TISA?
Mara ya mwisho 2012 Chelsea anabeba ubingwa wa FA na UEFA, Barcelona alicheza fainali ya Copa del Rey dhidi ya Bilbao, mwaka huu tena imerudia
Chelsea anafanya makubwa 2012, mchezaji wake Mwandamizi na tegemeo ambaye ni beki wa kati anaumia Raundi ya 16 UEFA alikuwa ni John Terry, mwaka huu ameumia Thiago Silva
2012 wakati Chelsea anatwaa UEFA, nyota Lionel Messi anakosa penati kwenye hatua za mtoano UEFA, mwaka huu pia Lionel Messi amekosa penati dhidi ya PSG kwenye mtoano UEFA
Wakati wanabeba UEFA na FA 2012, golikipa alikuwa Petr Cech waliomnasa kutoka Rennes na alikuwa na miaka 29 wakati huo, Mendy nae kajiunga kutoka Rennes na kwasasa ana miaka 29 hiyo hiyo
Kocha alietupa ubingwa alikuwa amezaliwa tarehe 29 ya mwezi ambaye alikuwa Roberto Di Mateo, mwaka huu pia Thomas Tuchel amezaliwa tarehe 29 kama Mateo na anaelekea vyema kwenye mbio
Msimu wa 2011/12 Man United walipigwa 6-1 na alitolewa Mchezaji kwa kadi nyekundu, msimu huu pia imejirudia United wamepigwa 6-1 na Mchezaji wao alitoka kwa kadi nyekundu
Mara ya mwisho Chelsea tumekutana na Guardiola nusu fainali, tulishinda FA na UEFA, msimu huu pia katolewa Pep na City yake tumeenda fainali ya FA na tupo nusu UEFA
Kwenye huo msimu wa UEFA 2011/12 Didier Drogba alikuwa na mabao sita, mawili ya kichwa, matatu ya mguu wa kushoto na moja mguu wa kulia, msimu huu pia Oliver Giroud ana mabao sita na takwimu kama hizo
Nahodha wetu alikuwa John Terry msimu wa 2011/12 na alikuwa na miaka 31, kama ilivyo sasa kwa Cesar Azplicueta nae ana miaka yake 31 pia
Tulipangiwa timu ya Hispania hatua ya nusu fainali ilikuwa FC Barcelona kwenye UEFA na msimu huu tumepewa Real Madrid kwenye nusu fainali ya UEFA
Mara ya mwisho fainali ya FA kuchezwa kabla EPL kuisha ni 2012 na Chelsea alikuwa bingwa na msimu huu Fainali itapigwa kabla ya EPL kutamatika na Chelsea tupo fainali
TUPEWE UEFA NA FA KABISA?