Mkuu unasema kweli kabisa. Halafu naona middle ya Kante na Jorginho haina mvuto kama ya Jorginho na Kova au Kante na Kova. Wakisimama Kante na Jorginho lazima mmoja awe juu zaidi ya mwenzake mfano juzi dhidi ya leeds Kante alikua na mchezo mzuri zaidi ya Jorginho lakini atakua mzuri akicheza na Kova.
Nadhani hata game ijayo dhidi ya Atlet lazima watacheza pamoja kwa sababu Jorginho nadhani atakua anatumikia adhabu ya kadi nyekundu so hata benchi hawezi kuwepo. Wewe unaonaje hiyo mechi?
Yes kuna namna fulani unaweza kuona double six ya Kante na Jorginho km haifanyi kz vzr lkn kuna kitu kimoja tunapaswa kutambua
Jorginho ni mzuri sn tukiwa na mpira na ktk kutoa pass.... Lkn sio mzuri tukitopeza mpira ktk recovery... Maana hana mbio kabisa na hana nguvu. Hiki ndio anachowazidi wenzake....
Wenzake ni wazuri sn kukaa na mpira na wana kasi sn ya kukimbia na wana uwezo mkubwa sn ktk kufanya recovery.... Lkn kutoa pass sn hasa za mwisho sio mafundi wao ni passes fupi fupi tu za move.
Nikija ktk game yetu ya juzi na Leeds... Leeds ktk huo mchezo walimlenga sn Jorginho hawakutaka kabisa achezee mpira au aguse mpira.
Alikua kila Mara lazima aangushwe chini asukumwe afanyiwe kila aina ya dhuluma ilimradi tu wasijipange au kutoa pasi ndefu za hatari... Maana km unawaona siku hizi Chelsea wamebadilisha mfumo kidogo... Hawakabii juu ktk half ya adui wanakabia mita 30 mpk 45 ktk eneo lao ili kutengeza magepu kwa adui na kuweza kufunga maana ile pressing ya juu na kumiliki mpira kule kunazifanya timu pinzani kucheza deep na timu kushindwa kabisa kufunga... Sasa Jarginho anacheza kwa chini kabisa ili apate uwanja mpana wa kutupia mipira ktk magepu ya wazi km kwa Meson Mount na Ziyench... Sasa timu pinzani zimeliona hili ndio zina muandama kinouma. Kila akigusa mpira tayari wamefika na kumchezea rafu....
Lkn Pamoja na yote haya, wakimdhibiti Jorginho wanampa nafasi Kante ya kutembea na mpira mbele maana anao huo uwezo na juzi tumeona namna alivyoweza kukimbia huko na kuko na kutengeneza move nyingi tu za nafasi...
Turudi ktk game na ATM....
Siku hiyo lazima ktk double six wasimame Kante na Kovacic... Yaani hii ni combination ya hatari sn.... Wote wana uwezo wa kukimbia na kukaa na mpira. Kufanya tackle, interception na recovery...
Yaani nakwambia mkuu leo j5 hawa jamaa watakimbia Km kila mmoja karibu 14... Wataivuruga kabisa ATM siku hiyo maana najua Diego Simeon atakuja na hasira km nyuki. Yaani watatupigia mpira wa nguvu mno siku hiyo... Tunahitaji kua imara sn siku hiyo. Watu km kina Alonso na James na Rudiger na Christiansen na Azpilicueta wanatakiwa kua imara sn na si kukurupuka... Tunatakiwa kufanya high pressing siku hiyo kuwazuia kabisa hawa jamaa ktk half yao. Odoi na Pulisic na Ziyench wakipewa nafasi siku huko mbele wasilete ujinga kabisa maana ATM wakipata goli tu basi wanakua wamepindua meza....
Sina mashaka na Giroud au Timo au Kai km watapangwa huko mbele. Mimi hawa attackers tu wanao wasaidia ndio shida yng yaani wapambane kweli kwsbbu dogo Mount siku hiyo hatokuwepo
Itakua ni game nzuri na ya ushindani na inapendeza kutazama sn....