"IN FRANK WE TRUST - Then. Now. Forever." Hiyo ni banner mpya iliyowekwa pale Darajani na kuonekana katika mchezo dhidi ya Luton. Watu mbalimbali wanaamini kuwa Lampard hakupaswa kufukuzwa mapema namna hii, ata boss mwenyewe kasema ulikuwa ni uamuzi mgumu mno.
Binafsi nilipenda sana hili jambo litokee, unajua baada ya kupata taarifa hizi sikuamini kabisa toka kwa mtu alie niambia. Ila baada ya kudhibitisha kuwa ni kweli ghafla nilimuonea huruma Lampard hii huenda ni kutokana na u legend wake.
Naam ni dhahiri kuwa Lampard ilipaswa afukuzwe, ila kitendo cha kumleta Thomas Tuchel kuchukua nafasi ya Lampard ni kuonyesha kuwa Chelsea wanakurupuka sana. Niseme hapa hapa mapema kabisa ili kwa baadae msije mkasema Chelsea ina plastiki fans, huyu Tuchel HAFAI kuifundisha Chelsea. Hakuna kocha mle ni utopolo kabisa.
Kocha anaetufaa kwa soka la sasa ni Julian Nagelsmann, huyu Nagelsmann ni kocha sahihi hasa kwa soka la kileo. Japo kuna taarifa kuwa hapatikani kwa sasa mpaka mwishoni mwa msimu huu, kama hizo taarifa ni kweli basi Lampard asingefukuzwa mpka mwisho wa msimu kicha akachukuliwa Nagelsmann. Real Madrid nao naona wanamtaka huyo kocha.
Ila hapa kwa Tuchel hakuna kitu kabisa