Katika mechi ambazo Ziyech alicheza chelsea walikua na 86 winning percentage. Baada ya majeruhi sasa hivi chelsea ina 33 winning perecentage.
Ziyech siyo kiungo mshambuliaji, ni winger wa kulia. Hii inamaanisha chelsea inategemea crosses kuliko hata ubunifu. Ndiyo maana wengi huona uwepo wa giroud utaleta magoli as giroud hurespond faster kwenye krosi.
Ambaye anatakiwa afanye ubunifu ni kai havertz. Yaani ni kwamba ilitakiwa mtengeneza chansi na mtoa pasi za mwisho awe kai. Ilitakiwa uwepo wa kai uongeze asilimia za ushindi na siyo ziyech.
Maajabu yake mchezaji aliyetengeneza chansi nyingi chelsea ni mason mount, anasemwa vibaya na mashabiki lakini anafanya kazi anayoishindwa kai kwa ufasaha, na hata siyo namba yake. Grealish anaongoza kwa kucreate chances, 51, huku mount akiwa 4 na ametengeneza chansi 34. Wa kwanza mpaka wa tatu wote ni AM.
Werner hajascore game ya 10 mfululizo. Kai ana assisst moja tu. Magoli ya giroud mpaka leo ni mengi kuliko jumla ya magoli ya werner na kai. Wameshaingizwa kwenye worst summer signings.
Nilisema werner siyo mzuri kutokea huko mbali kuna mwenzenu akawa anabisha ila mwaka ambao amescore sana mpaka mnamsajili ni mwaka ambao mbele alichezeshwa na forward mwingine. Yaani werner anaweza akaperform vizuri akiwa burnley kuliko chelsea kwa formation ya sasa.
Kama kawaida ya matatizo ya chelsea yanavyotatuliwa kocha kaomba mpunga mwingine. Jiandaeni kusifia watu wapya.