Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Hizo hattrick atafuta huko carabao siyo EPL mazee mmepigwa pale leo mnajifariji ila kwa magoli aliyofunga pia ni zawadi za wale Barnsley tu
 
Harvertz vs Ronaldo .. harvertz is best he scores hattrick vs Barnsley
 
Chelsea: 6 league title
1 champions league
2 europa league
8 fa cup
4 fa Community shield
1 uefa super cup
2 uefa cup winners cup
1 fifa club world cup
5 carabao cup
Man united: 20 premier league
3 champions league
1 europa league
13 fa cup
21 community shield
1 super cup
1 uefa cup winners cup
1 fifa club world cup
1 continental cup
Should i continue
 
Mkuu sasa hapo kwenye mechi 2 za ligi yao wanashika hyo nafac ndo inamaanisha hyo ni nafac yao...? Au nyumbu kushika nafasi ya 16 huko ndo inamaanisha ni nafasi yao?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nafasi waliyomaliza msimu uliopita haina tofaut Yani nafasi zake humo humo tu hii hapa ni last season alivyomaliza
IMG_20200924_001652_022.jpg
 
Maoni yangu juu ya Che vs Ban jana kwa ushindi wa 6-0 pale Darajani
  • Cleansheet jana Caballero kaisotea kwelikweli na kwa udakaji ule, Cabalero ni GK bora kuliko Kepa, Jana alicheza vizuri sana
  • Tammy abraham jana kakopi staili ya Giroud katoa assists nzuri takriban zote alizofunga Havertz
  • Kwa maoni yangu Fikayo Tomori na Odoi bado hawajafikia standard ya kuwa kwenye first team. Bado wana makosa ya kijinga jinga. Mfano kutoa pasi kwa opponents mara nyingi bila kujirekebisha tena saa nyingine kwenye maeneo ya hatari yenye kusababisha counter
  • Magoli ya jana ya Havertz yanaonekana marahisi lakini yalitoa picha kuwa Havertz anarudi kwenye ubora wake taratibu na pia kwa vile Kocha alimpanga kwenye nafasi ya CAM ambayo wengi wanaona kama ndio best position kwake
  • Thiago silva jana kafanya blunder moja ya kukosa concentration na kama hao Barnsley wangekuwa na akina Mane, tungefungwa kupitia blunder ya Silva. Bado anahitaji kupewa muda ili awe fit kwenye EPL japo jana alionyesha kuwa uzoefu wake utatufaa sana
  • Staili ya uchezaji wa Kovacic hafai kukaa benchi kwenye mechi zote labda awe majeruhi
  • Mount naye akicheza nyuma kama attacking midfield ni mzuri sana, anaonyesha dalili za kuja kuwa the next Fabregas, anaona chances za mbele na anajua kutoa pasi nzuri
  • Barkley ni clinical finisher mzuri, napenda jinsi anavyopiga makombora golini, akiongeza kasi kwenye kutoa pasi atafaa kwenye first team. Kosa lake tu ni mzito kwenye kukaa na mpira
  • Kwa ujumla utatu wa mbele wa Mount, Abraham na Havertz ulisababisha kwa sehemu kubwa yale magoli 5 kati ya 6
  • Kwa jinsi nilivyomuona Ben Chil alivyotoa krosi ile ya goli la Giroud, Atafaa sana kuliko hao LB wengine tulionao, Mimi namuona Chilwell kama anaona fursa za mbele kuliko Alonso au Emerson
 
Nazani sasa hvi mashabiki wa chelsea tumeanza kuongea lugha moja...

Huko nyuma nishawahi kumzungumzia loft cheek, kuwa ni miongoni mwa wachezaji wa ovyo ..

Hajawahi kuwa na kiwango kizuri kwenye msimu mzima.. Tangu hatue chelsea
 
CHELSEA 6-0 BARNSLEY, League Cup: Post-match reaction

Uwekezaji wa £89M ilikumnasa Kai Lukas Havertz umeanza kuzaa matunda. Kijana ameanza ku adapt baada ya kutupia brilliant hat-trick nakuiwezesha Chelsea FC kufuzu katika Carabao Cup round ya nne.

Tammy Abraham alikuwa wa moto , hakuwa mchoyo but alimtengea Kai Lukas Havertz mayai mawili huku akiwachakaza Barnsley kwa bao safi.

Chelsea tungeweza kupata bao la kuongoza ndani ya dakika ya kwanza ya mchezo, but Barnsley waligoma kabisa kuchinjwa. Kabla ya kimbunga kuanza, Barnsley walikuwa wamepiga mashuti ya kutosha na kumfanya Willy Caballero kuokoa michomo kadhaa.

Tammy Abraham alihitaji dakika kumi na tisa pekee kuwachana Malinda Barnsley baada ya kufanya clinical finishing dakika ya 19. Kai Lukas Havertz akigongea touches tamu tamu na wakali wenzake dakika ya 28 alituweka mbele kwa kugunga bao safi na kuupeleka mchezo half time ukiwa Chelsea 2-0 Barnsley.

Second half ilikuwa different story kwa Chelsea baada ya kutupia mawe mawili kupitia kwa Ross Barkley dakika ya 49 na baadae Kai Lukas Havertz dakika ya 55. Mwamba Thiago Silva alihitimisha siku yake akiwa amecheza dakika 60. Kai Lukas Havertz yeye alihitimisha siku yake kwa kufunga bao la tatu lililokamilisha hat-trick dakika ya 65. Kimbunga cha mabao kilihitimishwa na Oliver Jonathan Giroud akipokea cross safi kutoka kwa Chilwell dakika ya 83.

Frank Lampard alikuwa amefanya mabadiliko yakutosha huku akiwaacha Mason Mount, Kai Lukas Havertz, pamoja na Mateo Kovacic wakiwa ni wachezaji pekee waliokuwa katika game ya weekend iliyopita.

Ilikuwa ni debut kwa Thiago Silva huku Tammy Abraham, Callum Hudson-Odoi, Ross Barkley na Willy Caballero wakipata airtime za kutosha.

FB_IMG_1600920625085.jpg
 
Hizo hattrick atafuta huko carabao siyo EPL mazee mmepigwa pale leo mnajifariji ila kwa magoli aliyofunga pia ni zawadi za wale Barnsley tu

Mkuu mbona mnateseka na ushindi wa Chelsea. Chelsea akishinda tatizo, akifungwa tatizo, Heverts akipiga hat trick nayo tatizo. Mbona ninyi mmecheza na timu ndogo lakini wachezaji wenu wameshindwa kufunga hata 3 goals
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom