Kweli kabisa LAMPARD alipewa timu katika mazingira magumu kama:-
1. Hazard aliondoka
2. kuondoka Babu Sari (Kocha mpya kwa wachezaji)
3. Ban ya kutofanya usajili.
4. Uchanga wa Lampard Epl kama kocha
Tuseme ukweli Mungu anatuona, sidhani kama kuna shabiki yoyote wa Chelsea duniani alitegemea timu ingemaliza TOP 4, NEVER.
Mbio za kumaliza Top 4 zilikuja baada ya kuona tupo tupo top 4 muda mrefu, tukapata matumaini tunaweza maliza nafasi za juu.
Jamani Mnyonge mnyongeni haki yake tumpe. Kumaliza TOP 4 ni mafanikio makubwa sana kwetu kwa changamoto tulizopitia msimu huu.
Tumesajili wachezaji wapya msimu ujao ndio tutaanza kuupima ubora wa Lampard. Na hata hivyo tusitarajie sana ubingwa mi naona target iwe kumaliza ndani ya Top 2, Msimu ujao 21/22 tupambanie ubingwa.
Halafu Lampard karekebisha madhaifu mengi hasa yaliyoonekana kwenye mechi ya kwanza a Manure ya kupress high na kuacha void katikati mapaka viungo wa timu pinzani kupata mwanya wa kufanya counter.
Falsafa yake ya mwendo kasi inafanya mpira uvutie tofauti na mzee Sarri. Ujio wa akina Werner, Ziyech, Chilwell, Havertz, Silva, uwepo wa mkata umeme Kante na form nzuri ya Gilmour Pulisic, Mount, Kovacic na akina Odoi, Zouma wanaonyesha kuimprove utaifanya Chelsea msimu huu tusiwe na pressure na top 4 na silverware tutapata, hilo halina shaka
Mwaka jana wengi walitutabiria nje ya top 6 na wengine kutupeleka kwenye mid-table kabisa, lakini Lampard kawashangaza kwa kuipeleka timu top 4
Wengi wanamfananisha kimafanikio, Lampard na Sarri kwamba Sarri kaiwezesha timu kushika nafasi ya 3 na pia kabeba Europa
Bila kuzingatia kuwa alikuwepo playmaker Hazard na pia Sarri yeye alishiriki Europa mashindano ya vibonde wakati Lampard kashiriki UCL mashindano ya mabingwa
Pia hawakumbuki kuwa Chelsea na Man U ni kama wameshare nafasi ya tatu kwa maana ya points, Chelsea ana 66 na Man u 66
Pia wanasahahu kuwa Sarri hakuwa na majeruhi through out. Lampard karidhi timu yenye majeruhi wengi akiwemo Kante, Odoi na RLC ambao walianza kukiamsha kandanda safi.
Mimi naamini msimu uliopita ulikuwa ni pre-season kwa Lampard na sasa ndio anaanza ligi akiwa ameijua vizuri EPL kama kocha, mbinu na mikakati. Ni kocha kijana na mwenye akili sana.
Ndio maana EPL walimpendekeza kama kocha bora wa msimu, wao waliona mafanikio ambayo baadhi yetu hatuoni
IN LAMPARD WE TRUST