Umeongea point ndugu
Hawa academy hawana consistency kabisa. Wengine tuliwasifia wakati ule hatukuruhusiwa kusajili. Sasa tumefunguliwa tuwalete wachezaji kamili world class wenye kuamua matokeo dressing room.
Ukiangalia Bayern ya mwaka huu wako fit kila idara kwa nguvu, kwa skills, kwa mentality na kwa umakini vitu ambavyo Chelsea haipo kabisa
Kwa mechi ya jana na zinginezo nimegungua pia kukosekana kwa kiongozi kama Teri, Azpi anajitahidi sana ila jhajafikia leadership ya Tery hasa kule nyuma. Defenders wote wanakaba sana ila bila kutumia akili. Magoli ya jana vichekesho tupu hata siwezi kuelezea. Kepa sas naanza kumuelewa, Mabeki wetu hata kujipanga kukaba hawajui utafikiri hawajafundishwa.
Hii timu kwa ujumla ni ya kusafisha yote
Hata kule mbele Pulisic asipokuwepo wa kupiga chenga hatuwezi funga magoli. Ukiangalia jana Bayern hawakuwa wanapiga chenga kama Pulisic. Walikuwa wanapanga kufunga, wachezaji wanapelekwa mpaka wanappoteana halafu Lewandowski au Perisic anafunga kiulaini.
Mamanegement isajili wachezaji waliokamilika, wanaofundishika, wenye tallent binafsi na ambao ni professional.
ACADEMY wanafaa sana kwa sub, timu B na potentials za baadaye wakikomaa kama akina Tomori na Mount
Kwa maoni yangu benchi lote la defense tunahitaji kusajili first team
Katikati tunahitaji kiungo mfungaji na mtoa assists double digits kila mwaka kwenye magoli na assists. Ziyech anaweza hiyo kazi
Tuwapate winga calibre ya akina sancho, rahim. Tuwapate mabeki wa kumlinda kipa na tupate kipa world class. Nahisi kwa mahitaji haya, Bado Chelsea itaendelea kujengwa 2020/21
Aajiriwe fundi wa mabeki kama John Tery