Ziyech anacheza vizri CAM, hii nafasi CAM kwa sasa wanacheza Mount na Barkley na RLC ambao hawatoshi kwa maoni yangu. Kama tukitaka kujenga wide scope team basi tuwe na wachezaji wengi wenye kutumainiwa kama mwingine hayupo kwa sababu ya majeruhi au kuchoka mwingine aweze kucheza mfano Pulisic sio wa kumtegemea sana kwa sababu anaumia mara kwa mara, Odoi pia, Kante pia nk. Kumbuka ukweli ni kwamba timu haitaweza kunuanua wachezaji wote wazuri wanaotakiwa kwa msimu mmoja, Taarifa za ndani ya Chelsea zinadai kuwa Willian bado ni winga mzuri kwa suluhisho la muda mfupi. Odoi bado anapanda mlima na mpaka afikie kiwango cha kumtumainia Willian hatutakuwa nae tena
Sababu kuu ya Willian abaki anaendana na Lampard ambacho ni kitu cha msingi kwenye kujenga timu. We angalia Conte na Diego costa, pamoja na uzuri wa Costa lakini chemistry ilikataa kama ambavyo Willian chemistry ilikataa kwa Conte na Sarri. Kwa uchezaji wa Willian, Timo atafaidika sana. Mimi naamini bado Willian atatufaa sana kwa mkataba wa miaka miwili wakati tunatumia nguvu kujenga namba zingine zinazopwaya kama GK, LB, CB
Inavyoelekea Lampard atakuwa akitumia zaidi Back five ambayo inaonyesha vipawa viko vingi hasa za Alonso na Reece James wakicheza kama Wing-backs
Kwa formation ya 3-4-3
Pulisic/Kai Havertz/Mount - Timo/Giroud/Tammy - Ziyech/Odoi/Willian
Bill Gilmour/Jorginho ----------------------------- - Kovacic/Kante
Alonso/LB mpya -----------------------------------------------------------------------------------James
Zouma/CB mpya ----- Rudiger/Christensen ------- Azpilicueta
GK Mpya/ Cabalerro
Kwa formation ya 4-3-3 (4-1-2-3) CAM wawili na CM mmoja
Pulisic/Mount - Timo/Giroud/Tammy - Odoi/Willian
Kai Havertz/RLC ------------------------------------------------------------------- Ziyech/ Kovacic
Bill Gilmour/Kante/Jorginho/
Alonso/LB mpya ---------- Zouma/CB mpya --------Rudiger/Christensen ------ Azpilicueta /James
GK Mpya/ Cabalerro
Kwa formation ya 4-3-3 (4-2-1-3) CAM mmoja na CM wawili
Pulisic/Kai Havertz - Timo/Giroud/Tammy - Odoi/Willian
Ziyech/Mount
Kante/Jorginho ---------------------------------------------------------- Bill Gilmour/Kovacic
Alonso/LB mpya - Zouma/CB mpya - Rudiger/Christensen - Azpilicueta /James
GK Mpya/ Cabalerro
Akina Ziyech, Kai, Mount, RLC, Willian wanaweza kucheza namba nyingi kwa hiyo hiyo niliyotoa ni sample lineup tu
Kumbuka pia namba muhimu inatakiwa kuwa na wachezaji watatu au kama kuna wa kusiwtch kama nilivyosema, striker kwa mfano ni lazima wawe watatu, mmoja akiumia wa wepo wawili mmoja wa kucheza na mwingine wa sub