DullyJr
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 13,993
- 11,871
Mfundishe huyo kilaza aelewe kidogo.....na mimi nitaongezea kidogo hapo mkuu maana leo umeongea la maana,
Gambling haisemi hivyo
Kununua wachezaji inabaki kuwa kamari milele
Mifano hizi hapa
- Eden Hazard alitoka Lile na alipokuja Chelsea aliishia kuwa Legend wa timu kwa ubora wake
- Pepe - japo hatuwezi kumhukumu kwa sababu ni mapema mno lakini dalili za mvua ni mawingu, Pepe kashindwa kabisa kuonyesha ule ubora wake wa magoli 22 kwa msimu akiwa Lile
- Morata - alishindwa kutamba Chelsea sasa anatamba Laliga
- Cuadrado - alishindwa kutamba Chelsea sasa anatamba Serie A
- Diego Forlan - alishindwa kutamba Man U na akatamba Laliga na Vilareal na pia mchezaji bora wa kombe la dunia 2010
- Gerard Pique - alishindwa kutamba Man U chini ya Furguson na alipojiunga na Barcelona akatamba mpaka wa leo
- Radamel Falcao - alishindwa kutamba Chelsea ametamba Ligue one
- Angel Di Maria - alitamba na Real Madrid, alishindwa kutamba Man U na alipojiunga na PSG anatamba mpaka wa leo
- Jerome Boateng - alishindwa kutamba Man City alipojiunga na Beyern Munich akatamba huko
- Paulinho - alishindwa kutamba Spurs akaenda kutamba Barcelona Laliga
- Deco alishindwa kuonyesha ubora wake Chelsea
- Michael Owne alishindwa kuonyesha makali ya EPL alipohamia RM - Laliga mpaka ikamlazimu kurudi EPL baada ya msimu mmoja tu
- Cesc Fabregas alitamba sana EPL akiwa Arsenal lakini alipohamia laliga alifeli mpaka alipoamua kurudi EPL kuchezea Chelsea na ubora wake kama alivyokuwa Arsenal ukarudi tena
kiwango cha mchezaji kinaweza kuathiriwa na mazingira anayoyakuta ukicompare na alipotoka,maana kuna wachezaji wanaweza kucopy mazingira haraka na mwengine akashindwa.....
Katika mazingira kuna mambo mengi...
Mifumo ya kocha - Ozil alishindwa kucheza madrid,na sasa hivi Arsenal sababu ya kimfumo na hapa ndio utakuta wachezaji wengi wazuri wanapotezwa maana mara nyingi inapelekea mchezaji kucheza out of positions mf.Ox,Xhaka,Torrela
Aina ya wachezaji-kama ulimuona Pogba wa Juve basi utakubaliana na mimi,alipiga mwingi sana ukimcompare na huyu wa Manyumbu mpaka wakawa wanaulizana au tumeuziwa copy yake....sababu hapo Nyumbu anakosa watu aina ya kina Artulo Vidal,Pjanic na Pirlo....aiseeh Pogba yule hajawahi kurudi
Ugumu wa ligi-hili lipo dhahiri na linahitaji mchezaji kuwa mvumilivu ili aweze kukabiliana na hali halisi,maana huku kuna top6 lakini bado ukikutana na timu ya 17 kwenye msimamo shughuli unayo...pia makombe ni mengi sana hasa ukicheza hizi timu kubwa unajikuta una EPL,FA,CALABAO,UEFA/EUROPA then wikiend unakutana na kitimu kinashiriki EPL tu hapo utakamiwa mpaka ukome...
Kinachowamaliza wachezaji ni kelele za mashabiki hasa hizi timu kubwa zenye presha...ambapo mchezaji mara nyingi anaponzwa na ada yake ya usajili,maana watu wanataka kuona matokeo makubwa kwa muda mfupi sana ili wajiaminishe kuwa hawajapigwa...
Sasa mchezaji akikutana na mambo hayo hapo juu,itabidi avumiliwe na shabiki subra hana kabisaaaaaaaaaaa ...sasa ndio ukutane na mchezaji aliyenunuliwa kwa pesa ndogo anaperfom kuliko wewe hahahaaaa utaitwa kila aina ya jina na ndio hapa saikolojia ya mchezaji inapoharibika
