Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Sisi mashabiki tuna tabia za ajabu sana yan huwa hatueleweki linapokuja suala la wachezaji wetu. Leo tutamsifia kesho tutamponda na pia tutasahau aliyofanya nyuma. Mfano, Willian katika mechi za mwanzo msimu huu hasa aliporejea kutoka maheruhi watu walimponda balaa mpaka kuna wengine wakaandaa list ya wachezaji wa kuuzwa Chelsea na jina lake likawemo lakini ndan ya mechi mbili za mwisho kabla ya hii ya Grimsby amesifiwa balaa sasa unaanza kujiuliza siyo hawa waliokuwa wanamponda.

Haya issue nyingine ni huyu dogo Odoi leo hii kuna watu wanasema hamna kitu pale kikuweli mimi nawashangaa sana hasa kwa huyu dogo. Hebu rudini mkaangalie zile clip za msimu uliopita mjiridhishe tena ndio mje na izo negative comments zenu. Ukiachana na media za EPL kum hype tukija kwa mitazamo yetu kimpira yan hamuoni chochote kwa huyu dogo wa miaka 18? Ooh the world is difficult for the blind. Huyu dogo ana zaidi ya miezi hagusi mpira msitegemee arudi uwanjani aanze kuonyesha mambo yake halafu bado ni mdogo ndio anajifunza katika umri wake ni kazi kufikia kiwango cha Sancho au Mbappe. Tuache upofu tumuangalie mbele zaidi siyo sasa dogo anajua.View attachment 1217788
Mkuu wanaombeza Odoi si Chelsea fan. Mimi nilichocomment tu ni mshahara wake hauebndani na brand yake ya sasa. Alitakiwa angalau aanze na laki moja, hii ya laki 180,000 halafu kuna uwezekano mkubwa asitumike sana ni ubadhirifu wa pesa na kuwakatisha tamaa wenzake kama akina Tomori, Reece, na Mount plus hao academy wengine ambao wanacheza vizuri kuliko yeye.

Kuhusu mashabiki kugeuka kugeuka ndio ushabiki wenyewe. Mchezaji anasifiwa na kutiwa moyo anapocheza vizuri akitibua anasakamwa ili aondoke au arudi kwenye form. Mimi ni mmojawapo wa mashabiki ambaye naweza kumsifia asubuhi akicheza vizuri na kumponda jioni akiboronga. Ushabiki umebeba sehemu kubwa ya afya zetu. Pressure ya nini
Willian kwa mfano na Alonso wakati wa Sari waliboronga sana. Lakini kwa huu mfumo wa Lampard na pia kwa pressure ya Lampard naona Alonso na Willian wamerudi kwenye form yao nzuri.
So mkuu wala isikupe shida, hata wewe kesho Odoi akiboronga utakuwa wa kwanza kumponda na kumtaka kocha amweke benchi. Kwa umri wake tumuombee acheze vizuri na form yake izidi kuimarika kwa sababu anazo talents nzuri ambazo Chelsea itazihitaji sana
 
Odoi, loftus cheek hawa ni wachezaji wakuingia sub. Odoi na cheek ni wachezaji wazuri timu ikiwa inashambulia, ila timu ikizidiwa hawa jamaa wavivu kukaba aisee.

Haswa odoi akipiga vyanga vyake akanyang'anywa mpira hakabagi anasimama.

Kiufupi ni wachezaji wazuri timu ikiwa inashambulia mara kwa mara.

Kama mawazo yangu kwenye big match its better watokee benchi. Kwa match ndogo waanze 1st eleven wazidi kuimarika zaidi na zaidi.
Umeongea, Odoi hajafikia level ya kumuanzisha kwenye big matches, sio kwa sababu sio mzuri ila kwa sababu tuna option nzuri nyingi zaidi, ila pia Pulisic hawezi mweka benchi Odoi kwa sasa labda akiisha zoea EPL. pia Odoi hawezi mweka benchi Willian au Mount, form ya Willian sasa hivi iko mahali pake. Kwa possibility kubwa Odoi atakuwa sub kwenye mechi nyingi za EPL. Labda zile za Carabao na FA. Akirudi RLC ushindani ndio unakuwa mkubwa Zaidi. Na shida ya Lampard sasa hivi kule kwenye attacking ni nani amuweke na nani amuwache
 
Odoi, loftus cheek hawa ni wachezaji wakuingia sub. Odoi na cheek ni wachezaji wazuri timu ikiwa inashambulia, ila timu ikizidiwa hawa jamaa wavivu kukaba aisee.

Haswa odoi akipiga vyanga vyake akanyang'anywa mpira hakabagi anasimama.

Kiufupi ni wachezaji wazuri timu ikiwa inashambulia mara kwa mara.

Kama mawazo yangu kwenye big match its better watokee benchi. Kwa match ndogo waanze 1st eleven wazidi kuimarika zaidi na zaidi.
RLC ondoa weka Barkley. Huyo dogo anaona goli kuliko Barkley
 
Mkuu wanaombeza Odoi si Chelsea fan. Mimi nilichocomment tu ni mshahara wake hauebndani na brand yake ya sasa. Alitakiwa angalau aanze na laki moja, hii ya laki 180,000 halafu kuna uwezekano mkubwa asitumike sana ni ubadhirifu wa pesa na kuwakatisha tamaa wenzake kama akina Tomori, Reece, na Mount plus hao academy wengine ambao wanacheza vizuri kuliko yeye.

Kuhusu mashabiki kugeuka kugeuka ndio ushabiki wenyewe. Mchezaji anasifiwa na kutiwa moyo anapocheza vizuri akitibua anasakamwa ili aondoke au arudi kwenye form. Mimi ni mmojawapo wa mashabiki ambaye naweza kumsifia asubuhi akicheza vizuri na kumponda jioni akiboronga. Ushabiki umebeba sehemu kubwa ya afya zetu. Pressure ya nini
Willian kwa mfano na Alonso wakati wa Sari waliboronga sana. Lakini kwa huu mfumo wa Lampard na pia kwa pressure ya Lampard naona Alonso na Willian wamerudi kwenye form yao nzuri.
So mkuu wala isikupe shida, hata wewe kesho Odoi akiboronga utakuwa wa kwanza kumponda na kumtaka kocha amweke benchi. Kwa umri wake tumuombee acheze vizuri na form yake izidi kuimarika kwa sababu anazo talents nzuri ambazo Chelsea itazihitaji sana
Ninachoongelea mimi anapondwa kwa kuangalia mechi moja. Kijana wa miaka 18 ambaye bado anachipukia tunategemea awe na consistence ya kiwango tena katoka majeruhi hajacheza kwa miezi 4.?

Swala la mshahara nadhani ni target na timu yenyewe kumfanya asishawishike na deals toka timu nyingine. Though kweli kwa umri wake na kiwango chake ni mshahara mkubwa ili hii itakuja kusaidia miaka mitatu ijayo pale dogo atakapokuwa ameiva kweli kweli kama sasa ivi Sancho. Pale Dortmund anakula £210,000.
 
My predicted lne up

4-3-3 Lazima tushambulie

Mount-Tammy-Willian

Kovacic-Jorginho-Kante

Alonso-Tomori-Christensen-Azpilicueta(C)

Kepa
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Alonso anapiga cross matata ila muda mwingine shabiki unabaki unang'ata kidole pale anapoamua kurudisha pasi nyuma.

Muda ambao unadhani anapiga cross ndio muda anaosimama na kurudisha pasi nyuma, muda ambao hutegemei anamwaga maji ndio anamwaga maji.

Ananifurahishaga huwa akishika mpira siweki matarajio kichwani atafanyaje huwa namwangalia tuu hahahahahaha
 
Lampard ukicheza vibaya, game inayofuata hata benchi unaweza ukakosa, ndio maana akina Willian wanajitahidi tofauti na wakati wa Sarri ahta kama akicheza vibaya the next game ana uhakika wa namba
 
Ningekuwa mimi Lampard Barkley ni wa kumpumzisha kabla ya dk ya 60 aingie Kovacic
Pia Christensen angepumzishwa asije akatupa red card nafasi yake aingie hata Reece anaweza kucheza CB
Pedro pia apumzike aingie Odoi. Pedro anacheza vizuri ila tumjaribu Odoi yeye ni mwepesi
Anayefanya Brighton wacheze cheze ni Barkley kwa kupoteza poteza mipira hovyo, too slow na hayuko uwanjani sijui yuko wapi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom