Nilishawahi kujiuliza pia kwanini Alonso na Jorgninho wakiwa kwenye poor form walikuwa wakicheza kila mechi wakati Emerson yuko bench na Kante akicheza nafasi ambayo haikuwa na impact sana kwenye timu. Jorginho akiwa kwenye form ni mzuri sana, akiwa off ni mbaya sana kwa sababu ya role yake ni vital. Kila kocha huwa anajenga Imani na mahaba kwa mchezaji akitarajia atarudi kwenye formu huku form yake mbaya ikiendelea kuiumiza timu. Nilishawahi kusema hivyo kwa Luiz. Conte alimgundua akamfanya suplus, Sarri akaja akajenga Imani kubwa kwake kama alivyofanya kwa Alonso na Jorgninho ambapo mistakes zao ziliigharimu timu. halafu Lampard kwenye pre season akamgundua akamfanya suplus akachukia akahama timu.
Wewe ulishawahi kujiuliza pamoja na Luiz kutokuwepo ni kwa nini Chelsea bado inafungwa kirahisi, utakimbilia defense. Mimi nasema no. Attack huwa inatengenezwa na kuanzishwa katikati. Jorgninho ndie wa aidha kuiponya timu au kuiuwa. Mashambulizi yakishatengenezwa katikati na washambuliaji makini wakashusha mvua golini hata beki mzuri kama VVD hawataweza kuzuia goli lisifungwe. Na mashambulizi ya kijinga kama hayo ndizo zinazoforce mabeki kufanya mistakes halafu wanalaumiwa wao wakati walioruhusu mashambulizi ni Midfields. Na ndio maan Kante akiwa Lestercity na baadaye Chelsea alihakikisha anakata umeme na mawasiliano ili mabeki wacheze kwa uhuru. Hii kwa Jorgninho haipo, mabeki wanacheza under pressure na kufanya silly mistakes kwa sababu adui anakuja anavyotaka. Na ndio maana wataalamu wengi wanamtaka Kante arudi katikati. Uzuri wa Jo ni passing za haraka haraka, kwenye kucreate chances anajaribu ila bado, Kovacic is much better to that area than Jo
Conclusion
Kante wakicheza na Kovacic au Jo katikati ni much better kuliko kumtegemea tu Jo au Kova.
Wazo langu la kurotate ilikuwa ni ili wapate muda wa kupumzika na kuregain energy maana wote ni wazuri pamoja na shortcoming ndogo ndogo za kila mmoja