Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

Lampard ameusifia uamuzi wa Pulisic kukatiza likizo yake na familia na kujiunga na timu inayokwenda Japan kwa pre-season. Lampard kadai ingekuwa enzi yake angefanya hivyo hivyo.
Hii inaonyesha mentality nzuri ya kujali timu, kujali mazoezi na kuacha mengine kwa ajili ya timu
HONGERA PULISIC
 
Frank Lampard admits he was impressed with Michy Batshuayi and Tammy Abraham after Dublin pre season match against St Patrick’s
 
Ila kiukweli katikati tumekaa sawa, Kante, Joginho, Loftus Cheek, Kovacic, Barley, na Mount Moson ataanza kupigania first team choice. Mbele ndo bado hapajaeleweka hasa striker
Yeah mason mount yuko vizur sana
Kuna yule tomori nae naona yuko poa

Abraham n batshuay jana walikuwa wachoyo kila mmoja anataka kufunga ili aonekane
 
Wasipoangalia, mzee mzima OG atawapiku namba
Namba ya Giroud iko given, kati ya Tammy na Batshuaiy sioni wa kumbench Giroud. Baada ya misimu Tammy labda. Batshuaiy ana kitu cha kuproove msimu huu. Japo kwa Chelsea tuliyonayo nafikiri Lampard atatumia sana 4 1 3 2. Kwa mfumo huo Batshuaiy atapasa muda wa kucheza
 
Ila kiukweli katikati tumekaa sawa, Kante, Joginho, Loftus Cheek, Kovacic, Barley, na Mount Moson ataanza kupigania first team choice. Mbele ndo bado hapajaeleweka hasa striker
kweli pale kwa striker bado na sijui tutafanyaje na huku tumepigwa burn ya kusajili
 
Kuna watu wana wivu na Chelsea, waliisha shangilia kwa kupigwa BAN na kuondoka kwa Hazard na sasa wanasubiri Chelsea iangukie pua
Wengi wa hao wanatoka
  1. Liverpool
  2. Man U na
  3. Arsenal

Washabiki wa Chelsea bhana! Kwani nyinyi munaipenda Liverpool, Arsenal na Man U?

Yani munajikweza kama kwamba muna bonge la timu!

Hata Man U wanasema Liverpool, Chelsea na Arsenal wanachuki na timu yao.

Arsenal pia wanasema Liverpool, Chelsea na Man U wanachuki na timu yao.

Liverpool pia wanasema Chelsea, Arsenal na Man U wanachuki na Timu yao.

Sasa wewe unaposema Timu yenu pekee ndiyo inayochukiwa sijui umekusudia kuprove kitu gani?

Hakuna Timu moja inayompenda mwengine acha kujikweza na kajitimu kenu kalichoanzoshwa 2004.
 
Ila kiukweli katikati tumekaa sawa, Kante, Joginho, Loftus Cheek, Kovacic, Barley, na Mount Moson ataanza kupigania first team choice. Mbele ndo bado hapajaeleweka hasa striker
Ross Barkley amegeukia kuwa garasa hapo Chelsea
 
Ila ukimweka Man U lazima atinge first eleven

Barkley amweke nani benchi pale?

Midfield ya Man U ni Pogba-Matic-McTominay

Barkley kwa kiwango alichoonesha hapo Chelsea hawezi mweka benchi Scott McTominay
 
Barkley amweke nani benchi pale?

Midfield ya Man U ni Pogba-Matic-McTominay

Barkley kwa kiwango alichoonesha hapo Chelsea hawezi mweka benchi Scott McTominay
Hivi ni hao hao akina Pogba-Matic walioiweka Man Unite no. 6 msimu uliopita au ni wengine?
 
Sio pekee yao ila walikuwemo!!
Kuwa namba sita sio kigezo cha kusema kuwa MUFC haina viungo wazuri, huyo Barkley msugua benchi hapo na bonge la garasa hawezi pata namba mbele ya Scott
 
Kuwa namba sita sio kigezo cha kusema kuwa MUFC haina viungo wazuri, huyo Barkley msugua benchi hapo na bonge la garasa hawezi pata namba mbele ya Scott
Pogba sio professional ni msanii tu, afadhali ya Barkley ana nidhamu na anajituma, room for growth are open for him but for Pogba, hapo mpira unaishia
 
Pogba sio professional ni msanii tu, afadhali ya Barkley ana nidhamu na anajituma, room for growth are open for him but for Pogba, hapo mpira unaishia
Sasa Pogba umlimganishe na Barkley? Pogba midfield pale Juventus alikuwa anakupigia goli tisa za ligi wakati midfielder tu, anaweza kuchezesha timu, Mzee wa miassist msimu huu kacheza bila morale ila ana assist tisa za EPL pale Old Traford sasa unaanzaje kumfananisha na garasa la kiingereza Ross Barkley?

Ushabiki fulani wa kulinda mtu kisa ni anatokea Club unayoshabikia sio kabisa mkuu,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom