woodpacker
New Member
- Apr 21, 2011
- 1
- 0
Jioni ya leo tumeona Ferdnando Torres alivyoweza pata goli lake la kwanza toka ajiunge na club yake mpya ya Chelsea.Tumeweza kuona jinsi mashabiki pamoja na Kocha wao walivyo mshangilia mithili ya gamba jipya la sisi em linavyoshangiliwa na wanachama wake kwa kufanikisha kulivua gamba walilshindwa kulivua kwa mda mrefu na hatimaye wamefanikiwa kulivua.Uwanja mzima ulilipuka kwa furaha, wachezaji wote walimrukia Torres utadhani lile goli lilikuwa lina wapa ubingwa Chelsea.Swali ni kwamba, je kulivua gamba la kuto funga magoli kwa Torres kunatoa matarajio gani? Au kajivua gamba wakati sumu bado ileile nikimaanisha ukame wa magoli kuendelea? Atafanikisha kuleta taji tajiri na mashabiki walivyo kuwa wakitarajia?