Leo Babu Sari anatakiwa aje kivingine, 1st ELEVEN Kepa, Zappacosta, Rudger, David Luiz, Emarson, Ngolo kante, Backely, Joginho, Pedro, Hazard, Giroud. SUB Willan, Alonso, Azipiculeta, Kovacic, Fabrigas, Lotus Cheek
kwa kweli kwa sasa Alonso uchovu, hana kasi, Azipiculeta jembe letu limetumika muda mrefu sana na lenyewe linatakiwa lipumzike lirudishe makali ya kupanda kwa kasi na kumwaga maji, Willan huu ni mzigo style yake ya uchezaji wa kupooza kasi na kutaka kuwatoka mabeki kwa chenga umekuwa ukitucost sana. pedro nampenda ana kasi sana once anapata mpira ananyooka golini hana muda wa kuremba na kuupaka mpira rangi.
Siku zote nimekuwa nikikasirika pale Kovacic anapoanza 1st eleven huyu jamaa anachezea sana mpira lakini ni mzito sana kwenye kukaba pale anapopoteza mpira na anakata moto mapema sio chuma kama Backely. Backely anakaba na anapanda kushambulia anapumzi sana, Ross na Kante wakicheza pamoja mipira haipotei hovyo
hazard leo aache kuzunguruka na mpira, hazard yule wa kupata mpira na kuingia kwenye box kwa speed kali amepotea, sasa hivi tunaye hazard anayeingia na kutoka kuzunguka na kurudisha pasi nyuma.
kuhusu pale mbele forward Mungu ndiye anajua, bora giroud akaanza match ya leo at least ana makeke ya kosa kosa kule yule mrembo Morata.
Blue forever