
*Dondoo za international break*
*timu ya wakubwa iliyoitwa*
*

Kepa,Azpilicueta,Morata,Alonso*
*

Emerson,Jorginho*
*

Kante,Giroud*
*

Christensen*
*

Rudiger*
*🇽🇼Ampadu*
*

Kovacic*
*

Barkley*
*

Hazard*
*walioko kwa mkopo klabu mbalimbali na wameitwa*
```

Aina

Omeruo

Miazga

Zouma

Hector

Pasalic

Angban

Mount

Batshuayi```
*ambao hawajaitwa kutoka timu ya juu*
```Caballero, Green, Zappacosta, Luiz, Cahill, Fabregas, Drinkwater, Loftus-Cheek, Pedro, Willian, Moses, Piazon```
*Ambao wameitwa kutoka timu za vijana*
```Poland U20 : Bułka
Scotland U21 : Gilmour
Netherlands U19 : Castillo, Redan
England U21 : Clarke-Salter, Tomori, Abraham
U20 : James, Dasilva, Chalobah
U19 : Guehi, Lamptey, Gallagher, McEachran, Hudson-Odoi
U18: Anjorin
U17 : Livramento
Serbia U21 : Pantic
```
*

Fabregas "nikiwa kocha nitaiga Sarriball"*
```"nimekuwa hapa kwa wiki 2 tu,baada ya kuwa nje kwa wiki 7 au 8 hivi,najisikia vizuri sana na siku waza kama nitapata tena furaha klabuni hapa na kujisikia vizuri..
Kwa njia anayotumia Sarri na mpira unavyo onekana nimependa labda baadae nikiwa kocha basi na mimi nitaenda sambamba na anavyofanya Sarri ni kitu nachopenda na kukiona pia..."
```
*

Fabregas anaingoja Chelsea*
```fabregas anaisubiri Chelsea impe mkataba mpya,anasema
"nimebakiza miezi 8 hapa,ningependa kubaki hapa,nimekuwa hapa kwa furaha miaka minne na nusu,najisikia bado nina mpira umebaki ndani yangu,bado nimebaki nao,hivyo naiachia klabu kuamua"```
*

Sarri nimeshangazwa na wachezaji wa Chelsea*
```"Nimeshangazwa,nina bahati sana kuwa na wachezaji bora na tuna bahati pia kuwa na matokeo chanya ni kutokana na wachezaji wazuri,ni kweli ni tofauti na msimu uliopita lakini hii timu ia wachezaji wazuri kuendana na mtindo wangu wa uchezaji"```
*

Eden Hazard akoshwa na Kepa*
```"Kepa ni kijana mdogo na golikipa mzuri,pale unapomleta mtu kama huyu kwenye timu,ni vizuri sana kwa kweli,tulimpoteza golikipa bora duniani,lakini timu ni bora zaidi msimu huu kuliko msimu uliopita na tunaliona hilo kila wikiendi"```

*Mazoezi ya Sarri yamkera Willian*
```kipindi cha Conte wachezaji pale mechi inapokaribia walikuwa wanaambiwa wakae kwenye hotel karibu na Stamford ili kupiga tizi la maana,lakini Sarri anawaruhusu wachezaji watoke nyumbani sababu ana amini ni wachezaji wa kimataifa na hawapangii vitu vya kula wala kunywa, embu tumuone willian amekereka nini, anasema
"kwa kweli siyapendi mazoezi ya Sarri ya jioni,huwa napenda kufanya asubuhi,kwa sababu baada ya hapo tunaweza kukaa na familia zetu,nikiwa mazoezini jioni, watoti wangu wanarudi nyumbani, na nikifika nyumbani nakuta wameshakula na wamelala hivyo nawaona mara chache sana,ndo maana sipendi mazoezi jioni ..."
sasa. willian ukifika hata saa nane usiku hamsha watoto Wasalimie ukichoka waache walale ....```
*

Sarri ni baba yake Jorginho***
```"...kwenye vyumba vya kubadilishia nguo huwa tunamwita Sarri baba yake Jorginho kwani wanacheka wanaongea pamoja,naelewa kwa nini,kwa sababu Jorginho amefanya maisha kuwa mepesi kwetu,anakupa mpira sahihi katika wakati sahihi..." alisema Hazard
```
*

.Hazard amsifu Kante*
```"...Kante amewapa kombe la dunia ufaransa ,miaka miwili iliyopita alisaidia Chelsea kuchukua EPL na pia alisaidia Leicester kuchukua EPL ni mchezaji mzuri sana anasimamia vizuro idara ya kiungo,na ni mtu mzuri pia nje ya uwanja ..."```
*

"Tunamuhitaji Loftus Cheek"*
```"Tunamkubali sana" hiyo ni kauli ya kocha wa Crystal Palace ,Roy Hudgson akisema wangependa Loftus ajiunge na klabu yao kama Chelsea itapenda kumtoa kwa mkopo januari```
*

Chelsea anaweza kuwa bingwa*
```Hiyo ni kauli ya kocha wa Southampton ambaye kesho anacheza na Chelsea mida ya saa 10:15 jioni kwa saa za hapa bongo amesema
"...Chelsea wanaweza kuchukua ubingwa na tunahitaji bahati kuwa upande wetu kushinda mchezo huo..."```
_endeleeni kumsapoti Mr darajani katika kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii kama_ *Instagram,Twitter,Facebook* _kwa habari ya za Chelsea hata Nondo zangu pia atazipost yeye huko ili kufikia_ _jamii kubwa ya Wanadarajani_
_
```follow``` *@Darajani1905* _mimi tayari wewe unasubiri nini_
...



*Caleb Azpilicueta*